Hatari ya nchi yetu kumeguka vipande vpande inaweza kuzuilika na watawala

Mghaka

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
320
127
Siyo siri tena kwamba hali tuliyoizoea ya kujiona wamoja katika nchi yetu sasa wanasiasa wamo mbioni kuibomoa na kuingamiza ili wao waendelee kustawi katika mgawanyiko huo. Si usalama wa taifa au walinzi wetu wa kutumainiwa ambao wanaweza kusema hili hapana na kuwashauri watawala wasimamie ukweli uliowaweka madarakani kwa kuzingatia viapo vyao.

Tuliishi bila kujipima katika mizani ya imani za kidini sasa tunayaona hayo, tuliishi katika mizani ya usawa na kupeana majukumu bila kuulizana dini sasa mpaka baadhi ya nyaraka za kuuliza taarifa binafsi za mtumishi, dini ni kigezo tunakwenda wapi wajameni? Tulizoea kuishi katika mizani yenye kuzingatia ujuzi na ufanisi kama vigezo vya kuwatumikia watanzania sasa hata Mamlaka za uteuzi serikalini zikifanya kazi yake ya uteuzi watu wanauliza nani ni dini gani na nani ni nani? Tumetoka huko sasa tunauliza je wakati wa mchakato wa uchaguzi alikuwa kambi gani, tunachelea kutambua kuwa kipindi hicho ilikuwa ni katika kutekeleza matakwa ya kikatiba yetu hata kama tunaibeza kuwa inamapungufu kwa sasa. Tumeruhusu mbegu za chuki kuendelea kutuongoza katika kufanya maamuzi. Tumewapa nafasi watu wenye chuki na maslahi binafis jukwaa la kuufikia umma kupanda mbegu za chuki na tumenyamazia uovu na uozo huo na sasa tunaona matunda yake tumeanza kuyala kwa gharama kubwa na si haba gharama hiyo muda si mrefu itakuwa damu yetu.

Wale tunachukizwa na hali hii bila kujali imani zetu tujitenge na tupaze sauti ya kupinga uovu huo na kwa kuanza niseme machache ambayo watawala wanapaswa kuyasimamiakwa sasa

  1. wakubali kushindwa na wawe tayari kupokea maamuzi ya watanzania hata kama maamuzi hayo yanapingana na matakwa yao
  2. Tusisubiri matokeo ndio tuamke kufanya majukumu yetu, ziko redio, mihadhara na vikundi ambavyo vinatengeneza jukwaa la machinjio ya roho za watanzania kama si kesho basi ni wakati wowote ambao hakuna ajuaaye isipokuwa Mola mwenyewe
  3. tuharakishe kutengeneza maadili ya kitaifa na miiko ya vyama vya kisiasa kupitia mjadala wa kitaifa ili tutoe nafasi kwa umma kuyapa uhalali wake na baadaye tuyawekee nguvu ya kisheria kazi hii si ya msajili ambaye nae pengine anaangaliwa kwa mashaka na baaadhi ya wahusika wakuu
  4. tuandani uwanja bora wa ushindani na kuwashughulikia wanaopindisha kanuni za uchaguzi kwa kutoa hongo tatizo hili ni kubwa kwa chama tawala

Karibu tushiriki katika kujenga nchi yetu kila tone la damu lazime lilindwe pasitokee mtu kusababisha umwagikaji wake kama gharama yake si ununuzi wa haki

Tanzania yetu ni moja na ibaki hivyo hivyo


 
Back
Top Bottom