Hatimaye chadema yaipindua ccm arumeru

kifuniboy

Senior Member
Nov 25, 2010
191
17
Chama cha Democrasia na Maendeleo kimefanikiwa kutwaa ushindi wa jimbo la Arumeru ambalo
kwa mda mrefu limekuwa ni ngome ya CCM,Kuna tetesi kuwa kumekuwa na wizi wa kura
wa wazi wazi uliokuwa ukifanywa na CCM lakini bado CHADEMA wameshinda kwa kishindo
kikubwa cha zaidi ya kura 6000.Nafikiri huu ni wakati wa waTanzania wote kutafakari kuhusu
hatma ya nchi yao kwani siyo kila kanda wana muamko wa mageuzi ili kuweza kuweka chama
chochote cha upinzani madarakani ni lazima kujiandikisha na kupiga kura na siyo tuu kubaki
kulalamikia serikali iliyopo madarakani wakati hamna nia ya kuweka serikali mnayofikiri mnaitaka.
 
Ubabaishaji na kujiamini kwa ccm kutawaponza huo ni mwanzo tu,mbona zambia waliweza,watanzania tunatakiwa tubadilike.
 
Dunia sasa inabadilika sana na viongozi wabaya an vibaraka wao hawatakiwi kupewa nafasi. Mabadiliko ni lazima yalianza Misri, Yemen, Libya, Tunisia, Syria, Kenya bado Tanzania na Uganda. Tunahitajia viozi wakweli waadilifu wachamungu wa kweli watakaotengeneza ajira kwa vijana, unafuu wa maisha na kuhakikisha kuwa rasilimali zinatunzwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho
 
It is the matter of time, CCM will soon be playing a role of opposition. It does not matter how long gonna take.
 
Ni kweli watanzania tunapaswaa kutoka kwenye mkakati wa kulalamika na kuanza kuchukua hatua. tatizo watz wa Mkoa wa Dar es Salaam wanatuangusha katika juhudi hizi. Hawaonyeshi dalili za mapambazuko, sijui ni kwasababu Magogoni ipo mkoani kwao au tatizo ninini hasa?
 
Mwalimu aliwaasa ccm kuwa wakikumbatia viongozi wabovu watalia kilio ambacho watamkosa wa kuwafuta machozi, candiDATE WA CCM ANAKAA KAWE, YULE KANDIDETI WA CCM ANAYEITWA KAAYA ALIPIGWA CHINI KIMIZENGWE SASA UNATEGEMEA NINI, HUU NI USHUNDI WA HAKI KWAMBA HATA VITISHO NA NGUVU ZA FEDHA HAVIWEZI KUWABABAISHA WATU
 
It is the matter of time, CCM will soon be playing a role of opposition. It does not matter how long gonna take.

Nadhan Watakapokuwa Wapinzani Hawatalast for More than 5 years!! They will diminish to the earth surface soon after their failure!! Sijui akina Lusinde Wataweka wapi sura Zao with a standard 7 /8 (1980 - 1987) qualification with professional qualification ya Matusi!!
 
Back
Top Bottom