Hatima ya Siasa zetu uchwara!

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Kwenye uchaguzi wa kuchagua wabunge wa kwenda kutuwakilisha kwenye bunge la Afrika Mashariki (ingawa si bunge) tumejifunza mambo mengi sana.

Nimejifunza kama taifa hatuna kabisa mambo ya msingi tunayotaka yasimamiwe kwenye bunge la Afrika Mashariki. Wanasiasa wetu walioko bungeni kwa mara nyingine wametuthibitishia kwamba wako mule bungeni kwa bahati tu. sikuona kabisa wabunge wakiuliza maswali yenye mshiko kuhusu Jumuiya yenyewe ya Afrika Mashariki.

Kama mbunge anamuuliza mgombea eti atapataje taarifa za Afrika Mashariki au nini madhumuni ya kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo, sidhani kama maswali hayo yana fanana na hadhi ya wagombea ubunge wa Afrika mashariki. Hivi kwa nini wasingewauliza maswali ya kisera zaidi kuliko kuuliza maswali kama wanawauliza watoto wa kidato cha pili?

Hivi wale tuliowachagua walitueleza wanajua nini kuhusu sera za Ardhi za nchi nyingine za Jumuiya. wanafahamu nini kuhusu ajira na soko lake kwenye jumuiya. Masuala ya nishati na mazingira yakoje na msimamo wao ni upi kuyahusu. Kiwango chao cha ufahamu kuhusu chumi za nchi zilizoko kwenye jumuiya kikoje na Tanzania itafaidikaje kwa kuwepo kwao kwenye Bunge hilo?

Maswali hayo na mengine mengi hayakuulizwa kwa sababu kwa siasa uchawara za nchi yetu uchaguzi ulishafanyika siku moja kabla na kilichofanyika ndani ya ukumbi wa bunge ni kuthibitisha matokeo yaliyokwisha kuwepo tayari.
 
ha ha ha ha! Ukiwa katika jamii ya mazuzu basi jua unaongozwa na viongozi mazuzu kwa sababu imenenwa jamii ya wezi huongozwa na mwizi!!
 
ha ha ha ha! Ukiwa katika jamii ya mazuzu basi jua unaongozwa na viongozi mazuzu kwa sababu imenenwa jamii ya wezi huongozwa na mwizi!!
Lazima tufanye mabadiliko kwa hali yoyote ile!!
 
Back
Top Bottom