Hatima ya Ubunge wa Chenge baada ya hukumu

Kweli Tanzania there is no justice kabisa. Kama huyo Chenge amelipa 700,000/= inabiidi watoto wetu who are in jail should also be bailed out in the same manner than to Chenge. In actual fact, Chenge is suppose to rotten in jail forever as others.

We should also ask JK's government regarding the killing of Ernest Manumbu who was the Chief Medical Office at the Ministry of Health. And Anna Abdallah should be answerable to the killing. Why is so much Mafias in CCM.
 
Tatizo la Katiba yetu iko 'silent' kuhusu mtu anayekutwa na hatia akiwa tayari kwenye uongozi (mid-way) kama ilivyo kwa Chenge. Lakini la msingi hapa ni kwamba Chenge amepatikana na hatia na amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu (ambayo ni zaidi ya miezi sita) na option ya fine. Anapolipa fine haimaanishi kwamba conviction inafutika. Huyu kisheria ni CONVICT na haruhusiwi kugombea ubunge. Lakini kwa sababu tayari ni mbunge, kwa maoni yangu na interpretation yangu ya sheria hii, moja kwa moja anapoteza sifa ya kuwa mbunge, na Spika anapaswa kulitangaza jimbo lake la uchaguzi kuwa vacant na ni lazima by-election ifanyike.
Chenge huyu huyu mzee wa vijisenti? Sijui kama itawezekana.
 
Nimeangalia katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nimeona hivi kuhusiana na hali inayofanana na hii aliyo nayo Mh. Chenge.

Ibara ya 67
(2) Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge-
(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu.

Chenge amekutwa na hatia na amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu au faini 700,000Sh.

Sasa hatima ya Chenge inakuwaje baada ya hukumu hiyo?

Naomba wataalamu wa Sheria na katiba mtufafanulie vizuri.

Naona hiyo ya red inawasaidia wengi sana. Hata Chenge hiyo inamrudisha bungeni
 
Sasa CHADEMA kuna wanasheria wazuri inakuaje hawajaliona hili? Inatakiwa washinikize kuitishwa uchaguzi mdogo haraka iwezekanavyo sio kusubiri jamaa wasafishane as they do always maana katiba iko wazi katika hilo kama wadau hapa walivyoainisha... Chenge sio mbunge no more na jimbo liko wazi kama katiba inavyosema, what are they waiting for?
 
sherehe za krismasi na mwaka mpya zimechukua muda wangu sana na kushindwa kuendelea na mjadala wangu kuhusu katiba.

Kulingana na katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania ya sasa hivi, chenge amepoteza sifa za kuwa mbunge kufuatana na ibara ya 71.(1)(a) inayosema kuwa

"mbunge atakoma kuwa mbunge na ataacha kiti chake katika bunge litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo - (a) ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa
mbunge lingemfanya asiwe na sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi au asiweze kuchaguliwa
au kuteuliwa kwa mujibu wa masharti ya katiba hii;
"

hukumu ya kifungo cha miaka mitatu jela au faini ya shilingi laki saba aliyopewa chenge inamuondolea sifa za kuchaguliwa kuwa mbunge kwa mujibu wa katiba ya tanzania ibara ya 67(2)(c) inayosema "mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa mbunge-
(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na mahakama yoyote katika jamhuri ya muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya
kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa
uaminifu;
"


kwa hiyo, inabidi tume ya uchaguzi iitishe auchaguzi mdogo kujaza nafasi hiyo iliyoachwa wazi na chenge. Hata hivyo kwa vile tume hiyo hiyo ya uchaguzi ndiyo iliyokiuka katiba ta tanzania ibara ya 41(6) na kumtangaza kikwete kuwa rais wa tanzania wakati hakupata kura nyingi zaidi ya wagombea wengine, basi inawezekana tume hiyo ikaja na maelezo ya kuhalalisha kwa nini chenge ataendelea kuwa mbunge.

naomba kuuliza hivi ismail aden rage si ameshawahi kuhukumiwa mbona mbunge sasa ! Nothing personal just giving a real example !
 
naomba kuuliza hivi ismail aden rage si ameshawahi kuhukumiwa mbona mbunge sasa ! Nothing personal just giving a real example !

