HATARI HII: UDOM Walitaka kulipua Chuo- Prof. Kikula

Ingekuwa bungeni , prof angetakiwa kuthibitisha pasipo shsks kauli yake, Hapa imekaaje. ADIBITISHA PASI NA SHAKA
 
kama kweli hii hatari ila tunaomba ushahidi wa hili,ili tujue kama vijana wamekuwa tayari kwa mpambano tuwaunge mkono,tumechoka tumechoka jamani
 
Nchi ikiwashinda mnawalaumu Chadema. Ni sawa na msemo wa Makamba wa mbaazi ikikosa mauwa hulisingizia jua
 
Jana ktk taarifa ya habari ya radio mwangaza ya saa 1 usiku nilimsikia Prof. Kikula akiwaambia wakuu wa wilaya waliokuwa wametembelea chuo hicho kuwa wanasiasa wasimshinikize kuwarudisha wanafunzi hao kwani anazo taarifa kuwa walitengeneza mabomu ya petroli ili kupambana na Polisi endapo wangekwenda kuwatawanya kwa nguvu hivyo kungepelekea chuo kulipuliwa na kuwaka moto.

Na lazima watakuwa wafuasi wa MAGWANDA, kwani ile rangi nyekundu ndio maana yake ya mauaji, vurugu, fujo nk. Wafukuzwe tu ndio malipo yakumfuata kilaza Lema. Haya sasa Magwanda mmeona faida yake
 
Kama walichukua visu vya kumenyea machungwa (OMARY MAHITA 2000) wakasema et Cuf ni chama cha magaidi unafikiri wanashindwa kusema hayo??!
 
Na lazima watakuwa wafuasi wa MAGWANDA, kwani ile rangi nyekundu ndio maana yake ya mauaji, vurugu, fujo nk. Wafukuzwe tu ndio malipo yakumfuata kilaza Lema. Haya sasa Magwanda mmeona faida yake
akil mgando ndo zakutuma,mwambie shoga mwenzio alete ushahid so ushoga.vp leo ukiambiwa mie mmeo?
 
akil mgando ndo zakutuma,mwambie shoga mwenzio alete ushahid so ushoga.vp leo ukiambiwa mie mmeo?
mkuu mbona matusi mengi?hapa 2nakosoana kistaarabu bt co kwa jazba na matusi,take bow plz..
 
mkuu mbona matusi mengi?hapa 2nakosoana kistaarabu bt co kwa jazba na matusi,take bow plz..
njoo uwe sawa il kukutoa tongotongo za uzembe,mwiz rafikie mwinzie.hakuna tus ila maneno makal il uache akil za nyumbu na ushabik wa kizembe take care kimwana
 
Jana ktk taarifa ya habari ya radio mwangaza ya saa 1 usiku nilimsikia Prof. Kikula akiwaambia wakuu wa wilaya waliokuwa wametembelea chuo hicho kuwa wanasiasa wasimshinikize kuwarudisha wanafunzi hao kwani anazo taarifa kuwa walitengeneza mabomu ya petroli ili kupambana na Polisi endapo wangekwenda kuwatawanya kwa nguvu hivyo kungepelekea chuo kulipuliwa na kuwaka moto.
Kauli ya makamu mkuu huyo iliungwa mkono na wakuu hao wa wilaya ambao walitaka uongozi wa Udom usiwarudishe kirahisi wanafunzi hao ili wajifunze kwanza kuwa walichofanya hakikuwa kizuri.“Tena mkianza kuwarudisha rudisheni wana-CCM, hao wa Chadema achana nao maana ndio wanaoanzisha vurugu na uvunjifu wa amani hawana shukrani hao hata siku moja na wala hawajui kutoa fadhila zaidi ya kulalamika kila kitu,’’ alisikika akisema mmoja wa wakuu hao wa wilaya.Hivi hawa wakuu wa Wilaya zetu zimo kweli jamani? hiyo ni pointi yakuongea na wenzio wakusikileze? inamaanisha chuo ni cha waccm tu na sio vyama vingine? Tusiingize mambo yasiasa, kwenye haki. Huyo atakuwa kilaza na inabidi achunguzwe zaidi. refer MWANANCHI 27.6.2011
 
