Hasira za Wazanzibar kuchoshwa na Muungano

Hahahahahaaa nani alilkwambia kuwa rais lazima atoke ccm 2015??? Kama mkoa wa Zanzibar una mtu mwenye uwezo atapata tu lakini kama hakuna ndo hivyo tena!
 
Vijana wanaolumbana ni wa CCM. Kwani raisi ajaye lazima atoke CCM?? Kwa haya yanayotokea sasa majaliwa ya chama kuelekea 2015 yako shakani.

Zanzibar?? Itabidi ipite miaka kumi mingine baada ya 2015. Nafasi waliyokuwa waipate 2005 kupitia SAS waliiuza kwa hiyana na wanajua hilo vizuri sana. Sitofahamu yote iliyofuata baada ya hapo na matatizo ambayo yameendelea hadi sasa kimsingi ni kwa sababu ya wazanzibari.
 
Tutumie busara, hekima kuliepusha taifa na machafuko, raisi ajae awe Mtanzania mwenyewe uwezo wa kuongoza, uchungu na taifa na aliye ingia madarakani kihalali.
 
Mimi sitojali anatoka upande gani au chama gani, mimi nitampigia kura kwa kigenzo cha ukristo wake basi. ni hayo tu. Hata kama ni Lowasa nitampigia kura kwa sababu ni mkiristo mwenzetu.
 
Tunataka Rais ajae atoke CHADEMA lakini wa kutoka Zanzibar ili kuleta uwiano wa Muungano na kwa kuwa vipindi viwili vilivyopita Marais wametoka Bara itakuwa si haki Rais ajae atatoka bara tena! kama Bara watalazimisha Rais kutoka bara basi heri Muungano ufe!

Hapa CHADEMA watumie busara kumpitisha mgombea wao atoke Zanzibar na hapa watacheza karata vizuri maana hata kura za Waislamu huenda wakazipata kwani watakuwa wamethibitisha kuwa hawana udini na ukabila!!!!
 
Tunataka Rais ajae atoke CHADEMA lakini wa kutoka Zanzibar ili kuleta uwiano wa Muungano na kwa kuwa vipindi viwili vilivyopita Marais wametoka Bara itakuwa si haki Rais ajae atatoka bara tena! kama Bara watalazimisha Rais kutoka bara basi heri Muungano ufe!

Hapa CHADEMA watumie busara kumpitisha mgombea wao atoke Zanzibar na hapa watacheza karata vizuri maana hata kura za Waislamu huenda wakazipata kwani watakuwa wamethibitisha kuwa hawana udini na ukabila!!!!
Rais atokane na wingi wa watu na siyo sehemu anakotoka!!! Hii kusema kipindi hiki Zanzibar halafu hiki bara, hiyo haipo kikatiba labda katiba mpya iseme hivyo. Lakini mimi siungi mkono kwa minajili tu kuwa ukiwa Mzanzibar unauhakika kuwa lazima utamtawala Mtanganyika lakini katu Mtanganyika hawezi kuwa rais wa Zanzibar. Nadhani iwe ni kidemokrasia zaidi bila kujali mtu atokako lakini tuangalie utendaji kazi na uzalendo wake kwa Taifa la Tanzania na siyo kwa Uzanzibari wake au Utanganyika wake!!!!
 
Katika katiba ya Z'bar inawawapa fursa wananchi kushiki kikamilifu katika kujenga taifa la zanzibar,moja ya kuriki kwao ni kura ya maoni inawapa fursa hiyo katika nchi ya zanzibar,kama ilivyofanyika mwaka jana waliunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Sasa basi sasa hivi kumekuja mjadala wa katiba tanzania,zanzibar kumekuwa na mijadala ya muungano,makubaliano ya muungano,sasa basi wananchi wa zanzbar wamechoshwa na mfumo huu wamuungano wa serikali mbili wakati kabla ya muungano kulikuwa kuna nchi mbili huru ziliungana na kupata serikali ya muungano ambayo kitambulika kama serikali ya jamuhuri ya muungano wa tanganyika na zanzibar.

Kilicho fanyika ni usanii wa kuifuta tanganyika na kuita tanzania,na wakaenda katika umoja wa mataifa kukifuta kiti cha zanzibar na kuwa na kiti kimoja cha muungano kwa kisingizio,hivi nchi kama haina international relation vipi itakuwa kiuchumi ?

Vipi nchi itajiwakilisha katika nchi za njee,na kupata marafiki majirani,kusaidiana katika kuleteana maendeleo,kumekuwa na hoja nyingi za msingi,kiasi ambacho natabiri yakuwa ikiwa kutaitishwa kura ya maoni zanzibar basi mungano wataukataa.

Wazanzibari wanataka serikali tatu,lakini hata hivyo wanaogopa usanii tena ambao ulioikandamiza zanzibar nusu karne sana.

Natoa salamu kwa watanganyika,ilikiwa munataka muungano basi ipo haja ya kuirudisha tanganyika haraka iwezekananvyo,ili wazanzbari waingiwe na imani na serikali ya muungano,na kihisi kuwa kama watapendekeza kuwe na serikali tatu basi itakuwa ni suala moja zuri sana kwa watanzania wote.

Wakati itakapo itishwa kura ya maoni zanzibar wakati huku tanganyika ipo na bendera inapepea inaweza kuwafanya kuwarudisha nyoyo zao kuwa sasa tunaweza kurudi kule tulikotoka mwaka 1964 katika makubaliano ya muungano wa serikali tatu.

Jee watanganyika muko tayari kuirudisha tanganyika yenu ili tulete mfumo mpya wa muungano ? Au tuvunjilie mbali ?
 
Hakuna haja ya kuvunja muungano, serikali moja tu inatosha, tutaheshimiana na kuwa na muungano wa kweli.
 
HAKUNA HAJA YA SERIKALI MOJA WALA TATU ,ZANZIBAR WALALE MBELE HATUWATAKI SISI TUBAKIE NA TANGANYIKA YETU

halafu tuone kama hawataomba kuungana na sisi tena
 
Naomba kupata ufahamu jamani. Huu muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar oko vipi? Ni union, federation au confederation? Na una faida gani?
 
Naomba kupata ufahamu jamani. Huu muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar oko vipi? Ni union, federation au confederation? Na una faida gani?
Muungano huu si aina yoyote katika ulizozitaja.
Kimsingi haijulikani ni aina gani ya Muungano. Ni vurugu tu!
Lakini linalojulikana ni kuwa Muungano huu ulikuwa designed ili after 48 years utoke kutoka kwenye muungano wa serikali mbili na uwe muungano wa serikali moja.

Faida zipo nyingi ila iliyo kuu ni kuisaidia CCM ibaki madarakani kwa kisingizio cha kuulinda Muungano.
 
ninyi mlipoungana na wazanzibar mlichezewa changa la macho, ndio maana wao wanajiita wazenji ninyi watanzania, heri yangu mimi mtanganyika. kwanza sina rais, sina muungano na nchi yoyote, timu yangu ya taifa ni kili stars, n.k:drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum::drum:
 
Hadi leo,

Nimesoma mabandiko mengi lakini sio Tanzania bara au Tanzania Visiwani wanazungumzia kuvunjika kwa muungano!

Bali wanasema haya!

--->Kuwe na federal government (serikali ya muungano) na kuwe na independent Government of Tanganyika na na Government of Zanzibar.

Kwenye hili mimi sijaona anayesema muungano uvunjike... lakini naona vyombo vya habari na watu wengi wanatumia neno kuvunjika muungano sijui wanatoa maneno haya wapi haswa?
 
