Hatari ya chama legele,serikali dhaifu na bunge zembe kwa mustakabali wa amani yetu

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Ni mara nyingi nimekuwa nikizungumzia chombo hiki cha bunge kwa kushinda kutekeleza majukumu yao kikatiba ya kuisimamia serikali na kuwa chombo cha kusimamia na kutekeleza yale yanayo fanywa na baraza la mawaziri.Ukiwa na bunge la namna hii hatari yake ni nchi kupoteza sifa na wajibu wa serikali katika kusimamia ustawi wa wananchi.

Wakati mwingine nashindwa kujua makosa ya bunge letu huwa yanafanywa makusudi au nafasi ya party caucus ina kuwa kubwa na kutekelezwa zaidi kuliko maamuzi ya bunge zima.Ikiwa bunge liliazimia mawaziri wake kujiuzuru,hapo hapo wanasimama wabunge wa bunge hilo hilo na kunadi maamuzi hayo yalikuwa ya party caucus kuna haja gani kuwa na bunge ambalo lisilojua wajibu na nafasi yake ya kibunge.


Maamuzi mengi yamekuwa yakitekelezwa kwa msingi wa kiitikadi zaidi kuliko maslahi ya wananchi.Leo bunge limegawanyika sehemu mbili,wabunge wa CCM wanasimama kwa maslahi ya chama na wabunge wa upinzani wanao simama kwa maslahi ya wananchi.Athari yake ni kutungwa kwa sheria chovu zenye kubeba dhana ya maslahi binafsi na kusababisha anguko la uchumi wetu kutokana na wingi wao bungeni,sababu inayosababisha kupitishwa kwa sheria zenye kuwabeba watawala zaidi kuliko kuangalia maslahi ya taifa kwa ujumla.

Kitendo cha bunge hili kugeuzwa sehemu ya malumbano yasiyo na tija kwa wananchi yameshusha hadhi ya bunge hili,kwa kuonyesha udhaifu ambao wananchi wasipokuwa makini hata huo mlo wa siku moja unao patikana kwa siku utakuwa taabu.Uzembe aliousema JJ Mnyika ndio uliosababisha nchi kuwa omba omba na kushindwa kujisimamia hata katika mambo ya maendeleo yake binafsi.Upuuzi wa chama tawala katika kuendesha nchi ndiyo uliyopelekea kuzalisha serikali legelege na bunge zembe.

Kwa mantiki hii basi,tutegemee taifa legelege lenye serikali dhaifu na bunge zembe ambalo isipotumika busara ya hali ya juu kuinusuru hali hii, ipo siku nchi itageuka Tunisia na kwingineko kote ambako walichoka kuwa na serikali na bunge la aina yetu ambalo halijali maslahi ya wananchi wake.
 
Back
Top Bottom