Nakubaliana na Prof Kikula, hizo habari ata mimi nimezisikia kutoka kwa mwanafunzi mmoja ambae kasimamishwa chuo! Inasemekana ni maagizo kutoka kwa Lema

Dah sijaelewa vizuri kama umeandika wewe kwa utashi wako au kuna mtu alikua nyuma yako akikushurutisha kuandika hayo uliondika! hivi na wewe kabisa unaingia kwenye 'story' za kijiweni? kama mambo ndivyo yalivyokuwa, mbona hukupeleka taarifa kwa wahusika?ungesaidia sana wale wanafunzi wasirudishwe nyumbani ilhali 'mbaya' anajulikana. think globally before you speak, one day utafungwa. Chunga sana!!!!
 
Kwenye red
Nashauri pindi wanafunzi wakirudishwa nyumbani kwa maana ya kufunga chuo, walimu na viongozi wa chuo nao wapelekwe likizo isiyo na malipo hadi chuo kitakapofunguliwa. Kama wapo kufundisha na wanafunzi hawapo kwa nini waendelee kulipwa?

Niliwahi kuwa mwalimu wa pale Mlimani UDSM, na kati ya mwaka 1989 na 1990, chuo kile kilikuwa kimefungwa kwa mwaka mzima wa masomo eti kwa vile wanafunzi walim-punch mzee Mwinyi. Sasa katika kipindi hicho sisi waalimu na wafanyakazi wote wa chuo ikiwa ni pamoja na wafagia madarasa na wapishi wa kafeteria tukaendelea kuwa tunalipwa mafao yetu wakati chuo hakina wanafunzi. Kila nikikumbuka mwaka huo natamani kurudisha mshahara ule niliopewa kwa mwaka mzima bila kufanya kazi yoyote; huo ulikuwa ni wizi wa pesa za alipa kodi kabisa!

Tujikumbushe tena kuwa Chuo kinaundwa na wanafunzi pamoja na waalimu. Bila kundi mojawapo kati ya hayo mawili kunakuwa hakuna chuo. Wafanya kazi wote wa utawala pamoja na VC wako pale kuwatumikia waalimu na wanafunzi. Sasa iwapo VC anawafukuza wanafunzi basi na hata wafanyakazi wa utawala pamoja na wasilipwe chochote kwa sababu kunakuwa hakuna chuo tena.
 
Jana ktk taarifa ya habari ya radio mwangaza ya saa 1 usiku nilimsikia Prof. Kikula akiwaambia wakuu wa wilaya waliokuwa wametembelea chuo hicho kuwa wanasiasa wasimshinikize kuwarudisha wanafunzi hao kwani anazo taarifa kuwa walitengeneza mabomu ya petroli ili kupambana na Polisi endapo wangekwenda kuwatawanya kwa nguvu hivyo kungepelekea chuo kulipuliwa na kuwaka moto.
Chuo cha UDOM siku hizi kinafundisha ulipuaji wa mabomu? je kunauchunguzi wowote ambao umebainisha kama wanachuo hao wametengeneza hayo mabomu na kama imejulikana hatua gani zimechukuliwa zidi yao? au ni kukurupuka tu na kuingiza siasa za maneno pasipo vitendo? kinachohitajika hapo ni wanafunzi kupewa haki yao tu ndicho kitu cha msingi na sio visingizio eti walitaka kutengeneza mabomu. Wanafunzi wapewe haki yao na chuo kifunguliwe kama uchunguzi ukifanyika basi sheria ichukue mkondo wake sio kukurupuka tu na maneno yakuambiwa au kusikia ni kutaka kuzima jitihada za wanafunzi kupata haki yao.
 
Dah sijaelewa vizuri kama umeandika wewe kwa utashi wako au kuna mtu alikua nyuma yako akikushurutisha kuandika hayo uliondika! hivi na wewe kabisa unaingia kwenye 'story' za kijiweni? kama mambo ndivyo yalivyokuwa, mbona hukupeleka taarifa kwa wahusika?ungesaidia sana wale wanafunzi wasirudishwe nyumbani ilhali 'mbaya' anajulikana. think globally before you speak, one day utafungwa. Chunga sana!!!!
nakubaliana nawewe kabisa mkuu watu wengine wametumwa humu JF kuwakilisha mtu fulani, maneno yakusikia vijiweni sio yakukurupuka nayo watu wengine mawazo finyu.
 
