Hatimaye CCM yatimiza ahadi; Bajaji za Wagonjwa zapokelewa rasmi

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Mpango wa Serikali iliyouanzisha wa ununuzi wa Pikipiki za kubebea wagonjwa ili kuzuia vifo vya wakinamama na watoto katika maeneo ya vijijini. Serikali inakusdia kununua Pikipiki 400 ambazo zitasambazwa maeneo mbalimbali hapa nchini.

Pikipiki maalum iliyotengezwa na Kampuni ya E Ranger ya Afrika Kusini kwa ajili ya shughuli za kubebea wagonjwa ili kudhibiti vifo vya mama na watoto. Pikipiki hizo kila moja imegharimu Dola za Kimarekani 5,900.
 
Ukisikia vichekesho ndo hivyo!!! Kwa barabara zipi haswa??? Hizi za vijijini ninazozijua mimi au???
 
Mbona kama wanaozipokea wamevaa njano kama ccm,haya bwana nadhani kikwete kaenda pabaya na am sure wanaharakati wa haki za binadamu tutazikataa ,huwezi kumbeba ktk machela mjamzito ni matusi ,yani ni heri ya bajaj
 
kuna watu wanaplan kuiba hela zetu kwa ujanja ujanja kila siku, hawapendi kutatua matatizo permanently ili waweze kutuibia.nonsense
 
mmh!dola 6000 kwa hicho kipikipiki kimoja,nanusa harufu ya ufisadi au ndo mambo ya zabuni??bajaji 400 si zinaishia mbagala tu,kuna wanawake wangapi wanapata ujauzito..wao wanatembelea mavx
 
Inabidi watu wachunguze nani ana hisa katika kiwanda cha pikipiki hizo - au huo mkataba wa kuzileta utakuwa vipi. Tusisahau, kwa mfano, hata speed Governer haukuwa mradi wa kusaidia usalama, bali chakula ya watu.
 
hicho kitakataka kitafika loliondo kwa babu kweli...?
 
Serikali yake kwa kukurupuka haijambo? Nani ametoa wazo potofu kama hili? Wajanja tayari wamepata mlo.
 
ha? hivi kumbe zile kampeni za pikipiki ni za ukweli? Tumerogwa TZ live nawaambia kha?? am speechlless
 
Balance yake ikoje? Mgonjwa anakingwaje wakati wa hali ya mvua? Ajali za pikipiki zimeongezeka sana nchini, waendeshaji wa pikipiki hizi wamepata mafunzo gani?
 
mmh!dola 6000 kwa hicho kipikipiki kimoja,nanusa harufu ya ufisadi au ndo mambo ya zabuni??bajaji 400 si zinaishia mbagala tu,kuna wanawake wangapi wanapata ujauzito..wao wanatembelea mavx

Kama hii ni kweli, basi umbumbumbu wa sirikali hii umevuka mipaka. Na ole wao watuulie wake zetu kwa ajali. USELESS GOVERNEMENT
 
Piki piki za kubebea wagonjwa zimeanza kuwasili toka SA. Hili wakati JK akisema wakati wa kampeni nilidhani :blah: za siasa tu, kumbe amepania...hii ni hatari kwa wagonjwa:confused3:
 

Attachments

  • Piki piki ambulance.JPG
    Piki piki ambulance.JPG
    249.7 KB · Views: 154
ha? hivi kumbe zile kampeni za pikipiki ni za ukweli? Tumerogwa TZ live nawaambia kha?? am speechlless

Hahahaha ulizani Mzaha wa Mkuu wa Kaya.....kikao kilichopita ungeshuhudia wabunge wa CCM walivyotumia nguvu kuhalalisha uwezo wa bajaji hahahaha ni hatari tupu hakika utadhani wao huwa hawakwami na ma-VX yao sasa wanapeleka bajaj
 
ole wao watuulie wake zetu kwa ajali. USELESS GOVERNEMENT

Unabisha??wait and see......usijali speech za pole nyingi baada ya vifo zitatolewa na ubani juu. Kisha mradi baada ya miezi michache utakupa inaingia inshu nyingine
 
kweli tutaendelea kuwa wadanganyika milele, kwa hiyo wao watembelee vx za milioni 150 bibi zetu huko vijijini ndo watutuswe kwenye vumbi jua upepo na hatari namna hiyooooo dah dhihaka kubwa sana kwa wananchi nashangaa tunaendelea kumsujudia huyu jk
 
Haingi akilini kununua pikipiki kwa dola 6000 na ongeza gharama za usafiri,kwanini wasinunue ambulance zilizotumika kwa nusu wa hiyo bei ? nimeziona Dubai,Japan na Singapore,hapa akili haijatumika kabisa kwenye barabara za lami zinaweza tumika lakini vijijini na barabara mbovu mjamzito au mgonjwa mahututi ni kuwaumiza tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom