Hasira za Wazanzibar kuchoshwa na Muungano

...Lakini tujiulize hivi Zanzibar chini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haina uwezo wa kuunda majeshi?

Halafu ukishapata jibu naomba pia unijibu AMIRI JESHI MKUU WA MAJESHI YA ZANZIBAR ni nani?

We kweli ni mbumbumbu na bila shaka utakuwa mwanachama wa Chadema.


katika mambo tulioungana Ulizni na Usalama ni moja wapo hivyo Jeshi ni chombo cha Muungano pamoja na Polisi.

Usije hata siku moja ukasema kuwa Jeshi au Polisi ni mali ya Tanganyika.

Lakini hata hivyo Zanzibar ina vikosi vyake vya ulinzi wa ndani kama Valunteer , KMKM.

Suala nakuuliza je Tanganyika mna vikosi vya ulinzi?
 
kuishi kwingi kuona mengi,tunajua umetumwa na mchawi aliyekuloga ameshakufa kitambo,me sijui wewe umetokea chimbuko gani na wa enzi gani,kwanza kwa taarifa yako nimebaini njama yako ya kuleta mfarakano je utapata faida gani kuona vurugu na chuki dhidi ya waislam na wakristo inatokea,najua akili yako inaongozwa na mapepo na vyema kutafuta wazee wakuweke chini na kukufunda manakeee hujafunzwa na wazazi ati,kwa kifupi waraka pumba wako hauna mantiki katika kulijenga taifa na ni porojo tele na kama hukupata elimu ahera kajitaidi umwambie ustadhi wako arudie kipengele cha utu wa mtu na kutambua binadamu haongozwi na sheria ila hekima na utashi wa Mungu,kama huna Muda wa kuandika vitu vya msingi bora ukaimbe taarabu tujue moja manake labda ndiyo unaloliweza,mimi nimekusamehe kwani hujui utendalo na elimu yako ya a,e,i,o,u haijakusaidia kitu:wink2:
 
Uraya????????????????????????????
May be I am dumb but I will ask all the same. What is the connection between London, Paris, Toronto, Niagra Falls and the Tanzania Union. As a zanzibari you are supposed to know the answer to the question whether Tanzania is Uraya (or is is Ulaya)?
 
Jamani chungeni lugha tumia kiswahili sanifu acheni ushamba wa kuchanganya L na R inaonyesha jinsi watu hamjasoma URAYA ni ULAYA
 
strategy za wakristo Zanzibar
.ExternalClass .EC_hmmessage p { padding: 0px; }.ExternalClass body.EC_hmmessage { font-size: 10pt; font-family: Verdana; }
Waraka maalum kwa Wakristo Zanzibar

Wapendwa katika Bwana,


NDUGU Wakristo umefika wakati tumeonelea kuwa ipo haja ya kuwaelezeni
machache ili kuona maendeleo yetu na mafanikio tuliokwisha yapata hapa
Zanzibar, yanaendelezwa na hayarudi nyuma kwa namna yoyote. Hapana
shaka kuwa munaelewa kuwa idadi yetu hadi sasa ni ndogo sana na wengi
wetu tungali katika kiwango na hadhi ya wahamiaji na sio Wazanzibar
kama wanavyosema wenyewe.



MAFANIKIO YETU


KABLA kugusia yale ambayo tunahisi ndio lengo la waraka huu hapana
budi kuwatajieni mambo machache ambayo tumefanikiwa kuyapata hadi
sasa. Pamoja na jitihada zetu za muda mrefu bado tunapaswa tumsifu
Bwana kwa msaada wake mkubwa kwetu dhidi ya maadui zetu. Tunaamini
kuwa kupitia nguvu ya Roho Mtakatifu, Bwana atatupa ushindi na
mafanikio makuu zaidi ya haya na atawafumba macho maadui zetu wazidi
kulala ili mipango yetu yote ya kuibadilisha Zanzibar kidemografia
ifanikiwe katika kipindi kifupi kijacho. Mafanikio yetu yameenea
katika kila upande - katika uchumi, siasa, huduma za jamii, umiliki wa
ardhi, ujenzi, elimu na kadhalika ili kupata picha kamili ni vyema
tuorodheshe kwa ufupi mafanikio hayo:


Nafasi yetu kwa upande wa elimu imekuwa ya kuridhisha kupitia nafasi
za serikali. Hivi sasa ni rahisi na limekua jambo la kawaida katika
kila matangazo ya wito wa masomo kusikia majina ya Wakristo. Kati ya
vijana 7 hadi 10 ni lazima upate vijana wawili hadi watatu kutoka
katika makanisa yetu.