Nakubaliana na Prof Kikula, hizo habari ata mimi nimezisikia kutoka kwa mwanafunzi mmoja ambae kasimamishwa chuo! Inasemekana ni maagizo kutoka kwa Lema
Peleka unafiki wako kule, Lema hawezi kuwa kichaa namna hiyo. Hao ni watu wa usalama wa Taifa na fitna zao wanajitia wanafunzi kumbe wapo kazini wakijitahidi wafanye madudu ili ionekane chuo hicho kimeingiliwa na siasa hususani CDM.
 
Nakubaliana na Prof Kikula, hizo habari ata mimi nimezisikia kutoka kwa mwanafunzi mmoja ambae kasimamishwa chuo! Inasemekana ni maagizo kutoka kwa Lema
Mambo yakusikia wapi na wapi? ulichukua hatua gani baada ya kusikia au ndo umempa prof. taarifa? becareful na mambo yakijiweni utafungwa.
 
Jana ktk taarifa ya habari ya radio mwangaza ya saa 1 usiku nilimsikia Prof. Kikula akiwaambia wakuu wa wilaya waliokuwa wametembelea chuo hicho kuwa wanasiasa wasimshinikize kuwarudisha wanafunzi hao kwani anazo taarifa kuwa walitengeneza mabomu ya petroli ili kupambana na Polisi endapo wangekwenda kuwatawanya kwa nguvu hivyo kungepelekea chuo kulipuliwa na kuwaka moto.

Ama kweli CCM imefilisika kisera. Japokuwa wameamua kuingilia mambo ya mashuleni na kuacha siasa hili ni balaa kwao. Hii ni sumu kubwa sana katika jamii ya watanzania wa leo. Hapa ndio tunaona utendaji wa ccm ulivyo wa ovyo bila kufikiria madhara katika jamii inayoitawala. Kwanza wameshatuonyesha ni wabaguzi na wanaendelea kuhalalisha lile tabaka la alienacho na asienacho.

Kwa nini hawa wanachuo wasishirikiane wakampeleka huyu jamaa mahakamani, jamani watu ambao wanaweza kuwasaidia hawa vijana muwasaidie, tunajua dactari kama hajasoma kwa vitendo hawezi kufanya kazi ya kutibu au kutoa dawa.

Prof. Kikula hili la mabomu ni kitanzi umejifunga shingoni yaani mwezi umeisha ndio unawaambia jamii ya watanzania mambo ya kutunga, uongo, unafiki lakini tumesha wazoea kwa uongo nyinyi CCM.
 
Peleka unafiki wako kule, Lema hawezi kuwa kichaa namna hiyo. Hao ni watu wa usalama wa Taifa na fitna zao wanajitia wanafunzi kumbe wapo kazini wakijitahidi wafanye madudu ili ionekane chuo hicho kimeingiliwa na siasa hususani CDM.
Hilo ndio neno usalaa wa taifa wanataka kutawala nchi hii milele,ukweli ilipaswa mtu yeyote ambaye amepita usalama wa taifa asiwe mwanasiasa fikira akina Hassy Kitine, Mwang'onda jr, Jakaya Kikwete, Membe,nMkuchika,nChiliga, Zakhia Meghji, Mrema hawa watu wako madarakani wakati wanatumikia usalama wa taifa ndio maana nchi haiendi,kila wakati wananigiza propaganda za kutishia wananchi

Prof Kikula hataheshimika tena na jamii,hawezi kusema kulikuwa na mabomu ya petroli wakati hatuonyeshwa bomu lenyewe,hakuna mwanafunzi amekamatwa akitengeneza,halafu anaenda kuyasemea mambo ya wananfunzi kwa wnansiasa wa CCM this is ridiculous,ameshindwa kuongoza chuo aondoke aachie wengine
 
Back
Top Bottom