Elections 2010 Hata Mwalimu Nyerere Aliiogopa CCM kwa uovu wake.

Ngolinda

Senior Member
Apr 12, 2010
125
25
Ingawa alikuwa mwanzilishi wa CCM, kwa nia njema ya kuendeleza mapinduzi katika nchi yetu, miaka ilivyozidi kwenda Mwalimu Nyerere alishuhudia jinsi CCM ilivyobadilika na kuwa mzigo kwake na pia tishio kwa usalama wa Taifa.

Mwaka 1993 Mwalimu alichapisha kitabu kiitwacho Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (Harare: Zimbabwe Publishing House, 1993). Pamoja na mambo mengine katika kitabu hiki, Mwalimu alisema kuwa kuna kansa katika uongozi wa CCM. Nanukuu baadhi ya maneno yake:

Chama cha Mapinduzi, kwa sababu ya uzito wa historia yake, hadhi ya jina lake, mfumo wa wavu wake, mazoea ya watu, na ubovu wa Vyama vya Upinzani, kinaweza kuchaguliwa na Watanzania, pamoja na kansa ya uongozi wake. Au watu wanaweza wakachoka, wakasema, "potelea mbali:" wakachagua Chama cho chote, ilimradi tu watokane na kansa ya uongozi wa CCM. Hainifurahishi kuyasema haya, lakini uhai wa Nchi yetu unataka yasemwe
. (Ukurasa 61)

Mwalimu hakuishia hapo, bali aliongezea namna hii:

Nilisema awali kwamba kansa ya uongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi isingekuwa ni jambo la kutisha sana kama tungekuwa tumeanza kuona Chama kizuri cha upinzani kinachoweza kuiongoza Nchi yetu badala ya CCM. Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliofanya nikapendekeza tuanzishe mfumo wa Vyama Vingi. Nilitumaini kuwa tunaweza kupata Chama kingine kizuri ambacho kingeweza kuiongoza Nchi yetu badala ya CCM; au ambacho kingekilazimisha Chama cha Mapinduzi kusafisha uongozi wake, kwa kuhofia kuwa bila kufanya hivyo kitashindwa katika uchaguzi ujao. Lakini bado sijakiona Chama makini cha upinzani; na wala dalili zo zote za kuondoa kansa ya uongozi ndani ya CCM. Bila upinzani mzuri wa nje, na bila demokrasia halisi ndani ya Chama cha Mapinduzi, Chama hiki kitazidi kudidimia chini ya uzito wa uongozi mbovu. Kwa hali yetu ya kisiasa ilivyo nchini hili si jambo la kutarajia bila hofu na wasi wasi
! (Ukurasa 66)


My Take:
1. Leo wananchi wamegundua uovu halisi wa CCM na kwamba ndio chanzo cha umasikini wao.

2. Wameamua kusema "potelea mbali" na hakika sauti yao ina mwangwi mkubwa. Sasa tunaweza
kusema kwamba ile haja ya Mwalimu Nyerere kuona chama bora cha upinzani kikiinuka
imetimia.

3. LAKINI...CCM imedhihirisha uovu wake kwa kuwanyang'anya wananchi haki yao ya kuchagua
chama na viongozi wanaowataka. Wameipora haki hiyo kwa nguvu bila haya wala huruma.

4.Their evil is obvious to all, especially God. We can be certain that the wicked have not fooled Him

5. Hakika mwisho wa CCM umefika na maovu yao yamepanda hata mbinguni, sauti za vilio na
maombi ya watu wanyonge wa Tanzania imeyatekenya Masikio yake aliye juu, naye yu karibu
kutenda hata sasa.



Source: Hapa Kwetu: Mwalimu Nyerere Aliiogopa CCM
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom