Hatimaye Amin Bakhresa atemwa Rasmi kugombea DRFA

pilau

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
1,593
443
Lile sakata lililokuwa linawakera wapenda soka katika jiji la DSM la kamati ya Uchaguzi ya mkoa wa DSM iliyokuwa inaongozwa na Muhdin Ndolanga kulazimisha na kumbeba Amin Bakhresa bila kuzingatia vigezo ili awe mgombea wa uenyekiti wa soka mkoa wa DSM DRFA leo limefikia tamati baada ya Kamati ya Ligi TFF kumchinjia baharini na kuufuta mchakato mzima wa uchaguzi huo na kuwaamuru waanze upya mchakato huo. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi wa TFF Deogratias Lyato kutoa uamuzi huo mchana huu. pia kamati ya Ndolanga kufutwa na uongozi wa DRFA kuamriwa kuuteua kamati nyingine kabla ya tarehe 28/10 na uchaguzi Desemba 8 2012

chanzo
: vyombo vyote vya habati jioni hii
 
Afadhali yani alikuwa king'ang'anizi utadhani mpira wa DAR ES SALAAM ni mali ya familia yake kilaza mkubwa yule.
 
Back
Top Bottom