Hatibu Kihiri Senkoro adai yeye na Pesambili Mramba ni damu-damu.

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,408
54,886
..hii imetoka kwenye gazeti la raia mwema.


..Hatibu Senkoro amezungumza mambo mengi kuanzia masuala ya sekta ya madini, historia yake, mpaka mahusiano yake na Basil Pesambili Mramba.

Raia Mwema: Kuna hisia zimeibuliwa kuwa ilipotokea umemdhamini Mramba (aliyekuwa Waziri Basil Mramba) waliamini mnamiliki hisa katika Mgodi wa Dhahabu Geita, unasemaji?


Senkoro: Aaah! Hilo swali lako sina hakika nalo. Lakini ni kweli mimi nimemdhamini Mheshimiwa Mramba. Kama nilivyoeleza, mimi na Mheshimiwa Mramba tunajuana tangu NDC miaka mingi tukiwa bado vijana.

Tumesoma Tabora School. Tumefanya kazi wote Williamson Diamonds. Tumehamishwa wote kutoka Williamson Diamonds kwenda NDC. Tumefanya kazi wote NDC.

Wake zetu wamesoma shule moja pamoja. Wanafahamiana. Watoto wetu wanafahamiana. Mimi Mramba ni ndugu yangu. Simwoni kama waziri. Mramba namwona kama ndugu kutokana na uhusiano huo, mimi ni Mpare yeye ni Mchaga, lakini Mramba ni ndugu yangu damu-damu.
kusoma interview nzima bonyeza hapa.
 
..hapa anazungumzia sekta ya madini.


..naomba great thinkers mchambue hizi idea zake.

Raia Mwema: Watanzania wengi wanaona kampuni za madini, kama hii ya kwako ya dhahabu kama zinawaibia. Wanaona ni busara, fedha zinazotokana na uzalishaji madini za kampuni za madini ziwekwe kwenye mabenki yetu, pili; kama nchi tuwe na hisa kwenye migodi hiyo, kama Mtanzania ukiondoa madaraka yako mgodini, una maoni gani juu ya hisia hizi?


Senkoro: Suala la kwanza, hilo la kuweka fedha katika benki ya Tanzania, labda nitoe historia. Makampuni yote makubwa haya ya madini kama Barrick, na Anglo Gold Ashanti na hasa kwa dunia nzima, hawa mtaji wao mkubwa wakienda mahali kuanzisha mgodi ni kukopa kutoka benki za nje. Wanakopa.
Kwa hiyo, leo ukienda Geita au hata Kahama Gold Mine (Bulyanhulu) ukaona balance sheet zao, utaona mikopo ni mingi kuliko fedha alizowekeza yule mwenye hisa.
Sasa wakati ule mwekezaji wa Geita Gold Mine ambaye alikuwa Ashanti Gold, si Anglo Gold Ashanti ambao walikuja baadaye, wakati ule alivyoenda akaona mgodi wa Geita unamfaa na akataka kuununua na akaomba mkopo kutoka benki ya nje, na benki za ndani hazina uwezo wa kukopesha fedha hizo, kipindi hicho cha miaka ya mwishoni mwa 1990, hata mabenki mengi haya ya sasa hayakuwapo.
Sasa masharti waliyopewa na benki za nje ni kwamba; tutakukopesha na kama ilivyo kawaida ya benki, fedha zako za mauzo uweke katika akaunti ya benki yetu. Kwa hiyo, unakopeshwa na Barclays Bank London, Uingereza unapewa masharti fedha zako uweke huko.
Kwa hiyo katika mikataba ambayo kampuni hizi za madini zimeingia na Serikali ilibidi waombe kwamba wanasharti hilo ambalo wamepewa na benki za nje, na Serikali walikubali, kwa hiyo katika mikataba hiyo tunaita MDA kuna kipengele ambacho Serikali imekubali fedha zako kutokana na matakwa ya benki za nje unaruhusiwa kuzihifadhi London au New York kulingana na mkataba.
Kwa hiyo haya makampuni ya madini hayaweki fedha nje kwa sababu yanataka, ni kwa sababu yule aliyemkopesha anataka hivyo na hamna njia kama unataka fedha nyingi. Ni kama wewe Mtanzania ukienda Stanbic kukopa sharti la kwanza atakwambia akaunti yako Barclays hamisha ili aweze kujua mambo yanavyokwenda, vinginevyo kama wewe utaweka fedha zako NBC au kwingine nitatuaje mwenendo wako? Hiyo ni hali ya kawaida.
Hili la hisa, nadhani ni suala la sera tu kwa sababu nimeona Serikali ilikuwa na hisa katika mgodi wa Kahama, lakini baadaye wakaziuza, Serikali imekuwa na hisa katika Benki ya NMB lakini wakaziuza.
Kwa hiyo, suala ni sera, nadhani inauza hisa zake kwa sababu ilisema itajiondoa katika kufanya biashara. Kwa hiyo lazima tuelewe hilo, ikiwa sera ya Serikali ni kuacha sekta binafsi ifanye biashara ni wazi kuwa pale ambapo ina hisa wataziuza.
Sasa suala ni je, Mtanzania wa kawaida utamshirikishaje awe na hisa kwenye makampuni ya madini, mashirika mengine na mabenki. Nadhani suala hapo ni kumtaka huyu mwekezaji katika sekta ambazo ni nyeti, baadaye …baada ya kuanza kutengeneza faida na ameweza kukidhi matakwa ya uuzaji hisa katika soko la hisa, aorodheshe hisa zake katika Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) ili Mtanzania wa kawaida awekeze.
Sasa kwa haya makampuni ya nje kuna kikwazo kidogo. Kwa sababu tatizo kubwa kwa Soko la Hisa Dar es Salaam ni liquidity (ukwasi). Hata ukisoma kwenye magazeti ya nje au televisheni za nje huoni wakiizungumza kwa sababu ni mtoto bado mchanga na mtu anataka awekeze pakubwa, penye uwezekano wa uuzaji na ununuzi, hapa kwetu (DSE) mzunguko huo si mkubwa.
Kwa hiyo hawa wakubwa walisema kama mnataka tuweke hisa zetu kwenye DSE basi mruhusu hata wawekezaji wa nje ambao ndio wanaweza kuleta msisimko katika DSE, hivyo mfumue sera zenu ili muwezeshe huyu wa nje aweze kununua. Hii ina faida na hasara zake.


Raia Mwema: Hasara ni zipi?


Senkoro: Ni kama hivyo mlivyoona uchumi ulivyoporomoka majuzi kutokana na mtikisiko wa uchumi duniani.
Soko la hisa kama Nairobi ambalo wanaruhusu kwa kiasi fulani wawekezaji wa nje kuuza na kununua hisa, kwa takwimu nilizonazo, soko la hisa la Nairobi liliporomoka kwa zaidi ya asilimia 20.
Hapa kwetu hapakutokea kwa sababu hakuna mtu wa nje. Kwa hiyo, kuna tatizo hilo ikitokea dharuba ya kilimwengu, nawe utaathiriwa. Lakini ukikataa fedha za nje pia hutazipata, yaani hakutakuwa na mzunguko wa fedha kwenu kutoka nje ya nchi.


Raia Mwema: Lipo wazo kuhusu utaratibu wa kuhodhi maeneo ya kuchimba madini kwa leseni. Wapo wanaolalamika, kwamba wachimbaji wakubwa, mfano Bulyanhulu, aliyekuwa anamiliki anaweza kuuza eneo kwa bei kubwa kwa hiyo wanaendelea kuhodhi wakubwa. Kuna hoja utaratibu huu ubadilishwe. Wewe unafikiri ni utaratibu gani utakuwa mzuri?