Katiba mpya
Naomba kipengele hiki kiingizwe ili kuweka maadili kwa viongozi na watawala
Mgombea yeyote kwa nafasi ya uongozi akitoa ahadi ya aina yoyote ile kuwaahidi wapiga kura ama wananchi akishindwa kuitekeleza kwa kipindi chote cha uongozi wake
1/. afilisiwe mali yote aliyopata kipindi alichokaa madarakanipamoja na ndugu zake walionufaika kupitia kwake
2/. afungwe jela kifungo kisichopungua miaka kumi
3/.achapwe viboko kumi siku anaanza kutumikia kifungo na siku anapomaliza kifungo ili akamwonyeshe mke wake
 
Wakati tukielekea katika sherehe za kuadhimisha miaka 47 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, nimeona nijotekeze hapa kwenye jamvi na kuhoji ni nani kati yetu hapa anayeweza kusimama mbele yetu na kukiri kuwa muungano wetu ni muungano si wa nchi kwa nchi bali ni muungano wa ndugu wanaopaswa kuishi pamoja. Kwa nini nasema hayupo wa kusema hayo mbele ya kadamnasi na kuwa tayari hata kufa kuutetea muungano huu?? Ni kwa sababu tumeshuhudia katika miaka ya hivi karibuni mengi yakisemwa juu ya muungano huu. Tumeshuhudia wazanzibari wakisema walibakwa na sasa wanataka talaka yao baada ya miaka 47 ya ndoa wasiyoifurahia. Na tukawasikia watanganyika wakidai kwa nini tuwabembeleze acha waende. Na vitimbi vya kila aina ya hivyo lakini sikupata kusikia Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wala rais wa Zanzibar au mawaziri wao wakitoka hadharani wakisema kitu chenye kuwafanya watu waamini kuwa wana ufahamu japo kidogo kuhusu huu muungano. Tulichoambulia ni kupata msamiati mpya eti "kero za muungano". Nani kasema ndugu wanaishi bila kero ili leo kero ndio liwe jambo kubwa mnoo la kulijadili??? Nani kasema huu muungano ulilazimishwa mpaka leo ndoa ivunjwe?? Sisi hatujawa ndugu kwa sababu ya Nyerere na Karume. Siye ni ndugu tuliyeishi pamoja kabla hata neno Zanzibar wala Tanganyika hayajakuwepo kwenye ramani ya dunia hii. Hivi bado baada ya miaka yote ya wakoloni kuondoka nchini mwetu leo hii mtu ana simama na kuzungumzia mipaka iliyowekwa na wakoloni ili watutawale?? Huu ni ujuha uliopitiliza. Ndio ni ujaha maana siye hatuwezi kutengeza vya kwetu tukavienzi mpaka vya wakoloni? Kero gani zinazungumziwa miaka 15 zisizoisha???
Watanzania tuna matatizo tena makubwa. Ni kipi tunachokiweza kama hata kuuboresha undugu tuliorithi kutoka kwa babu zetu tunashindwa??
Kuna hoja eti muungano wa serikali tatu ndio suluhu ya matatizo yetu. Kwamba nchi zote duniani huwa ndivyo zinavyojiunga. Huu nao ni ujuha mwingine kwa sababu undugu wetu haufanani na undugu wa Uingereza na Ujerumani wala undugu wa Ufaransa na Italy nk. Huu ni undugu wa aina ya kipekee. Hatuwezi kutengeneza kitu cha kipekee basi mpaka tufanane na wengine??
Jamani ndugu zangu Watanzania, huu si muda wakujiuliza sisi ni ndugu ama si ndugu? Ni muda wakusema tutawajengea maisha yapi watoto na wajukuu zetu ili huu undugu wetu nao waukute na waheshimiane na kuthaminiana kama walivyokuwa babu na mababu wa babu zetu. Mimi nipo tayari kuutetea muungano huu hata kama itanigharimu maisha. Nawakilisha....
 
Mimi ni mtanzania kama walivyo watanzania wengine. Ila tofauti ya wengine mie naridhika na aina hii ya muungano wetu ambayo kwa kweli ni tunu ya kipekee sana.
 
Muungano wa nini banaaaaaaaaaa!, aaaaaaaaaaagh, wewe uteetee ugharimu maisha yako, mimi wala sitaki hata kuusikia.
Etu undugu, undugu gani wa lawama na chuki, ufilie mbali tu huu mungano
 
Back
Top Bottom