Sambamba na matangazo ya elimu, vijana wetu wamekuwa wanapata nafasi
nyingi za ajira katika serikali ya Zanzibar.


Hali ya kutoelewana kisiasa baina ya Wazanzibari imetoa mwanya kwetu kuingiza vijana wa
Kikristo wenye asili ya bara kwa wingi kwani wamekuwa wanaaminika
zaidi kuliko vijana wa Zanzibar.


Hali tulioieleza juu imetuwezesha kuwa na Wakristo wengi katika nafasi
za juu serikalini na katika chama tawala. Hali hii ni lazima
iendelezwe katika ngazi zote kwani ndiko kunako mambo mengi ya kila
siku.


Tumepata fursa ya kutumia Taasisi za serikali kwa uendeshaji wa ibada
zetu. Hali hii imefanya tuzidi kukubaliwa na Waislamu na kuvumiliwa na
inaweza kutupa nafsi ya kuwavuta katika NENO LA BWANA.


Kwa upande wa mashamba (vijijini) tumepata wasaa mzuri wa kununua
ardhi toka kwa Waislamu ambao hadi sasa bado hawajashtuka. Ardhi hizi
zimetuwezesha kujenga makanisa kadhaa ambayo hapo awali hayakuwepo.

Idadi ya skuli na vituo vyetu (ambavyo licha ya picha ya juu kuwa
haviendeshwi kwa misingi ya Kikristo lakini kiukweli ni vituo vya
kimisionari) vimeongezeka kwa hali ya kuridhisha. Skuli hizi ni
kuanzia kwa watoto wadogo hadi vituo kama hichi kilichopo mji mkongwe
(Stone Town Youth Centre) na zinafanya kazi vizuri katika kupandikiza
mila za Kikristo.


Sera zilizopo hivi sasa kwa upande wa uingiaji na utokaji Zanzibar
imetusaidia sana katika uingizaji wetu (Wakristo) kutoka Bara na hivyo
kusaidia kufuta ile imani ya kuwa Zanzibar ni kisiwa cha Waislamu eti
Wazanzibari kwa zaidi ya asilimia 99 ni Waislamu.


Ujaji wa Wakristo kwa wingi kutoka Bara umewezesha kuongezeka kwa
idadi ya mabaa na kilabu za pombe. Hivi sasa ni jambo la kawaida kuona
magari ya aina mbalimbali yanayomilikiwa na eti Waislamu yamebeba
kreti za bia na pombe kali.


Kujiingiza kwetu katika taasisi za dola katika ngazi za mitaa
kumetuwezesha kupata nafasi ya kutangaza Ukristo kwa njia ya mihadhara
na wakati huo huo kudhibiti mihadhara ya wazi ya Waislamu kwa kutumia
madai ya kashfa na kutatanisha maelewano mazuri baina ya watu wa dini
tofauti.

Tumefanikiwa kupata viwanja vingi katika maeneo ya mjini ambayo
yangali mapya. Maeneo haya ni kama Tomondo, Mombasa, Mwanakwerekwe na

kadhalika ambayo tayari tumeshajenga makanisa yetu ingawaje kwa sasa
hayajawa na waumini wengi wa kuyatumia na bado yanaonekana ni matupu.

Ndugu wapendwa katika Bwana,

Mafanikio hayo yasitufanye tukalewa na kusahau jukumu la kanisa la
kuona kuwa utawala wa Bwana unashuka Zanzibar haraka iwezekanavyo.
Kosa lolote utakalofanya hivi sasa litaweza kuturudisha hatua kadhaa
na huenda nafasi hii tuliyonayo hivi sasa tusiipate kwa karne mpya
ijayo.


