Chimunguru
JF-Expert Member
- May 3, 2009
- 10,680
- 4,345
Babu yangu alimkataza baba yangu asijiunge na polisi sababu kazi hiyo ina LAANA. sasa ndo naelewa laana iko wapi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Siyo kwamba hawajui kudanganya,hawaoni umuhimu wa kutumia sophisticated means kwasababu wanawadharau sana wananchi.Wanaona hakuna haja ya kutumia hizo efforts na wanauhakika litapita tu kwasbabu watanzania wengi wanasubiri hadi siku ya kiama ndo wauwaji waadhibiwe na mungu.
Kumbe ndo ujanja wa kukimbilia mahakamani siku hizi ili ku-silence watu wasiseme
UKITAKA KUJUA ATHARI ZA SINEMA ZA KIHINDI KURATIBIWA NA UONGOZI WA KI-CHINA BASI KAMUULIZE ALHAJI AFANDE SELE PALE 'MAMBO YA NDANI' NA JINSI GANI ALIVYOLITIA KOVU LA KUDUMU JESHI LA POLISI
Kwa akili tu ya kawaida, busara zinatuamrisha ya kwamba pindi tunapoinuia kutengeneza sinema ama yaa Kihindi, Kimang'ati au hata ya Kichina, ni vema tukawapa nafasi watu wenye ufahamu mzuri na tamaduni za mahali husika wakatusaidia kuratibu mambo.
Ajabu na kweli ni kwamba katika jaribio la kumchukua uhai Dk Ulimboka, majina ambayo yatokea kutajwatajwa yametokea kuwa ni wa upande fulani tu. Madai ya Uhalifu huo ni wao, Uchunguzi ni wao, Usemaji ni wao, na hata Uratibu mzima bado ni wao tu.
Hakika hili kidogo linatatiza kwa kuwa jeshi letu la polisi sote tunajua halina dini lakini kwa mwenendo huu wa mara Abeid wa Ikulu, Ahmed Msangi wa Kanda Maalum, Selemani Kova kubwa lao, Saed Mwema ambaye ndiye Back-stopper hapo -- mmmmmmhhhh!!!
Japo ni jambo ambalo halisemwi wazi wazi na wengi LAKINI mmmhhhhh!!! Kwa nini na kwani kuna nini??? Siku zote Matokeo ya mambo kama haya, pengine ni ajali tu imetokea hadi hapo, mwisho wa siku huleta taswira kama vile ya Picha ya KIHINDI kuratibiwa vile na WACHINA.
Mtu akiangalia ki-undani, pale kwenye ONYESHO LA PILI, jinsi gani ka-Gwajima (Mkristo) na Joshua (nalo jina la kikristo ila mbebaji wa jina hilo HATUNA UHAKIKA na dini yake mpaka atakapotuthibitishia kwa kinywa chake mwenyewe) wanavyovutwa kwa nguvu zote kuwa sehemu ya mchezo katika filamu hii - yote yanayojitokeza ni VITUKO VYA KARNE katika historia ya mambo ya kipolisi duniani kote.
Kwa watazamaji wapya wa picha hii ya 'KOVA KATIKA MABAWA YA MABADILIKO YA NGUVU YA UMMA NCHINI TANZANIA', kwa kukumbushia tu, ONYESHO LA KWANZA ilianzia pale Leaders' Club na kuishia Mabwepande Tegeta na walioonekana mwishoni mwa picha ile ni Mama Kijo Bishimba, Mzee Mwanakijiji, Mjeruhiwa Dk Ulimboka pamoja na wanakijiji katika yale mandhari asili ya MabwePande.
Sababu ya kusema hivyo ni kwamba Alhaji Afande Sele (Kanda Maalum Jijini Dar), kwa kosa moja tu la kutokufahamu desturi na taratibu za madhehebu ya ki-Kristo ki-ajali kabisa kajikuta AMEUNGUZA PICHA ZIMA kwa kudai kwamba mgeni wake Joshua Muyungi alienda na AKATUBU katika kanisa la Nabii Mkuu na Askofu Gwajima juu ya uhusika wake kwenye jaribio la kumua Dr Ulimboka. Hii ndio maana kila wanapojaribu kuunganisha picha hizo mbili hali inaendelea tu kuwa kama mafuta ya taa na maji kwenye maabara zetu za kibongo hizi.
Ukweli wa mambo ni kwamba mbali na Kanisa Katoliki ambako watu hujichagulia kwenda kwa Padre na kutubu dhambi zao, madhehebu mengine yote ya ki-Kristo hayana utaratibu huo. Lakini kwa kuwa Alhaji alikua anatafuta MNOGO WA PICHA YENYEWE ndio hapo maini yakaingia nyongo.
Kama bado tu mtu hajashtuka kitu hdi hapo, hivi watu bado tu hamjiulizi kwa nini ONYESHO LA TATU (linalotegemewa kuwa ndefu sana mpaka hadhira kujikuta wachapa tu usingizi badala ya kuendelea kufwatilia picha) la filamu ilivyoanza kwaa usiri mkubwa katika mahakama ya Kisutu na kwamba wahusika wote huko wakawa ni WATU WA KUFIKIRIKA tu huku wengine wakidaiwa kuwasili tu kutoka katika taifa la KUSADIKIKA ('nimewasili na bado ninaendelea kuwazoea').
