Hatimaye ADC yapata Usajili wa Kudumu

hasan124

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
716
128
Leo Jumanne tar.28-08-2012 majira ya saa4 hivi za ASUBUHI chama chetu cha ADC kilichojizolea umaarufu mkubwa katika Nyanja za Siasa NCHINI Tanzania hata Kabla ya kuanza rasmi kazi za kisiasa, kimefanikiwa kupata usajili WA kudumu baada ya kukamilisha zoezi la UHAKIKI katika mikoa kumi (10).

Mikoa iliyohakikiwa na ofisi ya Msajili WA vyama vya Siasa CHINI ya MHE. john Tendwa ni pamoja na Tanga, Mwanza, Pemba, Mara, Unguja, Tabora, Dodoma, Lindi, Mtwara na Dar ES Salaam ambapo chama kilifanikiwa kuvuka idadi iliyo kuwa inahitajika na ofisi ya Msajili ya wanachama wadhamini 200 kwa kila Mkoa.

Tukio hili la kihistoria linaashiria mwanzo WA Harakati za chama cha ADC katika duru la Siasa NCHINI Tanzania, Kama ambavyo moja kati ya Madhumuni yake kuwa (1) Kushika dola kwa njia halali na za kidemokrasia.
Akizungumza na waandishi WA Habari mara baada ya kukabidhiwa HATI ya Usajili Mwenyekiti WA ADC TAIFA MHE. Said Miraji alinukuliwa akielezea furaha Yao ya kukamilisha sehemu ya kwanza na nyeti ya kupata usajili WA kudumu na Leo hii katika Hotel ya Lamada Ilala chama kinafanya MKUTANO MKUU WA KWANZA KAMA CHAMA RASMI CHA SIASA ambapo watapata fursa ya kupitisha Katiba ya chama pamoja na Kuchagua viongozi WA Kitaifa WA chama.
GOD BLESS ALLIANCE FOR DEMOCRATIC CHANGE.

ADC - DIRA ya Mtanzania.
+++++++++++++++++++++++++++++++++
Latest Picture Mkutano Mkuu wa Kwanza ADC Taifa mara baada ya usajili wa kudumu 28-08-2012 Lamada Hotel and Apartment Ilala.

ADC Mkutano Mkuu.JPG Mkutano Mkuu ADC.JPG
Wajumbe wa Mkutano Mkuu ADC Taifa.JPG
 
Baada ya kulamba posho ya uchaguzi ujao tutawasoma vizuri!
 
Karibuni sana katika uwanja wa kupigwa risasi za moto na mabomu ya machozi, labda muwe chama D.
 
Karibuni sana katika uwanja wa kupigwa risasi za moto na mabomu ya machozi, labda muwe chama D.

Madhumuni yetu ni:
(1) Kushika Dola kwa njia hatlali na za kidemokrasia.
(2) Kujenga Umoja na Mshikamano imara kwa waTanzania wote.
(3) Kujenga uchumi imara na kulinda raslimali za Nchi kwa manufaa ya waTanzania wote.
(4) KUPINGA KWA NGUVU ZOTE AINA ZOTE ZA UBAGUZI NA UKANDAMIZAJI.
Naona Namba NNE (4) itakuonyesha msimamo wetu katika Hilo la risasi za moto na mabomu.
 
Hicho chama kweli ni mitambo kama wewe ndio wamekupa kazi ya kueneza na unaweka andiko dhaifu hivyo kweli mnayo! karibuni sana.
 
Kilichofanyika ni kuongeza idadi ya vyama na si kupata chama bora. Kama miongoni mwa vyama vilivyopo hawakuona cha kuwafaa unategemea wao wanakuja na jipya gani.
 
. hasan124 Kuna uhusiano wowote kati ya chama hiki na Hamad Rashid Mohamed?
 
Last edited by a moderator:
Sera za chama ni muhimu,hiki chama kinafuata mlengo gani wa siasa?
 
Leo Jumanne tar.28-08-2012 majira ya saa4 hivi za ASUBUHI chama chetu cha ADC kilichojizolea umaarufu mkubwa katika Nyanja za Siasa NCHINI Tanzania hata Kabla ya kuanza rasmi kazi za kisiasa, kimefanikiwa kupata usajili WA kudumu baada ya kukamilisha zoezi la UHAKIKI katika mikoa kumi (10).

Mikoa iliyohakikiwa na ofisi ya Msajili WA vyama vya Siasa CHINI ya MHE. john Tendwa ni pamoja na Tanga, Mwanza, Pemba, Mara, Unguja, Tabora, Dodoma, Lindi, Mtwara na Dar ES Salaam ambapo chama kilifanikiwa kuvuka idadi iliyo kuwa inahitajika na ofisi ya Msajili ya wanachama wadhamini 200 kwa kila Mkoa.

Tukio hili la kihistoria linaashiria mwanzo WA Harakati za chama cha ADC katika duru la Siasa NCHINI Tanzania, Kama ambavyo moja kati ya Madhumuni yake kuwa (1) Kushika dola kwa njia halali na za kidemokrasia.

GOD BLESS ALLIANCE FOR DEMOCRATIC CHANGE.

ADC - DIRA ya Mtanzania.

I hope nyie sie kile chama cha kaskazini kama cha wenzetu fulani wapenda vurugu na kutofuata sheria. Ila hiyo rangi nyekundu kwenu yamaanisha nn? kwani kwa wenzenu ina maana ' TUTAMWAGA DAMU KWA NJIA YOYOTE ILI MRADI TUINGIE IKULU'.

Back
Top Bottom