Mambo ya kufanya yanayotukabili ili kuimarisha nafasi yetu ni kuona
yale tuliyokwisha yapata hayatutoki na kuyafanya dira kwa karne ijayo
ni haya yafuatayo:


Tusahau tofauti zetu dhidi ya adui

Ingawaje tupo madhehebu nyingi lakini tunawajibika kuelewa kuwa
Waislamu na Uislamu wao ni adui yetu namba moja ambaye hatutofaulu
kupambana nae mmoja mmoja. Uislamu hapa Zanzibar ni dini iliofungamana
na mila na utamaduni hivyo kila itakavyowezekana tusahau tofauti zetu
ndogo ndogo na hata kubwa kukabiliana nao, vingienvyo tutarudi kama
wakati wa Karume.


Tuhakikishe tunapata ardhi

Hii ni mbinu kongwe katika usambazaji wa Ukristo. Wazee wetu
walipoleta Ukristo Zanzibar na katika Afrika, jitihada waliyofanya ni
kupata ardhi kuwa kwa ajili ya ujenzi wa maeneo yetu, majengo ya
hospitali, shule, zahanati na vituo vya chekechea, makanisa na
kadhalika. Tunahitaji ardhi kubwa ili kuziweka huduma hizo mahala
pamoja kwa ajili ya kueneza injili ya Bwana na Muokozi wetu.


Tununue nyumba na viwanja kwa ujenzi wa Makanisa

Inaonekana Waislamu wenye siasa kali na baadhi ya watendaji kwenye
serikali wameanza kushtuka na ongezeko kubwa la makanisa katika kisiwa
cha Unguja. Kuna dalili kuwa tunaweza kupata ugumu katika kupata
viwanja kwa ajili ya makanisa. Njia tunayoweza kuitumia kwa muda huu
ni kununuwa viwanja vitupu au nyumba za Waislamu kwa bei kubwa
itakayowashawishi kuziuza na baadaye tukaweza kuvijenga au kugeuza
nyumba hizo kuwa makanisa.


Tujenge shule na hospitali kwa wingi

Hizi ni taasisi ambazo tunaweza kueneza neno la Bwana kwa Waislamu
walio wengi hapa Zanzibar. Kwa kutumia umaskini unaowakabili wengi ya
Wazanzibari na uchache wa huduma hizo tunaweza kujitangaza vizuri,
tujitahidi kutoa huduma nzuri kuweka vifaa vya kisasa kuweka bei
ndogo, kuweka upendo ili vituo vya Waislamu au hata vile vya serikali
visiweze kuvikaribia vyetu. Shule ni sehemu muhimu ya kupandikiza
mafundisho yetu zaidi kwa watoto wadogo (Nursery).


Tunadai muda zaidi katika vyombo vya habari (TV na Radio)

Kwa muda mrefu sasa Uislamu na Waislamu wamehodhi vyombo hivi vya
habari mbali na kuwa siku ya Ijumaa ambayo yote humilikiwa na vipindi
vya Kiislamu vyombo hivyo hutenga siku nyingine kadhaa kwa vipindi vya
Kiislamu na hata kuthubutu kutia adhana kila wakati wa sala hali hii
inaudhi na inatoa picha ya wazi ya serikali kupendelea Uislamu
ingawaje inadai kuwa haina dini. Wakati wa kusherehekea miaka 25 ya
TVZ tulizungumzia suala hili lakini halikupata mtu wa kulifanyia kazi.
Sasa tuhakikishe kuwa Ukristo unapata muda zaidi katika vyombo hivyo
au Uislamu nao upunguziwe nafasi.


Tuongeze mhadhara wa wazi

Wakati Waislamu wamezuiliwa kufanya mihadhara ya wazi, sisi tujitahidi
kuhakikisha kuwa mihadhara yetu inaongezeka kwa kiwango kikubwa. Kwa
kuwa Waislamu hawahudhurii mihadhara hiyo, lazima tuone Wakristo wa
mjini na mashamba wanahamasishwa na kupatiwa nyenzo ili kuhudhuria.
Vipaza sauti vitumike kuhakikisha kuwa neno la Bwana linafika kila
pahala. Mihadhara ifanyike karibu na nyumba, Misikiti na kwenye
viwanja vya wazi.


