HATARI: Vifaa vibovu vya kupima UKIMWI & Malaria vyatumika Tanzania

Ndio maana malaria Tanzania haiishi.....! Kuna siku nilijaribu kupima vituo vya afya vitatu, Cha kwanza niliambiwa na malaria 4, nikaenda cha pili wakakuta malaria 3, nikaenda kingine nikaonekana sina malaria.

Ukienda dispensary ya UDOM hawana historia ya kukuta mwanafunzi ana Maralia hata kama upo mahututi kutokana na maralia.,kumbe walikuwa wanalaumiwa bure ma Dk wa pale kumbe tatizo ni vifaa feki...
 
mimi ni mdau katika sekta ya afya,vipimo vya malaria alivyovitaja mleta uzi ni aibu kwa wizara ya afya! Hebu jiulize: wagonjwa 518 waliopimwa mwezi Nov.kituoni kwangu ni wagonjwa 3 tu walioonekana wana malaria kwa mujibu wa vipimo hivyo! Ajabu nyingine huyu mfamasia wetu ni mwizi nouma wa vifaa lakini madude haya ya malaria bado yamejaa stoo dalili kwamba hayauziki kwa Wakongo!
 
Kiukweli Tanzania ni shamba la bibi mambo mengi yamefanyika na yatafanyika mpaka tutakapo amua sote kwa pamoja kupaza sauti zetu... Swali moja hivi ni nani anayefahamu kwamba piki piki za matairi matatu (ambulance) ambazo zilipigiwa chapuo kama Power Tiller zinaozea pale EPI??
Jamani kama Mh. JK aliingizwa mkenge kwenye pikipiki ambazo zinaonekana bila kutumia darubini sembuse eti vipimo ambavyo wataalamu wanaoongea at very profile level juu ya efficiency, effectiveness, validity and specificity?
Kumbuka Samaki wa mionzi tumekula na bado tunadunda..... ahaaa Tanzania zaidi tuijuavyo.
 
Mkuu, ngono si njia pekee ya maambukizo na je, malaria pia huambukizwa kwa ngono? Maana vifaa vya kupima malaria pia ni vibovu. Hapa issue si ugonjwa ni UFISADI wa kutumia afya za watu, kama vifaa havina maana (kwa mawazo yako), basi serikali isiagize, iagize chakula!
MM hao ndio watanzania akili zao sijui zikoje hapo kinachozungumzwa ni juu ya vifaa halafu mtu anakurupuka na kusema watu waache ngono,sijui kama malaria nayo inaletwa na ngono,hapa tatizo ni matumizi ya vifaa na sio nini kifanywe kupunguza magonjwa,watanzania ni sawa na kumpigia gitaa mbuzi,hasa ufisadi unapojadiliwa watu huwa wakali kweli na kutoa pumba nyingi
 
Mwanakijiji
Wanaoathirika ni wananchi, mfumo mzima wa serikali umetawaliwa na ufisadi, kumbuka watendaji wa serikali wao wameshaamua moja UFISADI watatafuta kila njia ili waibe hili la kuleta vipimo ambavyo ni vibovu waathirika ni sisi wananchi ndipo niliposema tukazanie elimu ya afya ya jamii; hili la ufisadi dawa yake ni kuchagua viongozi wenye kuwajibika kwa wananchi; vinginevyo naunga mkono kauli yako.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
MM hao ndio watanzania akili zao sijui zikoje hapo kinachozungumzwa ni juu ya vifaa halafu mtu anakurupuka na kusema watu waache ngono,sijui kama malaria nayo inaletwa na ngono,hapa tatizo ni matumizi ya vifaa na sio nini kifanywe kupunguza magonjwa,watanzania ni sawa na kumpigia gitaa mbuzi,hasa ufisadi unapojadiliwa watu huwa wakali kweli na kutoa pumba nyingi

Mfianchi.
Ni hivi hili suala unaweza kulijadili kwenye sehemu mbili
1. Ubadhirifu/ufisadi
2. Afya
Mimi nimeona nijadili kwenye hizo athari ya kutumia vyombo vibovu kwenye kupimia afya za wananchi; ndipo niliposema tukazanie elimu ya jamii, kama unajua namna ya kujikinga na ukimwi na malaria utakuwa na haja gani kwenda kupimwa kwa kutumia vyombo vibovu? Inawezakana mzee hilo la ngono limekugusa sana maana sikuishia kwenye ngono tu! Ukimwi ni janga linalotukabili na hauna tiba kuwa mwangalifu.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
mimi ni mdau katika sekta ya afya,vipimo vya malaria alivyovitaja mleta uzi ni aibu kwa wizara ya afya! Hebu jiulize: wagonjwa 518 waliopimwa mwezi Nov.kituoni kwangu ni wagonjwa 3 tu walioonekana wana malaria kwa mujibu wa vipimo hivyo! Ajabu nyingine huyu mfamasia wetu ni mwizi nouma wa vifaa lakini madude haya ya malaria bado yamejaa stoo dalili kwamba hayauziki kwa Wakongo!

wewe ni nesi,daktari,mganga au mpishi hospitalini.maoni yako hayaonyeshi kama wewe ni mtaalamu katika sekta ya afya.
 
ni mpishi tu mkuu! Kuna watu Tanzania hii ili upate salam yake lazima uwe na Phd...kibaya zaidi mtu huyo amevaa hirizi ya kumkinga na wabaya wake. Nadhani u miongoni mwao.Hata mgonjwa ni mdau tu mkuu.
 
Mwanakijiji
Kipimo sahihi ni watanzania kuelemishwa kuachana na mambo ya ngono tu; elimu ya afya itiliwe mkazo, nchi nyingi duniani zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza maambukizo kwa kutumia afya ya jamii; na viongozi wamekuwa mstari wa mbele kwenye vita hivyo.

Chama
Gongo la Mboto DSM

Ningekuelwa sana kama ungesema 'Kinga' badala ya kipimo, Bahati mbaya sana Ukimwi hauna 'kinga'. Maana kazi ya kipimo si kukinga bali ni kubaini uharibifu uliopo ambao hupelekea kutafuta mbinu za kuutibu huo uharibifu.

Ukimpima mtu na kumwambia mgonjwa kutokana na vipimo vibovu na kuanza kumpatia dawa ambazo hazihitaji ni sawa na kumpatia sumu, na ukimpima mtu ukamkuta mzima wakati ni mgonjwa kwa ubovu wa vipimo ni sawa na kumpatia kibali cha kufa mapema kwa kumyima matibabu.

Tanzania hatuna utamaduni wa kuthamini maisha ya wananchi. Public safety is not a priority in Tanzania unless it is connected to political motive like Alshabaab threats to curb oposition demonstrators.

Kuna wakati mtu mmoja aliwahi kuniambia kuwa wizara ya afya imejaa wagonjwa wa HIV. Unapokuwa na watu walioathirika na kuwapatia nafasi ya kuwalinda walio wazima inakuwa ni ngumu sana hasa kwa ubinafsi wetu wanadamu wa kitanzania. Kenya wao wamepewa barua na WHO kuhusu vifaa hivi na wamechukua hatua ya kuvirudisha na kuvi skip vyote. Sisi tunaangalia pesa na hasara zaidi ya maisha ya binadamu. Huyo aliyekalia taarifa hii hastahili kuwa mganga mkuu wa nchi.
 
Mkuu, ngono si njia pekee ya maambukizo na je, malaria pia huambukizwa kwa ngono? Maana vifaa vya kupima malaria pia ni vibovu. Hapa issue si ugonjwa ni UFISADI wa kutumia afya za watu, kama vifaa havina maana (kwa mawazo yako), basi serikali isiagize, iagize chakula!

You have been in US for too long and you are forgetting how things work in Tanzania, they work by not working. Ukija nenda Muhimbili uone panavyonuka, hutaamini kama ile ni hospitali, nenda Mwanyamala hospitali au Temeke, Ilala n.k. usiombe kuingia kwenye labs. Sehemu kubwa ya dawa zinazouzwa kwenye pharmacy uwezeo wake wa kutibu ni 40% ikilinganishwa na OTC za nchi nyingine zenye drug administration department.

The fact is Afya za watu ni mtaji wa watu kujinufaisha, hata useme otherwise. Ukiwauliza wanasiasa watapiga porojo tu, mambo yataendelea. Unatakiwa kujiuliza kwanini Malaria mpaka leo inaua, na inaweza kutibiwa kwa chini ya dola 10.
Tunavyolalamika kuwa nchi yetu hovyo, we know what we mean.
 
hili suala ni la kushtua mno kwa sababu limegusa sehemu nyeti kwenye sekta ya afya.ukweli upimaji wa ukimwi ni jambo linalotakiwa kufanywa kwa umakini wa hali ya juu sana.kumuambia mtu ana ukimwi wakati hana huleta gharama au athari kwa mgonjwa,ndugu wa mgonjwa,daktari anayemuhudumia na serikali kwa ujumla.
inasikitisha mganga mkuu kiongozi,mkuu wa kitengo cha uchunguzi,mkurugenzi MSD,wahusika wa manunuzi ya dawa/vitendanishi,mkurugenzi NACP(National Aids Control programme) kukaa kimya kuhusiana na suala hili.ni kwa nini watu hawa wamekaa kimya?kama walikuwa wanaogopa kuwashtua wananchi, je walitoa taarifa kwa waganga wakuu wa mikoa ili nao wawape tahadhari madaktari na manesi kuhusiana na accuracy ya vipimo hivi?...................kwa kweli uwajibikaji wa wataalamu umepungua sana,tunapoelekea ni pabaya mno......

maoni yangu kwa wanajf
upimaji wa virusi vya ukimwi unaratibiwa kwa umakini wa hali ya juu.na vipimo hivi vya SD Bioline ni vipimo vya kuchuja(screening test) hivyo mtu hawezi kuambiwa ameathirika kwa matokeo ya kipimo hiki pekee,iwapo kipimo hiki kikisoma +ve mtu huyo hufanyiwa kipimo cha pili (determine) ili kuthibitisha au kuendelea na mlolongo mwingine wa vipimo.hivyo sio rahisi kihivyo kwamba mtu akisemekana ni muathirika baadaye ikawa sio.kwa upande mwingine mtu hawezi kuambiwa hajaathirika iwapo SD bioline imesoma -ve,atatakiwa kurudia vipimo hivyo baada ya miezi mitatu huku akipewa ushauri wa kujikinga na maambukizi.sina maana makosa hayafanyiki lakini sio kweli kwamba makosa ni mengi.siwatetei wizara ya afya kwa uzembe huu lakini sipendi kuona suala hili linakuzwa kisiasa kwa sababu matokeo ya kufanya hivyo ni hatari zaidi.wizara na wote wanaohusika wanapaswa kuwajibika hasa kwa kutofanyia kazi kwa wakati ushauri kutoka WHO.

tufanye nini?
watendaji wanaohusika watoe tamko la kitaalamu kuhusiana na sakata hili(sio tamko la kisiasa),taarifa hii ilenge katika kuwatoa hofu wananchi.

wizara ya afya itoe maelekezo kwa wadau wote wa afya kuhusiana na sakata hili na pia watoe maelekezo ya nini kifanyoke kwa sasa(kama WHO walivyofanya)

wahusika wote (wizara ya afya) hasa watendaji wawajibike au wawajibishwe.

tuombe msaada wa ushauri wa kitaalamu kutoka WHO au nchi nyingine zilizoathiriwa na tatizo hili.
 
Back
Top Bottom