Senkoro: Kwanza sikubali kwamba hizi kampuni kubwa zinahodhi hizi sehemu za uchimbaji madini. Wanapewa leseni mahali fulani ili washughulikie mambo yao. Haiwezekani wakachukua eneo dogo ni lazima wapate eneo kubwa.
Kwa kawaida sehemu hizo hasa wachimbaji wadogo wadogo wanazinyemelea kwa sababu zimethibitishwa zina madini. Ukiangalia kwa kuzingatia utafiti, nchi yetu ina baraka kubwa za kuwa na madini, kwa nini huyu mwekezaji mdogo asiende maeneo mengine….zipo sehemu nyingi.
Wachimbaji wakubwa waliopo, haya makampuni makubwa kutokana na maeneo wanayomiliki ya kuchimba dhahabu, wanachimba asilimia nne tu ya hifadhi yote ya dhahabu nchini kwa mujibu wa tafiti za Wizara ya Nishati na Madini. Ipo asilimia 96 nyingine, ambayo mwekezaji yeyote kwenye madini anaweza kwenda kuomba leseni na kuchimba. Kwa nini wagombane katika nafasi za wawekezaji wakubwa wasiende kwingine?
Sasa ikiwa asilimia nne tu ndiyo inayochimbwa kwa nini ugombane na mwenzako usiende kutafuta ya kwako na sehemu zipo? Hizi ndizo hoja zangu mbili, moja kutokana na urahisi wachimbaji wadogo wanataka penye urahisi kumnyemelea mwekezaji aliyepo lakini pili hata kama mkubwa mwingine au mdogo, ilimradi mchimbaji aliyepo leseni yake haijaisha aachiwe aendelee kwa sababu maeneo ya kuchimba Tanzania ni mengi.


Raia Mwema: Wafanyaje sasa ili hao wachimbaji wadogo wakue?


Senkoro: Wachimbaji wadogo wana matatizo sana kutokana na Serikali kutokuwa na sera thabiti ya kuratibu na kudhibiti na kusaidia shughuli zao.
Wachimbaji wadogo wamekuwa na matatizo kutokana na Serikali kutowashirikisha wachimbaji wakubwa kikamilifu jinsi gani ya kuwasaidia wachimbaji wadogo.
Wachimbaji wakubwa wako tayari kufanya kazi na Serikali kuwasaidia wachimbaji wadogo hasa katika suala la elimu na kiteknolojia, lakini nadhani Wizara haijafika huko, inatakiwa ijenge uwezo kuwa na kitengo maalumu cha kusaidia wachimbaji wadogo na hicho kitengo kishirikiane na haya makampuni makubwa waangalie ni jinsi gani wanamsaidia mchimbaji mdogo.
Wachimbaji wadogo leo wanachimba lakini hawana soko, bidhaa ambazo ni dhahabu au almasi zao wanauza mkono kwa mkono, sasa huyu anayemuuzia anamnyonya tu. Kwa hiyo, tungewasaidia kwa elimu, teknolojia na hata soko.
Najua Waziri anafanya juhudi jinsi ya kusaidia lakini nadhani ni eneo linalopaswa kutazamwa kwa kipaumbele na umakini zaidi.


Raia Mwema: Hukifiri kwamba kuna haja ya kuwa na kiwanda chetu cha kusafisha madini badala ya kuuza madini ghafi?


Senkoro: Ni vizuri kuwa na kiwanda hicho, unakumbuka mwanzoni Williamson Diamonds ilikuwa na kiwanda Iringa…kiliitwa Tan-Cut. Lakini kilifika wapi, kilikufa kwa sababu kilikuwa hakiendani na design za soko. Walikuwa wanazalisha almasi fasheni ya mwaka 1947 na soko linataka fasheni ya leo.
Tulifanya huko nyuma tukashindwa. Kwa hiyo inategemea na aina ya madini. Kitu kama Tanzanite ni rahisi kuwa na kiwanda na hata almasi. Lakini kitu kama dhahabu inawezekana kwa kiasi fulani lakini ukizungumzia madini yote yanayozalishwa nchi haina uwezo kuyagaueza kwa kiwanda ili yasiwe ghafi. Kama dhahabu wengine wanahifadhi tu kama mche kwa sababu ni fedha.


Raia Mwema: Kuhusu umeme, ankara mnazolipa zinakuwa ndogo mno kuna tatizo gani, tunakosea wapi kama nchi?



