Mkuu wangu nisome vizuri. Nachoamini mimi sio lazima kifanyike nchini isipokuwa unatazama WATU na MAZINGIRA yaliyopo. Binafsi ningependa kuona utawala usiojali kabila, jinsia, wala dini lakini mnaambiwa kwa siasa za Tanzania hili haliwezekani na muhimu sana kutazama vitu hivi (Watu na Mazingira) kwa sababu ndivyo wananchi wote wanategemea kuona uuwiano ktk maswala yote ya kitaifa...Nilikuwa nakuona umeelimika lakini kwa sentensi hiyo nimekupuuza sana.
Sasa Kama Chadema wanaelewa hivyo, na hakika kutojali hali hiyo ndiko kumepelekea wao kuonekana chama cha Kidini na kikabila (mimi sioni) kwa nini bado wanaendelea na mfumo huu ambao unawapotezea umaarufu zaidi?.Na haya niliyajua baada ya kukutana na Kitila akanambia swala la Udini na Ukabila nchini ni very sensitive na Politically lazima kulitazama kwa makini sana tofauti na kuchagua mtu yeyote kulingana na uwezo wake wa kuongoza..
Kama Chadema wangekuwa chama tawala nadhani wangeweza kuunda mfumo wa kiutawala ambao hautazami dini, kabila, Utanganyika -Uzanzibar lakini hawawezi kufanya wanayoyafanya chini ya WATU wanaofiiria kwamba Udini na Ukabila upo ndani ya Chadema ktk utoaji ajira. Kwa hiyo usitazame sana maoni yangu kama yangu mimi, bali natazama WATU na MAZINGIRA waliyopo Chadema na kutoa hoja zangu.