Hata Mwinyi amshangaa Kikwete, Serikali lazima ilinde ajira za wananchi wake !

Jamani KIKWETE amefumbua fumbo alililifumba miaka mitano iliyopita :MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA,KASI MPYA ,HARI MPYA Kafumbua hilo fumbo kwa kusema kuwa AKILI YA KUAMBIWA,TUMIA NA YA KWAKO!=MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA!Bado hamjaelewa tuuuu!!!!
 
Kuongea na wananchi kwa JK kulikuwa na ulazima gani wa kuwepo kwa RO, Mwamunyange na Said Mwema na (Malisa na Tosi walikuwepo) ? What was the message ukiangalia ile hotuba kwa undani ?

Msaada wenu tafadhali

Maana yake

"Ndugu wananchi, safari hii ninachosema ndicho ninachomaanisha FULLSTOP"
 
Mzee Mwinyi anahitaji kutafutiwa jukwaa la kuweza kuzungumza na taifa; kila jamii ina wazee wake.. Tatizo langu ni kuwa hakuna anayeweza kunyosha vidole kwa serikali kama alivyofanya Nyerere Mei Mosi, 1995
 
jamaa kachukia kwa kutoalikwa, mbona hotuba ile ya kwanza alijishusha sana kwa kuwasihi akina Mgaya sasa kaona wamemkosea adabu akajibu mapigo
 
mkuu umenikumbusha, kimsingi ccm inabidi waondoe hiyo alama ya nyundo ya wafanyakazi, watafute alama nyingine ya mafisadi waiweke hapo, kwani m/kiti wao kaisha sema wafanyakazi kura zenu hazimtishi na hana shida nazo! Sasa alama yao ya nini? Weka ya mafisadi ambao kimsingi ndio chama kina walinda kwa nguvu zote.

ni kweli ccm itabidi waondoe nyundo ambayo ni alama ya wafanyakazi
 
Jamani tumpongeze Rais, kwa mara ya kwanza kaamua kutotoa ahadi - au mlitaka awaahidi tena?

Nani kakwambia hakutoa ahadi? Aliposema kuwa watakaoandamana watapata kisago cha manyagu hiyo haikuwa ahadi? Power has gotten into the guys skull!!
 
mwinyi ni mzalendo wa kweli asiye na maamuzi ya jazba na kukurupuka
nchi zote duniani zinathamini mchango wa wafanyakazi isipokuwa nchi yetu tuu
 
Bendera ibadilishwe; wafanyakazi wameshakataliwa na CCM; Ibadilishwe sasa WAFANYAKAZI sio sehemu ya CCM tena; HIi ndio ajenda mhimu sana jamani 2010; bendera ibadilishwe; napiga yowe sasa benderfa ibadilishwe; au tuwarushie mchanga wenye bendera hiyo tukiwaona maana imekosewa
 
Kikwete ameshauriwa vibaya, ana washauri wa...

Kwa hiyo kuna mtu kamwambia Kikwete, Rais nenda pale ujikasirishe kasirishe, tisha watu wa TUCTA kwa majina, soma karatasi hii saa nzima kwa mapovu halafu ondoka...?


Ingekuwa kila anachofanya Rais ni cha kushauriwa basi tungeweza kuweka yeyote au wewe Chupaku au roboti tu iwe Rais halafu tukampa washauri.

Rais kachemsha mpaka Mwinyi anampiga madongo tunasema tatizo washauri.
 
mshukuru amefanya hivyo, ili watz wengi tupate nafasi ya kumwondoa madarakani katika uchaguzi ujao. ninyi wafanya kazi ndo mpate akili sasa, siku zote tulikuwa tunawaambia ccm haina maana, viongozi wa ccm hawana maana lakini nyie ndo mlikuwa wakwanza kuwapongeza, wamewang'ata panauma sasa ndo mmepata akili....akili hiyo itumieni kwenye uchaguzi ujao sasa. jamaa kawadharau vibaya mno yaani....we fikiria mtu anajua kabisa kuwa anakumbana na uchaguzi mwaka huuhuuu, lakini kafanya jeuri kwa watu ambao ndo wapiga kura wengi zaidi kuliko wote na wenye influence kubwa kuliko zote,ANAJUA HAMUWEZI KUMFANYA KITU, NA URAIS ATACHUKUA TU, kwani mtamfanya nini? wakati nyie ndo wengi wenu wavaa mashati ya kijani, fulana za njano na wagawa vitenge/kanga wakati wa uchaguzi, ndugu yenu kawageuka sasa ...wafanya kazi ndo watu wenye influence kubwa kuliko wato wote ktk uchaguzi...we angalia hata kijijini wananchi wanaacha kumsikiliza hata mwenyekiti wanawasikiliza waalimu wa shule za msingi kwasababu tu ni wasomi na wafanyakazi.....so this is your opportunity to show him that you are important kwenye uchaguzi, ili liwe fundisho na kwa viongozi wengine wote wasiojali maslahi ya wafanyakazi, fanyeni kweli kwenye uchaguzi huu. pigeni kampeni kali against him ili muwatie adabu. kama hamtafanya hivyo, sisi wengine hata hatutegemei mishahara....hiyo huwa ni hela ya soda ya watoto shuleni tu, tulishadharau na kuamua kufanya miradi mingine mikubwa. unaelewa wewe mfanyakazi unayesoma lakini?
 
Back
Top Bottom