Hatimaye ADC yapata Usajili wa Kudumu

Hamna jipyahapo zaidi ya kuongeza watu wakula ruzuku za walipa kodi

angalia vile wavyo iga hadi rangi za bendera ili kuwachanganya wananchi

karibu sana na huku kwetu muone

Jipya nililoona ni kwa Chadomo kusababisha watu kupoteza maisha kwa ujinga Kama ilivyotokea jana Morogoro, Hivi ile kesi ya Mnyika ya kusababisha mauaji Kule kwa Nchemba inaendelea vipi? Mpori naye anachekesha sana kapigwa mjengoni eti kisasi unamfuata MTU kwake si ndio balaa sasa.
 
Hata maswala ya sheria una tuuliza sisi we mwanasheria gani usiye fuatilia mambo?

Hapa ADC hawana mwanasheria bora hii kazi wampe Prof.Maji marefu awe anapiga manyanga!

Jipya nililoona ni kwa Chadomo kusababisha watu kupoteza maisha kwa ujinga Kama ilivyotokea jana Morogoro, Hivi ile kesi ya Mnyika ya kusababisha mauaji Kule kwa Nchemba inaendelea vipi? Mpori naye anachekesha sana kapigwa mjengoni eti kisasi unamfuata MTU kwake si ndio balaa sasa.
 
Mhmmm!!!!! Yule Rashid wa cuf Naye ni padri? Lakini nasikia wanachama wake lazima wawe wamehifadhi juzuu za kutosha kichwani

Bwana Precise kama ulikua hujui basi hiki ulichoandika hapo kwenye blue ndio zile waswahili wanaziita 'Akili za kushikiwa'. Kwa taarifa yako hili la udini halitoweza kutuganda sisi huku ADC, ADC ni chama makini na ndio maana tumepokewa kwa shangwe na bashasha, tunaona wenzetu wanavyohusishwa na siasa za kidini na kikanda na tushalifanyia kazi hilo kwa kiasi kikubwa tu hivyo halitakuwa na madhara kwetu kama unavyotamani lituathiri. Karibu ADC - Tumaini la Mtanzania.
 
Nahitaji kadi najitolea nyumba yangu kuwa tawi la chama na ofisa chanika buyuni. 0715386011

Kwa niaba ya chama nashukuru sana kwa kuona kilicho sahihi bila kushurutishwa na mtu yeyote, Karibu ADC tunahitaji wapambanaji kama wewe kwani ndio njia pekee ya kuelekea kwenye Ukombozi wa nchi yetu. Sio baadhi ambao wametanguliza lugha zisizofaa za kashfa kisa tunapishana kiitikadi.
Nimechukua namba yako naahidi tutakutafuta.
ADC - Dira ya Mabadiliko.
 
Mkuu hivi JF kwako ni uwanja wa mapambano dhidi ya Uislam, badilika mkuu mapambano ya dini hayana faida jijengee heshima na kijengee heshima chama chako.

Mkuu Ritz,mwache azuzuke hapa jamvini tena nina wasiwasi huyu Precise Pangolin ni mhashamu kardinali Mwanya.
 
Du hawa nao wamepata usajli, adui mwingine wa cdm ameingia kwenye siasa za tz, ccm d karibuni na unafiki wenu, ngoja Hamad aanze kuvujisha siri za chama kwa liwalo na liwe, chama cha pemba hiki hamna jipya nyie.
 
Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed akihutubia Mkutano Mkuu wa Kwanza tangu ADC kipate Usajili wa Kudumu baada ya kualikwa na Uongozi wa ADC Taifa.
Kamanda Mwenyewe.JPG Sehemu ya Hotuba aliyoitoa Mhe. Hamad Rashid inasema "Nashangazwa na wale waliodhani kwamba hamtoweza, watu wenye vijicho na hasada kama hawa wako wengi...Ngoja niwape kisa cha bwana mmoja mchonga mtumbwi ili umsaidie kupata riziki yake; hasidi akasema hatoweza kuuchonga, alipoona umemalizika akasema hautoelea majini, alipoona unaelea akasema utapasuka, mchonga mtumbwi alitia masikio pamba akaendelea na lengo lake la kujipatia riziki na akafanikiwa, hayo ADC yaliwakuta ya mahasidi, wachoyo, vijicho na wakatishaji tamaa lakini mmefanikiwa, dumisheni matunda haya, msibweteke"
 
NDIO.......MHE. Hamad Rashid Mohamed ni mlezi WA ADC Kama aliva yo Sabodo kwa Chadema.

Nahitaji kusoma katiba ya chama chenu pengine nikashawishika kuchukua kadi maana nimekuwa undecided kwa muda mrefu, hebu ni PM ili nijue napataje katiba.
 
Increasing the number of opposition parties will not save the Tanzanians from makucha ya CCM, Nilidhani jitihad zingefanyika kupunguza vyam badala yake nyie mnaongeza!!!!!!! Ndio ni haki yenu kikatiba, lakini Demokrasia ya kweli haipimwi kwa wingi wa vyama!!!! Au mlivyosikia vyama vingi ndo mnataka vifike 1000!!!???? Mlipaswa kuunga mkono vyama vya upinzani vilivyopo, Muuingie mfanye mabadiliko ya kasoro zilizopo!!, Kuna haja gani kuwa na karatasi za kura zenye wagombea Lundo mwisho wa siku wengine wanapata kura 1??? Kuna haja gani kuwa na vyama vinavyofanya kampeni mikoa miwili tu badala ya nchi nzima!!?? Kuna haja gani kuwa na vyama vinavyoishia kujitoa uchaguzi unapokaribia??? Kuna haja gani kuwa na wagombea ambao mikutano yao ina watu 3 tu!!??? Kuna haja gani kuwa na vyama ambavyo mwisho wa cku wagombea wake hukata tamaa na huanza kuwapigia debe wengine!!??? Tunataka vyama vichache vyenye upinzani wa kweli!!!
 
Mkuu hivi JF kwako ni uwanja wa mapambano dhidi ya Uislam, badilika mkuu mapambano ya dini hayana faida jijengee heshima na kijengee heshima chama chako.
Mkuu nimekuelewa Ngoja nichomoke kabisa kwenye hii thread Asante kwa ushauri
 
Back
Top Bottom