Tuendelee kutumia shule na sehemu za umma

Ili kuwafanya Waislamu watuzoee na kuondosha chuki yao kwetu ni lazima
kuendelea kutumia mashule na sehemu za umma zilizo wazi kwa mambo yetu
ya ibada kwa kipindi kirefu hali hii inaweza kuwafanya washindwe kuona
tofauti yetu na wao.


Tufanye suala la uhamiaji Zanzibar kuwa jepesi

Uzoefu unaonesha kuwa ni jambo gumu kuwabatiza Wazanzibari Waislamu.
Hali hii inafanya ongezeko la Wakristo kuwa dogo au halipo kabisa
ukitoa wale wanaozaliwa katika familia za Kikristo.


Njia pekee ya kuhakikisha ongezeko la makanisa na taasisi zetu ni
kuongezeka kwa Wakristo. Jambo hili litawezekana kwa kuingiza Wakristo
wengi kutoka Tanzania Bara au wapagani ambao tutaweza kuwabatiza kwa
kutumia udugu wetu wa kikabila au asili ya Bara. Kwa kuwatumia ndugu
zetu waliomo serikalini (SMZ au SMT) tuhakikishe kuwa suala la
uhamiaji linabakia wazi na rahisi na linaendelea kwa kila hali.


Tuzuie jaribio lolote la kadi za uraia au vitambulisho

Wakrsito tunapaswa kuelewa kuwa iwapo serikali ya Zanzibar itaamua
kufanya chochote ili, kuwa na vitambulisho au kadi za uraia kwa
Wazanzibari basi jambo hilo litaathiri sana mipango yetu ya muda mrefu
kwa Zanzibar. Jitihada zozote za kuiimarisha Zanzibar kama Zanzibar na
nje ya Utanzania ni lazima tuelewe kuwa Uislamu utapata nguvu na kuwa
tishio kwa hapa Zanzibar na hata Bara. Iwapo tutawajibika kuunga mkono
ni kadi za Uraia na vitambulisho vya Watanzania kwa ujumla na sio
Zanzibar peke yake.


Tujipenyeze na kushika nafasi muhimu

Lazima tuelewe kuwa chama chochote cha siasa kinalenga kukamata
serikali ili kiweze kutekeleza yale yanayoaminika kuwa mazuri kwa
chama hicho. Tunapozungumzia vyama vya siasa kwa Zanzibar tunahusisha
zaidi kwenye CCM na CUF. Watu wetu wamefaulu kuingia kwa wingi katika
chama tawala na katika jumuiya zake.


Tuunge mkono sera za utalii

Hadi sasa wengi wa watalii wanaoingia Zanaibar hutokea nchi za
Kikristo. Desturi za watalii hupingana na zile za Kizanzibari na hata
za Kiislamu. Watalii wanasaidia kuongezeka kwa mabaa na vivazi ambavyo
Waislamu wanataka visivaliwe hasa na wanawake.

Tujenge mabaa na kuongeza pombe

Waislamu wengi huchukia pombe na huweza kuhama iwapo duka la pombe au
baa ipo karibu nao. Waislamu hatari ni wale wanaosoma na kupata muda
wa kujishughulisha na dini yao.

Pombe ni kitu ambacho humtoa Muislamu katika Uislamu wa vitendo na
kumkaribisha na Ukristo.


Uwafuate Wakristo waliosilimu ili warudie Ukristo

Watu wa aina hii wanakuwa bado hawajatulia na mara nyingi huwemo
katika matatizo. Pana haja ya kuwalenga watu hawa ili kuwarudisha
kabla hawajatulia au kupata elimu nzuri. Matatizo yao ndipo mahala pa
kuanzia ili Bwana atawateremshie roho ya utulivu. Uzima wa Ukristo ni
kuwa na wafuasi wengi kadiri iwezekanavyo.


Tuwafuate wanawake kwa misaada

Jumuiya zisizo za kiserikali zinaungwa mkono duniani kote na hasa zile
za wanawake na watoto tujiweke pamoja ili tuweze kuwavutia kwa jina la
kuwasaidia.


