Hata nyie huwatokea?

Kitty Galore

JF-Expert Member
May 24, 2011
345
100
unapigiwa simu na mtu anakwambia amekuta miscall ya namba yako, au mwingine anakuuliza mbona unambeep, na kiukweli wewe hujapiga hiyo namba na wala huijui, na ukiangalia kwenye dialled namba zako haipo, sasa ukute mtu si mstaarabu anakupigia kukuuliza halafu na wewe uanze kushangaa shangaa, mbona utajibeba, hebu nisaidieni wataalam, hii husababishwa na nini?
 
Hata mimi imewahi kunitokea kama mara tatu hivi. Hata sasa kuna mtu ananitumia SMS kwa namba nisiyoijua na anaandika mabo ambayo siyajui. Kuna tuwasubiri wajuzi watufafanulie
 
mi iliwahi kunitokea katikati ya mazungumzo akatokea jamaa mwingine upande wapili anaomba msamaha sijui kwa demu wake..wakati mi nilikuwa naongea na mtu mwingine kabisa..jamaa nae kusikia sauti yangu kapagawa...sijui hata ziliingilianeje...afu ilinitokea kama mara 4 hivi kwa siku moja mpaka nikashangaa..!!
 
Back
Top Bottom