Imeshajibiwa kwenye postings za thread hii.

Rage alikata rufaa na kushinda rufaa yake mahakamani. Hivyo mahakama ya ngazi ya juu ilitengua adhabu iliyotolewa na mahakama ya ngazi ya chini, na kutangaza kuwa hana hatia.

Kwa hiyo kisheria adhabu hiyo kwa Rage imefutwa. Rage ni sawa na mtu ambaye hajahukumiwa kifungo.
 
bado sijapata kipengele ambacho kinazungumzia kuhusu mbunge au kiongozi akipatikana na kosa wakati tayari ni kiongozi kwenye katiba yetu, kwa hiyo kivuli hiki kinaweza kumvunika Mzee wa vijisent na akaendelea mpaka muda wake wa miaka mitano uishe
 
bado sijapata kipengele ambacho kinazungumzia kuhusu mbunge au kiongozi akipatikana na kosa wakati tayari ni kiongozi kwenye katiba yetu, kwa hiyo kivuli hiki kinaweza kumvunika Mzee wa vijisent na akaendelea mpaka muda wake wa miaka mitano uishe

Soma posting #67 thread hii.

Yahusu ibara ya 71 (1) a ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Sherehe za krismasi na mwaka mpya zimechukua muda wangu sana na kushindwa kuendelea na mjadala wangu kuhusu katiba.

Kulingana na katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya sasa hivi, Chenge amepoteza sifa za kuwa mbunge kufuatana na ibara ya 71.(1)(a) inayosema kuwa

"Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake katika Bunge litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo - (a) ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa
Mbunge lingemfanya asiwe na sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi au asiweze kuchaguliwa
au kuteuliwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii;
"

Hukumu ya kifungo cha miaka mitatu jela au faini ya shilingi laki saba aliyopewa Chenge inamuondolea sifa za kuchaguliwa kuwa mbunge kwa mujibu wa katiba ya Tanzania ibara ya 67(2)(c) inayosema "Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge-
(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya
kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa
uaminifu;
"


Kwa hiyo, inabidi tume ya uchaguzi iitishe auchaguzi mdogo kujaza nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Chenge. Hata hivyo kwa vile tume hiyo hiyo ya uchaguzi ndiyo iliyokiuka katiba ta Tanzania ibara ya 41(6) na kumtangaza Kikwete kuwa Rais wa tanzania wakati hakupata kura nyingi zaidi ya wagombea wengine, basi inawezekana tume hiyo ikaja na maelezo ya kuhalalisha kwa nini Chenge ataendelea kuwa mbunge.

kama jf kuna waelewa wengine kama 100 walio na ujuzi kama wako, mimi nakuwa na amani. Chenge amesimamishwa ubunge na Mahakama ya kinondoni kwa kumtia kolokolo kwa zaidi ya miezi 6,au faini sh.lak7,au vyote kwa pamoja. Hakimu kutotaja "vyote kwa pamoja" inamaana chenge hatoenda jela ila kifungu icho kinamhusu na ndo kilichomtia hatiani,labda na kifungu kile kivunje vipengele vpengele ili kwenda jela na kulipa faini vijitegemee. Pili katiba kwa ibara no.67 na 71 ya katika ya Tanzania,chenge si mbunge tena ila asubiri huruma ya Mafisadi ya kumlinda. Nakumbuka wakati anagombea ubunge rais Jakaya alisema ni mtuhumiwa mpaka Mahakama imtie hatiani,akaruhusiwa kugombea,sasa mahakama imemtia hatiani,KIKWETE atamke tena kuwa kwa kuwa maneno aliyotuhaidi yametimia. Ametiwa hatiani,ila ujanja ujanja wa sheria umeifunga nyara/ela lak7 ya jamhuri kiasi cha miaka3 badala ya chenge!
 
bado sijapata kipengele ambacho kinazungumzia kuhusu mbunge au kiongozi akipatikana na kosa wakati tayari ni kiongozi kwenye katiba yetu, kwa hiyo kivuli hiki kinaweza kumvunika Mzee wa vijisent na akaendelea mpaka muda wake wa miaka mitano uishe

mkuu ibara ya 71 ipo kwenye katiba yako au?
 
