Hata wa "Mbagala" twastahili kupendwa!

Busara na upole na hekima niliyorithi kutoka kwa mama yangu mama, vyote hukuvijali ukaona silingani kabisa kuwa na wewe,makuti na mkole ukakata kabisa na shina la penzi langu nanana.. eti kisa mali ukaona bora uniache mimi na uolewe,ile siku Shekhe namuona anachoma ubani unavishwa pete unakuwa mke wa fulani NILIUMIA SANAAAA..............

Lyrics inaonyesha imesimama kiukweli
 
Mbagala sio kali kama single ya SAMBUSA TAMU aliyotoa Mwanakijiji, mashairi yake yana vina safi na video yake si mchezo sio hii ya Mbagala full matakataka jalalani kama unakula sambusa waweza tapika.
 
Ila watu wa Mbagala naskia hawaipendi... wandai inawadhalilisha...

Huo ni mtizamo wao tu. Hali halisi iko hivyo na yeye kama msanii tayari kafikisha ujumbe alivyocheza kama mhusika, jamii inayoishi sehemu hizi na kwa mamlaka husika. Kila mmoja ana sehemu inayomhusu iwapo hauhusiki au hauko maeneo ya hivyo unapotezea tu Suala la nani kachukia au haupendi ni kazi kwao. Kama hayapo yeye angeyapata wapi? Wabongo wamezoea kusikia mambo mazuri tu. Binafsi nimeukubali una quality zote za kuwa wimbo bora. By the way tayari uko kwenye chart ya juu kwenye baadhi ya TV stations
 
Hii ni mojawapo ya exceptions zangu za nyimbo za Bongo Flava.. kwani huu ni mziki mzurii wenye kufuata historia ya nyimbo nyingine za zamani za Kitanzania. Una mahadhi mazuri, vyombo vimepangwa murua kabisa na sauti ya mwimbaji inaweza kumchoma moyo binti yeyote ambaye amewahi kumkatalia mtu penzi kwa sababu anatoka "mbagala ambapo mbele ya nyumba ni jalala". Ujumbe wake hata hivyo sielewi bado ni mgumu, je angekubaliwa penzi angeendelea kukaa kwenye nyumba ambayo mbele yake ni jalala au angejitahidi kwa ajili ya maisha ya baadaye kuhama? Au angekuwa ni mwanaharaka wa kuhakikisha kuwa jalala hilo haliwi karibu na maskani ya watu? Katika fasihi ya muziki hili tunawaachia wasikilizaji wenyewe kuamua.

Last edited by a moderator:
I like the song and clip also... thumps up...

Wow the groom wore just like Arabs? amazing...
 
Naifuatilia; kutokana na simulizi zenu hapa yaelekea kubeba uhalisia wa tunayokemea hapa kila siku!
 
Busara na upole na hekima niliyorithi kutoka kwa mama yangu mama, vyote hukuvijali ukaona silingani kabisa kuwa na wewe,makuti na mkole ukakata kabisa na shina la penzi langu nanana.. eti kisa mali ukaona bora uniache mimi na uolewe,ile siku Shekhe namuona anachoma ubani unavishwa pete unakuwa mke wa fulani NILIUMIA SANAAAA..............

yaah shairi zimeenda shule na zinafunsidha
 
Busara na upole na hekima niliyorithi kutoka kwa mama yangu mama, vyote hukuvijali ukaona silingani kabisa kuwa na wewe,makuti na mkole ukakata kabisa na shina la penzi langu nanana.. eti kisa mali ukaona bora uniache mimi na uolewe,ile siku Shekhe namuona anachoma ubani unavishwa pete unakuwa mke wa fulani NILIUMIA SANAAAA..............

yaah shairi za kueleweka na zinakubalika amejitahidi sana kijana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom