Hati miliki ardhi Tanzania za kitapeli kabisa zinaleta umaskini

RICHEST

Member
Jun 23, 2011
25
16
Hebu ona unapewa hati miliki ya ardhi ambayo inatambua kitu kilicho juu ya ardhi mfano jengo na mazao na maendelezo uliyofanya juu ya ardhi.Umiliki huu umetia umaskini watanzania. Hati miliki bora ya ardhi ni ile ambayo ingekuwa inatambua unamiliki ardhi ikiwa na maana unamiliki kila kitu kilicho chini ya ardhi kilometa kadhaa kwenda huko chini na kilomita kadhaa kwenda huko angani usawa wa kiwanja chako au shamba lako.

Hii ina maana kama madini yakigundulika chini ya kiwanja chako au mafuta ni mali yako na fidia wakikuhamisha izingatie na madini yaliyovumbuliwa chini kwenye kiwanja.

Vinginevyo hati hizi miliki za Ardhi za TANZANIA ni hati sawa na za kumiliki vumbi lisilo na maana lililo juu ya Ardhi.Wakazi wa maeneo ya madini wangekuwa na hati miliki zinazotambua ardhi kuwa ni pamoja na vile vilivyo chini kwenye kipande chako cha ardhi unachomiliki leo wangekuwa matajiri wa kutupwa maana makampuni ya madini ingebidi yawalipe fidia mabilioni au wawape hisa wamiliki.

Wabunge wapiganie sheria ya ardhi ibadilishwe wakitaka watanzania wawe matajiri kupitia ardhi.Wengine waliozoea kukariri vitabu na kuiga viinchi vingine watakuja kunipinga wakisema nchi zilizoendelea hakuna sheria kama hizo hakuna.Jibu ni kuwa Sisi si lazima tuige wengine. Kwani hatuwezi kuanzisha KIPYA wengine wakafuata? si lazima tu kopi sheria za uingereza,india wala marekani twaweza ibuka na sheria yetu we
 
Ni ideal nzuri yaani sisi tuwe kama testing ya wengine,lakini nafikiri ukiwa na hati miliki na kama hapo chini ya ardhi kuna madini wakitaka kukuamisha lazima wanigotiate na wewe wakitaka kuichukua kwa nguvu unahati ambayo itakulinda kisheria,otherwise raisi wa nchi aicancel hati yako.
 
Wengine waliozoea kukariri vitabu na kuiga viinchi vingine watakuja kunipinga wakisema nchi zilizoendelea hakuna sheria kama hizo hakuna.Jibu ni kuwa Sisi si lazima tuige wengine. Kwani hatuwezi kuanzisha KIPYA wengine wakafuata? si lazima tu kopi sheria za uingereza,india wala marekani twaweza ibuka na sheria yetu we

Hii nimeipenda sana kwa kweli. Kiukweli kuna watu huwa wananikera sana, maana unakuta mtu unamwambia kitu halafu anakwambia hakuna kitu kama hicho duniani kama vile sisi hatuwezi kuanzisha chochote na wengine kufuata.
 
Back
Top Bottom