kama jf kuna waelewa wengine kama 100 walio na ujuzi kama wako, mimi nakuwa na amani. Chenge amesimamishwa ubunge na Mahakama ya kinondoni kwa kumtia kolokolo kwa zaidi ya miezi 6,au faini sh.lak7,au vyote kwa pamoja. Hakimu kutotaja "vyote kwa pamoja" inamaana chenge hatoenda jela ila kifungu icho kinamhusu na ndo kilichomtia hatiani,labda na kifungu kile kivunje vipengele vpengele ili kwenda jela na kulipa faini vijitegemee. Pili katiba kwa ibara no.67 na 71 ya katika ya Tanzania,chenge si mbunge tena ila asubiri huruma ya Mafisadi ya kumlinda. Nakumbuka wakati anagombea ubunge rais Jakaya alisema ni mtuhumiwa mpaka Mahakama imtie hatiani,akaruhusiwa kugombea,sasa mahakama imemtia hatiani,KIKWETE atamke tena kuwa kwa kuwa maneno aliyotuhaidi yametimia. Ametiwa hatiani,ila ujanja ujanja wa sheria umeifunga nyara/ela lak7 ya jamhuri kiasi cha miaka3 badala ya chenge!

Yap!
 
Nanukuu tena ibara ya 71 (1)a

71 - (1) Mbunge atakoma kuwa mbunge na ataacha kiti chake katika bunge litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo -
(a) ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa mbunge lingemfanya asiwe na sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi au asiweze kuchaguliwa au kuteuliwa kwa mujibu wa masharti ya katiba hii;"
 
Spika, mwenyekiti wa NEC na mwanasheria mkuu wako kimya na sitegemei kuwasikia wakizungumzia ili swala. Alafu bado mnadai Tanzania tunafuata utawala wa sheria. Smh! Happy New Year kwa wote.
 
Hivi wachangiaji wengi humu wanakimbilia kutype kabla ya kusoma? Icho kifungu (c) ukisoma utaona kuna comma.

Mkuu wangu, ni kweli kuna comma katika kifungu hicho ila maneno makuu ambayo ndiyo inabidi yaangaliwe kwa makini ni haya niyopigia mistari.

(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu; ".


  • Chenge kahukumiwa na mahakama halali katika jamhuri wa muungano
  • Hukumu yange ni ama kufungwa jela miaka mitatu au kulipa faini ya shillingi laki saba. Hukumu hizi mbili zinalingana mbele ya sheria, ila mtuhumiwa anapewa uhuru wa kuamua atumikie ipi; yeye kaamua kulipa faini. Penal code kifungu 29(ii) kinasema "Kwenye kosa linalopasiwa adhabu ya faini au kifungo,
    utozaji wa faini hiyo au kifungo hicho litakuwa ni jambo la hiari ya hiyo mahakama."

Nadhani tunakubaliana na hayo; tatizo sasa ni kuelewa iwapo mojawapo ya makosa ya Chenge yanaambatana na utovu wa uaminifu. Kwa maoni yangu, na kulingana sheria nyingine kadhaa zilizo nje ya Katiba, nina imani kuwa Chenge alikosa uaminfu na hivyo kupoteza sifa za ubunge kama ifuatavyo:


Penal code ibara ya 123 inasema hivi:

123. Kila mtu ambaye, kwa makusudi, hatii sheria yoyote kwa kutenda kitendo chochote ambacho chakatazwa na sheria au hatii sheria kwa kutotenda kitendo chochote ambacho chahusika na watu au sehemu yoyote ya watu, mtu huyo ni mwenye hatia ya kosa dogo, na isipokuwa yaonekana kwamba sheria ilikusudia kutoa adhabu nyengine, atapasiwa kifungo cha miaka miwili.

Chenge alikutwa akiendesha gari lisilokuwa na bima. Sheria za usalama barabarani zinataka kila gari liwe na bima. Kwa kosa hili Chenge alitakiwa afungwe miaka miwili.


