Hata Bunge letu nalo ni bunge la kata tu...kama zilivyo sekondari na baadhi ya vyuo

Mwenda_Pole

JF-Expert Member
Jul 5, 2008
281
66
Wakati nchi imejaa matatizo ya msingi kama barabara mbovu,kina mama kila siku wanapoteza maisha wakijifungua kwa huduma mbovu mahospitalini na rushwa, wanafunzi wa vyuo kukosa nyenzo, wameanzish shule za kata na sasa matokeo yanaonekana. Wanafunzi wanafeli kupindukia, hakuna vitabu, hakuna walimu. Wananchi vijijini wanaishi kwa kubahatisha tu. Hakuna umeme wa kuaminika na mambo mengi kibao tu.

Badala ya bunge letu kujadili mambo hayo pamoja na jinsi gani tunaweza kuboresha shirika la reli, kuboresha mapato kutokana na madini, kuboresha hali za maisha ya wananchi kwa ujumla...!! jamaa wanashinda kwenye mambo ya "uchama" kutumia nguvu zote kutetea mambo ya kichana hata kama hayana msingi, kutetea wanachama hata kama wanavurunda na wanatuhumiwa kwa ufisadi. Kazi ni kupigana vijembe tu kama wanapisho na kushangilia kama watu wapo vijiweni. kutokana na sababu hizo na nyingine nyingi sana sasa naweza kusema rasmi HATA BUNGE LETU NALO NI BUNGE LA KATA TU..
 
Acha maneno yakejeli na dhihaka kwetu watoto wa masikin. Kama wewe na mafisadi wenzio mmesoma ACADEMY kimpango wenu. Nani kakwambia shule za kata ni walopokaji na wafanya fujo. Toa maneno ya kufananisha na hoja yako sio shule za kata.
 
na Katibu Kata Mkuu ni Spika Makinda ha ha ha. Mwenda Pole upo sahihi kabisa
 
CCM wana laana kweli bungeni wanapendeleana na kufanya mazuri kuwa mabaya kila sehemu wameharibu ila tusikate tamaa kazi inaelekea kuisha bado kidogo tuu wajue nini tunataka
 
Back
Top Bottom