Hati ya mashtaka isiyotaja kosa ni batili!

sulphadoxine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,257
645
Hati ya mashtaka ndiyo inayoanzisha rasmi mashtaka dhidi ya mshtakiwa yeyote wa makosa ya jinai.Hati hiyo hutayarishwa kwa msingi wa kisheria ambapo lazima izingatie masharti kadhaaa muhimu
 
Hebu tuanze kwanza kwa kuzungumzia sheria inasemaje kuhusu "Hati ya Mashtaka" au "Taarifa ya Mashtaka". Taarifa ya Mashtaka haina tofauti za kimsingi na Hati ya Mashtaka isipokuwa katika uandishi wake ambapo hueleza wazi kuwa mahakama inaarifiwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwamba mnamo tarehe fulani mshtakiwa atashtakiwa kwa kosa fulani.

Tofauti hizo zinatokana na maelekezo ya kisheria kwamba kuna baadhi ya makosa ambayo husikilizwa na Mahakama Kuu tu ambayo ndiyo yenye uwezo wa kufanya hivyo, kwa mfano uhaini na mauaji. Kwa hiyo taarifa za mashtaka hutumika kwa kesi za jinai za Mahakama Kuu. Hata hivyo masharti yote ya uandaaji wa hati ya mashtaka yanahusu pia utayarishaji wa taarifa ya mashtaka.
 
Sharti moja muhimu katika uandishi wa hati ya mashtaka au taarifa ya mashtaka ni kuwa kwanza lazima itaje kosa na maelezo ya kosa analotuhumiwa kulitenda mshtakiwa. Hii ni kwa mujibu wa matakwa ya kifungu cha 132 cha SHERIA YA MWENENDO WA MASHTAKA YA JINAI YA MWAKA 1985 [Sura ya 20 ya Mapitio ya 2002] maarufu "CPA". Mfano, kama kosa ni la wizi maelezo ya hati ya mashtaka yataeleza hivyo na kifungu husika cha sheria.

Wakati mwingine katika hati ya mashtaka kunakuwa na maelezo ya kosa fulani kwa kifungu fulani cha sheria na adhabu yake kutolewa na kifungu kingine cha sheria. Mfano ni wizi ambao hufafanuliwa katika kifungu cha 258 ambapo adhabu huelezwa katika kifungu cha 265 cha SHERIA YA KANUNI YA ADHABU, SURA 16. Hivyo ni makosa kwa hati ya wizi kutoa maelezo ya kosa kwa mujibu wa kifungu cha 258 badala ya kifungu cha 265.
 
Je vipi kama kuna zaidi ya kosa moja kwa mfano wizi na mauaji hati ya mashtaka hapo inasemaje
na je kama mshatakiwa ametenda makosa zaidi ya moja na katika siku na tarehe na mahali tofauti hati ya mashtaka inasemaje
Na je kama washtakiw ani zaidi ya mmoja walishiriki inakuwaje hati ya mashtaka
na je kosa kama la wizi na mauaji ni kosa lipi litakuwepo kwenye hati ya mashtaka maana kosa kubwa hapo ni mauaji
na je hati ya mashtaka ikiwa deffective inakuwaje
 
Back
Top Bottom