Senkoro: Nimezungumza mwanzoni suala la miundombinu. Hilo nadhani ndilo tatizo kubwa linalowakabili wawekezaji Tanzania, wa nje na ndani.
Sisi kama Geita, na wachimbaji wengi….madini yanapatikana mbugani, ni mahali ambako miundombinu hakuna.
Umeme, maji na barabara hakuna, inabidi vitu vyote hivyo aidha taasisi za Serikali zikuletee au utengeneze mwenyewe. Sasa kwa upande wa umeme tuna matatizo mengi na migodi mingi inabidi izalishe umeme wake yenyewe. Sisi Geita tunazalisha umeme wetu, tunafanya hivyo kwa sababu hatujaunganishwa katika Gridi ya Taifa, tumeomba Tanesco bado hawajafanya. Hawana uwezo huo hata kama wanania, umeme wao ni mdogo.


Raia Mwema: Tunashindwa kuwa na uwezo huo? Kwa nini tusikope kama Tanesco au kama nchi?


Senkoro: Ninachoweza kusema kama nchi yetu Pato la Taifa ni dogo kwa hiyo kitu kama uwekezaji katika Tanesco au miundombinu mingine ni lazima kitafanyika kwa awamu. Hakuna uwezo wa ghafla kumaliza kila tatizo.
Lakini jambo ambalo lingeweza kufanyika, tena hata wakati fulani hawa wachimbaji wakubwa wa madini walikuwa na nia ni kuzungumza nao na kuangalia uwezekano wa kushirikiana na kuanzisha kampuni ya kuzalisha umeme megawati 100 au 200, hawa wawekezaji wakubwa wakiwa wachangiaji ili umeme huo mwingine uende kiwandani na hasa kwa kutumia gesi na uwezekano wa kuzalisha upo na mazungumzo yalikwisha kufanywa.
Umeme huo utakidhi mahitaji ya kiwanda na mwingine usambazwe kwa wananchi. Hili linawezekana kama tukitumia gesi, lakini vinginevyo tutakuwa na matatizo yasiyokuwa na sababu.


Raia Mwema: Una ushauri gani kwa Watanzania wenzako kuhusu madini tuliyonayo kama ulivyosema dhahabu inachimbwa katika eneo la asilimia nne tu, 96 bado?


Senkoro: Nadhani suala la madini hasa dhahabu tusiwe na jazba. Madini hasa dhahabu, yanataka fedha nyingi sana. Kama Geita kuna kama bilioni zaidi ya 600 zimewekezwa huko. Faida kwenye madini haipatikani mwanzoni, inapatikana baada ya mgodi kukomaa. Baada ya mgodi kulipa gharama zote kama mikopo.
Kwa hiyo ushauri wangu kwa Watanzania wenzangu ni kwamba tuwe na subira, hilo wanalosema kuna ndege zinakuja usiku zinaingia zinabeba dhahabu si kweli, haiwezekani. Ndege haiwezi kuingia Tanzania na rada zote zilizopo bila kibali.
Madhambi hayo yanayozungumwa wakati mwingine ni kutoelewa. Kwa upande wa Serikali waelemishe watu, na hata wawekezaji wana jukumu kubwa la kuelewesha wananchi.
Naweza kusema leo madini usafirishaji wake nje tangu tufungue sekta hii kwa wachimbaji binafsi, uuzaji wa madini nje ya Tanzania umepanda hadi Dola 860 bilioni ambayo ni zaidi ya asilimia 40 ya bidhaa za Tanzania zinazouzwa nje, na hii tunazungumzia asilimia 4 tu ya eneo la madini linalotumika.
Tukienda asilimia 10, 20 au 50 itakuwaje? Kwa hiyo kwa uzoefu wangu, madini ni rasilimali muhimui na kubwa inayoweza kubadilisha uchumi wa nchi, tuwe na subira tuzidi kuwa na wawekezaji kama alivyosema Rais tuwe na win-win, lakini baadaye tutapata faida kubwa.
 
Back
Top Bottom