Hata wewe yanaweza kukuta

platozoom

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
9,364
11,150
Hivi juzi Nilikuwa napita mahali mara nikawaona wazee wawili wamesimama kimtindo kwenye kona ya nyumba (babu around 70s na bibi 60s) nikashikwa na udadisi nikabana karibu yao na kusikiliza maongezi yao:

Babu; jana nilikuita lakini hukuja
Bibi: mmh miguu ilikuwa inauma sana halafu wewe uwe usiwe unamtuma yule mjukuu wangu anaweza kujifunza tabia mbaya.
Babu; sawa lakini ujue nakupenda sana,nashindwa kuvumilia.Sasa lile ombi langu vipi?
Bibi; nilikwambia uwe mvumilivu nitakupa jibu
Babu; Muda mrefu unanizungusha,leo nipe tu jibu la kueleweka umri unakwenda na nguvu zinapungua
Bibi:Wewe hukumbuki nilipokuwa binti nilivyokuwa nakutukana ukiniiita?shukuru Mungu sasa hivi nakubali kuongea na wewe.Vumilia tu nitakupa jibu la kueleweka mvumilivu hula mbivu
Babu; (Huku akilengwalengwa na machozi) sawa...kama nimesubiria zaidi ya miaka arobaini..nitajitahidi tu kuvumilia.

Baada ya hapo ikabidi niondoke huku nikisononeka moyoni kwa namna babu alivyoppigwa tarehe,lakini pia nikajaribu kufanya comparison na namna kizazi chetu cha sasa kinavyotongoza......................!
 
Tazama signature yako lazima utakuja na thread kama hii.
 
Babu asije akafa hajaonjeshwa tamu ya bibi!!!!!!!!!!
Hivi juzi Nilikuwa napita mahali mara nikawaona wazee wawili wamesimama kimtindo kwenye kona ya nyumba (babu around 70s na bibi 60s) nikashikwa na udadisi nikabana karibu yao na kusikiliza maongezi yao:

Babu; jana nilikuita lakini hukuja
Bibi: mmh miguu ilikuwa inauma sana halafu wewe uwe usiwe unamtuma yule mjukuu wangu anaweza kujifunza tabia mbaya.
Babu; sawa lakini ujue nakupenda sana,nashindwa kuvumilia.Sasa lile ombi langu vipi?
Bibi; nilikwambia uwe mvumilivu nitakupa jibu
Babu; Muda mrefu unanizungusha,leo nipe tu jibu la kueleweka umri unakwenda na nguvu zinapungua
Bibi:Wewe hukumbuki nilipokuwa binti nilivyokuwa nakutukana ukiniiita?shukuru Mungu sasa hivi nakubali kuongea na wewe.Vumilia tu nitakupa jibu la kueleweka mvumilivu hula mbivu
Babu; (Huku akilengwalengwa na machozi) sawa...kama nimesubiria zaidi ya miaka arobaini..nitajitahidi tu kuvumilia.

Baada ya hapo ikabidi niondoke huku nikisononeka moyoni kwa namna babu alivyoppigwa tarehe,lakini pia nikajaribu kufanya comparison na namna kizazi chetu cha sasa kinavyotongoza......................!
 
Barua ndefu kama hii ''mariam Bar''
Dauda Dieng na Ramatoulaye
 
Back
Top Bottom