Ibara ya 120 ya penal code inasema kuwa

120. Mtu yeyote aliyeajiriwa katika kazi ya Serikali ambaye katika kufanya shughuli za kazi yake, afanya udanganyifu wowote au uvunjaji uaminifu ambao utadhuru watu, iwe udanganyifu huo au uvunjaji uaminifu huo ungekuwa ni jinai au sivyo lau kama ungetendewa mtu raia, mtu huyo ni mwenye hatia ya kosa dogo.

Chenge huyo aklikuwa akitumia gari alilopewa na serikali kama mbunge bila kulilipia bima, na hivyo kuwa amevunja uaminifu unaoendana na matumizi ya gari hilo. Uvunjaji uaminifu huo uliendana na kuwadhuru watu ambao hawataweza kulipwa fidia kwa vile gari la mbunge Chenge halikuwa na Bima.


Sasa ninapounganisha vifungu hivyo viwili hapo juu na hukumu iliyotolewa kwa Chenge, nainaona wazi kuwa amepoteza sifa za kuwa mbunge. Kumbuka pia kuwa kupata leseni ya udereva siyo haki bali ni privilege inayoendana na kuaminiwa na serikali. Ukikosa uamifu huo basi seriukali inaweza kukunyanyang'anya leseni hiyo wakati wowote. Kupatikana na hatia ya kuendesha gari bila kuwa na bima, hata kama halikuwa gari la ubunge baso ni kuonyesha kuwa Chenge alikosa uaminifu wa matumizi ya leseni yake.
 
• Tafsiri Mbalimbali za kisheria( toka Mwanachi)


1. Dr. Mvungi

"...kwa mujibu wa sheria Chenge ataendelea kuwa mbunge kwa sababu hajatumikia kifungo na badala yake amelipa faini. ...Kama angeenda moja kwa moja kutumikia kifungo asingekuwa na sifa ya kuitwa mbunge na hata uchaguzi ujao asingeweza kugombea tena lakini, kwa sababu kalipa faini tu, hajapoteza ubunge wake.”

Dr wa sheria naye hajui kuwa sheria haisemi kutumikia kifungo bali inasema kuhukumiwa kifungo. Mtu anaweza kuhukumiwa kifungo lakini rais akamsamehe aseinde jela kutumikia kifungo hicho bila kufuta hukumu.

2. Prof. Safari

"...kama zingekuwa zinatumika sheria za zamani, kwa hukumu hiyo, Chenge asingeweza kugombea tena ubunge. Unajua hata sheria mpya ya uchaguzi sijaipitiakuona inasemaje kuhusu suala hili lakini, ninachoweza kukumbuka ni kwamba sheria ya zamani ya makosa yote yaliyokuwa yakihusu ‘mortality’ ulikuwa huwezi kugombea tena. Sasa sijui kwa sheria hii ya sasa,”.

Profesa wa sheria hajui sheria inasemaje; afadhali yeye hakutoa tafsiri mbovu.

3. Wakili Harlod Sungusia
“...hukumu ya Chenge haina madhara yeyote kwake katika nafasi zake kisiasa. ...Hukumu ilikuwa sahihi wala hakimu hakukosea kuitoa. Kilichopo pale ni kwamba makosa aliyokutwa nayo Chenge si ya kukosa uaminifu hivyo, hayamfutia nafasi yake ya kuendelea kuwa Mbunge
,”.

Wakili naye anaangallia tafsiri ya uaminifu kwa dirisha dogo sana, anasahau kuwa kuongopa kwa aina yoyote ni kukosa uaminifu. Kutotekeleza wajibu wa kisheria na kujifanya kuwa umetekeleza wajibu huo ni kuongopa. Chenge hakutekeleza wajibu wa kulikatia bima gari lake lakini akaendelea liendesha barabarani kama vile amelikatia bima. Kitendo hicho ni kuidanganya serikali na hivyo kukosa uaminifu.
 
