Hatima ya waliofutiwa matokeo darasa la saba

JamboJema

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
1,143
209
Nimekuwa nikijaribu kujiuliza maswali mengi kuwa nini itakuwa hatima ya hawa watoto waliofutiwa matokeo juzijuzi na NECTA....ndo wameishia hapo au kuna nafasi ipi tena kwao kielimu?
Je, ni wao ndo walishawishi udanganyifu huu (kama kweli ulikuwepo)?
Na kama sio wao walioshawishi kosa hili kutendeka, ni haki wao kuhukumiwa hivi?
Na waliotenda HASA HILI KOSA (i mean - wasimamizi, walimu wakuu, n.k) wanashughulikiwa vipi?
Hakika siamini kama watoto hawa walikuwa na uwezo wa kushawishi huu uozo regarding their age. Ningewashauri wahusika wafikirie suala la kuwapa second chance kwa kuwapa mtihani mwingine wenye usimamizi thabiti ili future yao tusiiharibu kwa vile tu sie wanetu wako intanesheno za Manzese na ulaya.
JUST THINKING ALOUD!
 
Back
Top Bottom