Mpaka hapa wala mtu hahitaji kutngaziwa kwamba kwele Alhaj Afande Kova kalitia kovu chombo hiki, tulichopata kukiamini na kukithamini sana miaka hiyo, kwa namna ambayo itachukua miaka kuturudisha imani sisi Umma wa Tanzania.
Sasa kilichobaki pengine ni wahusika wkuu wa filamu hii warudi tena mezani ili waje na ubunifu mwingine maana huu wa sasa ndio kama hivo umekwishagonga mwamba.
Kova anapata wapi mandate ya kukataza watu wasiongee kuhusu masuala muhimu ya nchi, kwa nini tunakuwa mbumbumbu. Kova hana mamlaka ya ku-silence watu na watu wana haki kikatiba kudai na kupewa taarifa:
kila mtu anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu masuala muhimu kwa jamii
Hakika hili ni tukio muhimu
kwa maisha na shughuli za wananchi na pia linahusu suala muhimu kwa jamii.
Kova hebu mjibu Gwajima, ili wananchi tupate taarifa juu ya mkanganyiko ulioleta kwa kumkamata huyo mkenya!!!!!!!
Hawa majaji ni wa voda fasta,Kova anajidanganya sana ati jambo liko mahakamani hivyo lisijadiliwe kwani hapo umesevu????picha ndio kwanza inaanza wee ruka vihunzi tu wakukumaliza ni Dr Uli.utavaa miwani na hayo makengeza yako.Mahakama siku hizi imekuwa kama FFU. Yaani kitu kikija moto wanakipeleka mahakamani afu hakuna kuhoji. Kama kweli mahakamani wangekuwepo majaji wenye weredi na kazi zao wangeisha piga stop hali hiyo. Naweza kukubaliana na Mh Lissu kuwa na majaji wa fasta fasta.
Katika onyesho la nne, watatafutwa watu wengine ambao watabebeshwa huu mzigo wa nani mhusika, maana ili picha iishe salama lazima watafute mtu watakayemtwisha mzigo walioubeba maana unawaelemea nisawa na kubeba gunia la mavi usipolemewa litakunukia, Inavyoonekana mkuu wa kaya amewapa muda wafanye haraka kumsafisha
Sasa Mahakama ni Chaka la kuchimbwa dawa na Wahalifu wote Tanzania.
Mahakama sasa inatumika kufunga midomo Watanzania wasihoji upuuzi wa serikali,
Mahakama ni pazia la chuma la viongozi wa CCM na serikali yake kujikinga kisiasa.
Wanavuruga,wanadanganya, wanaiba,wanaharibu na kuvunjavunja
kisha wanatimua mbio kujificha nyuma ya mahakama.
Kuna haja ya kujenga hoja ya kuchunguza kwa ukaribu Chaka hili la Mahakama.
Kama kazi ya Ukamishna wa POLISI ndo hii falla na mjinga yeyote anaweza kuwa njagu.
Tulieni tuangalie Movie wazazi,maana mnapiga makelele kama mko mpirani tusubiri ubalozi wa Kenya waje tupa raha mtuhumiwa si mkenya ni mgogo mkazi wa mpwapwa wala Kenya hajui iko upande gani!
Dr Uli akirudi atahojiwa tu na hapo ndipo atapotiririka na kumwacha kinywa wazi huyu afande mrangi.Ngambo Ngali.
Hapa ndio katiba mpya inapotakiwa kubadilisha hii tabia mimi sio mtaalamu sana wa sheria ila navyoujua serikali ina mihimili mitatu bunge, mahakama na dola sasa hapa kila kimoja kinasheria zake na miongozo yake so, kwa uzoefu swala likishakua mahakamani uwezi kulijadili tena hata kama wananchi wakitaka kulijadili bado litakua limevunje sheria za nchi so mtalijadili wapi? Pia hata ulimboka akirudi atalijadili wapi? Either avunje sheria ya nchi kujadili jambo lilipo mahakamani.
serikali inatengeneza kaburi lake lenyewe,watatuzuia kwa fitna kulijadili suala hili kwa hila zao za kichaka cha mahakama,watafanikisha...ila trust me kumziba mtu mdomo ni kumuongezea chuki,heri mtu asemeee anyamazee...serikali haiaminiki,polisi hawaaminiki,mahakama hazina mvuto kwa wanyonge,viongozi hawana touch ya wananchi,hawapendwi.
Kinacho tokea ngado-singida ni kielelezo cha chuki ambayo ipo juu ya serikali na watu wanao i support serikali hiyo,chuki hii watawala wanaijenga kwa wananchi,chuki hii inaanza kukua,itahamia kwa akina nappe,mwigulu,wasira et el..ipo siku watapigwa kama wezi na wananchi...!
Ukiwashitaki polisi wataachiwa,ukiwapeleka mahakamani watashinda....lakini nikirusha jiwe,panga,au mkoki siwezi kuwakosa....they will feel the pinch that i always feel,the pains caused by them to me shall be paid as permanent torture to them..
Make my word