Elections 2010 Hatimaye CHADEMA wapewa kibali cha kufanya mkutano Arusha

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,619
4,292
Lile dukuduku la chadema kuzuiwa kufanya mkutano leo Arusha wamesharuhusiwa! Ndesamburo/Lema/Mbowe ndani ya uwanja leo:peace::whoo:WAO WANAPESA SISI TUNA MUNGU!
 
Wao wana pesa sisi tuna mungu.

Naipenda

peoplesssssssss powerrrrrrrrrrrrrr
 
Lile dukuduku la chadema kuzuiwa kufanya mkutano leo Arusha wamesharuhusiwa! Ndesamburo/Lema/Mbowe ndani ya uwanja leo:peace::whoo:WAO WANAPESA SISI TUNA MUNGU!

cool kama kuna mdau yeyote huko asogee aturushie yanayojiri
 
Kwa hiyo zile taarifa za "kiintelijensia" zilizowafanya polisi wazuie mkutano zimeyeyuka??
 
hii umeitoa wapi wakati uwanja wa mkutano wa nmc umezingirwa na ffu na mabomu na farasi? hali ni mbaya arusha kwani polisi hawataki mkutano na wananchi wamefunga kazi zao tayari kupambana na polisi na wengine wameamua kukodi magari toka moshi kuongeza nguvu,polisi wa wilaya za arusha wameitwa kuongeza nguvu pia.
 
Kwangu tatizo nini hasa hawa CCM wana shida gani? Mkutano ni haki ya chama chochote sasa kwa nini wanawazuia Chadema?
 
hii umeitoa wapi wakati uwanja wa mkutano wa nmc umezingirwa na ffu na mabomu na farasi? hali ni mbaya arusha kwani polisi hawataki mkutano na wananchi wamefunga kazi zao tayari kupambana na polisi na wengine wameamua kukodi magari toka moshi kuongeza nguvu,polisi wa wilaya za arusha wameitwa kuongeza nguvu pia.

Nguvu ya UMMA siku zote ni mshindi tukatae huu ubeberu wa CCM kufanya wanachokitaka tutapambana nao mpka kieleweke!
 
na leo busara za polisi zisipotumika inawezekana hata vifo kutokea kwani maji wamenunuliwa kwa wingi tayari kukabiliana na mabomu. wananchi wanaona kama mbunge wao anadhalilishwa ndio maana wamepandwa sana jazba na sasa wamefurika ofisi za mbunge na wengine kandokando ya barabara tayari kwa kazi moja tuu UKOMBOZI.
 
Lile dukuduku la chadema kuzuiwa kufanya mkutano leo Arusha wamesharuhusiwa! Ndesamburo/Lema/Mbowe ndani ya uwanja leo:peace::whoo:WAO WANAPESA SISI TUNA MUNGU!
Mkuu niko eneo husika polisi wamefunga barabara na wako wengi sana kujianda kukabiliana na wanachadema..kuna polisi wali walikuwa wana fanya mazoezi yaani inachekesha...unauhakika na hizi taarifa ulizoleta
 
Thanks for information, ina maana wewe uko uwanjani?, lete taarifa ya kweli
 
kawaida haki hua inacheleweshwa tu na mara zote kucheleweshwa au kuminywa kwa haki ndio chanzo cha migogoro africa.....sehemu zote ambazo chadema walishinda haki ilicheleweshwa na migogoro ilitokea na mpaka sasa imefikia kuwagawa watz kwa itikadi mbalimbali .a kwa ccm kuleta mvurugano kwao ni mafanikio..................
 
Human Right is anything that no ONE can take from You, This is our Right.

Watanyong'onyea wenyewe;

watu toka Njiro,Ngurero,kisongo,Usa River, sanawari,Filips, Ngare na viunga vya Arusha ndiyo kwanaanza wanzidi kuingia Mjini kati.

Aisee, Arusha kama Mwanza.

peoples................Power:whoo:
 
Du..kwakweli mambo ya hapa mjini ni vituko vya ajabu!
Unaazima hadi polisi wa wilaya za jirani kukabiliana na mkutano tu wa wapenzi wa chama...shida kubwa ni nini?
Wapenzi wa CDM hawatakaa wapungue, zaidi sana wataongezeka, sasa kuzuia mikutano yao kutakuwa hadi lini?
Kuna suluhu inatakiwa itafutwe, na wala si kuzuia mikutano!
 
Lile dukuduku la chadema kuzuiwa kufanya mkutano leo Arusha wamesharuhusiwa! Ndesamburo/Lema/Mbowe ndani ya uwanja leo:peace::whoo:WAO WANAPESA SISI TUNA MUNGU!

WanaJF,

Wadau, hii dhana ya polisi kutoa kibali kwa chama cha siasa kufanya mkutano si sahihi.Vibali vinaombwa na watu binafsi, au vikundi vyengine ila sio, vyama vya siasa.

Vyama vya siasa vinapaswa kuwataarifu polisi,ili polisi watoe ulinzi,wahakikishe hali ya usalama inakuwepo katika mikutano.

Hili la polisi kusema inazuia mikutano ya vyama vya siasa. Au inatoa kibali ni kutokujuwa kazi yao. Au kutumika kisiasa.

Ninashangaa na ninaudhika sana kwa huyu Bw.Tendwa ambaye anatakiwa kusimamia sheria hii, kukaa kimya kama vile hayamhusu. Sisi pia kama wananchi bado hatuelewi haki hii ya chama cha siasa.

Chama cha siasa hakitakiwi kuomba kibali cha kufanya mkutano, kinatakiwa kutoa taarifa ili Polisi watoe ulinzi.

Polisi wanatuchanganya na sisi wenyewe tunajichanganya na kuchanganyikiwa.

Tufute dhana hii potofu ya "kibali cha polisi" kwa mkutano wa chama cha siasa vichwani mwetu. Na tumtake Tendwa aende public, tena sio mara moja tu, kukemea uharamia huu wa polisi wanaofanya kazi kama tawi la CCM.
 
WanaJF,

Wadau, hii dhana ya polisi kutoa kibali kwa chama cha siasa kufanya mkutano si sahihi.Vibali vinaombwa na watu binafsi, au vikundi vyengine ila sio, vyama vya siasa.

Vyama vya siasa vinapaswa kuwataarifu polisi,ili polisi watoe ulinzi,wahakikishe hali ya usalama inakuwepo katika mikutano.

Hili la polisi kusema inazuia mikutano ya vyama vya siasa. Au inatoa kibali ni kutokujuwa kazi yao. Au kutumika kisiasa.

Ninashangaa na ninaudhika sana kwa huyu Bw.Tendwa ambaye anatakiwa kusimamia sheria hii, kukaa kimyakama vile hayamhusu. Sisi pia kama wananchi bado hatuelewi haki hii ya chama cha siasa.

Chama cha siasa hakitakiwi kuomba kibali cha kufanya mkutano, kinatakiwa kutoa taarifa ili Polisi watoe ulinzi.

Polisi wanatuchanganya na sisi wenyewe tunajichanganya na kuchanganyikiwa.

Tufute dhana hii potofu ya "kibali cha polisi" kwa mkutano wa chama cha siasa vichwani mwetu. Na tumtake Tendwa aende public, tena sio mara moja tu, kukemea uharamia huu wa polisi wanaofanya kazi kama tawi la CCM.

Mkuu umenena ukweli mtu.
 
tuombe mungu isje mwagika damu huko Arusha. Wana JF walioko huko tupeni up date.
 
Back
Top Bottom