• Tafsiri Mbalimbali za kisheria( toka Mwanachi)


1. Dr. Mvungi

"...kwa mujibu wa sheria Chenge ataendelea kuwa mbunge kwa sababu hajatumikia kifungo na badala yake amelipa faini. ...Kama angeenda moja kwa moja kutumikia kifungo asingekuwa na sifa ya kuitwa mbunge na hata uchaguzi ujao asingeweza kugombea tena lakini, kwa sababu kalipa faini tu, hajapoteza ubunge wake."

Dr wa sheria naye hajui kuwa sheria haisemi kutumikia kifungo bali inasema kuhukumiwa kifungo. Mtu anaweza kuhukumiwa kifungo lakini rais akamsamehe aseinde jela kutumikia kifungo hicho bila kufuta hukumu.

2. Prof. Safari

"...kama zingekuwa zinatumika sheria za zamani, kwa hukumu hiyo, Chenge asingeweza kugombea tena ubunge. Unajua hata sheria mpya ya uchaguzi sijaipitiakuona inasemaje kuhusu suala hili lakini, ninachoweza kukumbuka ni kwamba sheria ya zamani ya makosa yote yaliyokuwa yakihusu ‘mortality' ulikuwa huwezi kugombea tena. Sasa sijui kwa sheria hii ya sasa,".

Profesa wa sheria hajui sheria inasemaje; afadhali yeye hakutoa tafsiri mbovu.

3. Wakili Harlod Sungusia
"...hukumu ya Chenge haina madhara yeyote kwake katika nafasi zake kisiasa. ...Hukumu ilikuwa sahihi wala hakimu hakukosea kuitoa. Kilichopo pale ni kwamba makosa aliyokutwa nayo Chenge si ya kukosa uaminifu hivyo, hayamfutia nafasi yake ya kuendelea kuwa Mbunge
,".

Wakili naye anaangallia tafsiri ya uaminifu kwa dirisha dogo sana, anasahau kuwa kuongopa kwa aina yoyote ni kukosa uaminifu. Kutotekeleza wajibu wa kisheria na kujifanya kuwa umetekeleza wajibu huo ni kuongopa. Chenge hakutekeleza wajibu wa kulikatia bima gari lake lakini akaendelea liendesha barabarani kama vile amelikatia bima. Kitendo hicho ni kuidanganya serikali na hivyo kukosa uaminifu.

Hilo naona ndo litaishia hivi.

Sina hakika kama angekuwa mbunge asiye kigogo au asiye wa CCM tafsiri hizi zingewekwa hivi.
 
Hapana yule alitoka kwa msamaha wa rais, na pia nakumbuka wakati wanamuhoji kituo fulani cha redio yeye alisema, siku hiyo ya msamaha asubuhi aliitwa na bwana jela na kuambiwa umepata msamaha wa rais kwa hiyo leo utatoka.

Hakutoka kwa rufaa
.

Eliakim, Ni ukweli Rage alitoka kwa msamaha wa Rais lakini alipokuwa uraiani alikata rufaa Mahakama Kuu. Nayo ilimwona hana hatia na kosa alilofungwa nalo pale Mahakama ya Hakimu Mkazai Kisutu. Kwa kushinda rufaa yake inamaanisha alifungwa kimakosa na kwa hiyo Mahakama Kuu ilimsafisha.

Chenge anachoweza kufanya naye ni kukata Rufaa, Mahakama ya juu. Na iwapo Mahakama itamsafisha basi anaweza kugombea ubunge tena. Kinachojadiliwa hapa ni kwamba Chenge anastahili kuendelea kuwa Mbunge wakati ameshapatikana na hatia na kuhukumiwa? Tatizo wanasheria wetu humu ndani badala ya kutuelewesha wanakuwa wakali kama piripiri. Kwa umbumbumbu wangu naona kama katiba imenyamaza kimya hapa kuhusiana na Chenge.

Kwenye fomu za kugombea ubunge kuna mahali ambapo unaulizwa kama uliwahi kuhukumiwa kwa makosa ya jinai, nadhani hapa ndipo Spika na watu wengine wangeweza kutumia kipengele hicho kwamba Chenge amewahi kuhukumiwa (Kama itakavyokuwa mwaka 2015 kama atataka kutetea kiti chake au kiti kingine chochote) lakini kwa sasa Katiba haiko wazi.
 
Back
Top Bottom