Tuongeze vituo vya mafunzo ya Kikristo

Kituo cha vijana cha mji mkongwe (Stone Town Youth Center) kimekuwa
kikifanya kazi yake vizuri kwani hadi sasa lengo lake la ndani bali
halijaeleweka na vijana wanaohudhuria hapo kwa shughuli mbalimbali,
jitihada zifanyike ili kuwa na vituo vya aina hii katika maeneo
mengine. Lengo kuu liwe ni vijana na wanawake bila ya kuonesha dalili
za kidini.


Tuwaoe wanawake wao kwa kusilimu kimajina

Jitihada za makusudi zifanyike ili kila itakapowezekana kuwaoa
wanawake wa Kiislamu ili tuweze kuwabatiza baadae, njia nzuri iwapo
patakuwa na ugumu ni kusilimu kiuongo ili kuruhusiwa kuwaoa wanawake
wao.

Tuanzishe NGOs na sisi tuwe viongozi

Kwa kuwa hivi sasa wafadhili wengi wameonesha hamu ya kuzisaidia NGOs
moja kwa moja badala ya serikali ni lazima tujitahidi kuunda jumuiya
zetu ambazo zitawashirikisha Waislamu lakini uongozi wa juu ni lazima
uwe mikononi mwetu. Hii itatuwezesha kuona sera zetu na malengo
yanatelekezwa kwa kivuli hicho.


Tujenge ukaribu na viongozi ili kuwadhibiti Waislamu

Mambo yetu mengi yamekuwa yanakwenda vizuri katika maeneo mbalimbali
baada ya wenzetu kuwemo katika kamati za masheha, na matawi ya vyama,
na kamati za maendeleo za maeneo mbalimbali. Hali hii ni lazima
iongezeke ili udhibiti wa shughuli za Waislamu uwe mzuri zaidi na
wakati huo huo kuona kuwa mambo yetu yanakwenda yakiwa na baraka ya
vyombo vya dola na vyama vya siasa.


Tuwachonganishe Mashehe wenye msimamo mkali

Mashehe wenye misimamo mikali wamekuwa ni tatizo kwa Ukristo kwani
wana wafuasi wengi na wamekuwa wakisema wazi na kushutumu maendeleo
yetu. Mashehe hao ni lazima wachonganishwe na serikali ili hali
ikiruhusu wazuiliwe kuendesha shughuli zao. Wakati tukifanya hivyo
hatuna budi kuwaunga mkono Mashehe wote ambao wamekuwa wakitusaidia
kwa njia mbalimbali.


Tulenge kuifuta Tabligh

Pamoja na kuwa na Tabligh sio hatari moja kwa moja kwa Ukristo lakini
bado inastahili kupigwa vita kwa sababu ina aina pekee ya mihadhara ya
Waislamu inayoruhusiwa humu Zanzibar. Tabligh inaweza kuwazindua
baadhi ya Waislamu ambao ni vema kubaki bila ya kuzinduliwa.

Tudai turudishiwe taasisi zetu


Serikali ya Zanzibar bado inaonekana kuwa ngumu katika milki ya
makanisa, ardhi na taasisi zetu. Dalili za huko nyuma zilionekana
nzuri kwani tulifanikiwa kupata hospitali yetu Walezo na eneo la
Kiugani hata hivyo panakuwepo na ugumu wa kurudishwa shule zetu. Kwa
kuwatumia wenzetu waliomo serikalini na baraza la wawakilishi
tuzidishe harakati na madai ya taasisi zote zilizobaki.


Tulete waumini kutoka mashamba kuanza makanisa

Hivyo sasa pameibuka wasi wasi kuhusiana na wingi wa makanisa ambayo
hayajapata waumini wa kuyajaza. Ili kuficha dosari hii na hoja kadhaa
utaratibu uliopo hivi sasa chini ya baadhi ya makanisa ni lazima
uungwe mkono. Wakristo wahamiaji wengi hufikia mashamba hivyo pawekwe
na utaratibu wa kuwaleta mjini ili kujaza makanisa.

Neno la mwisho

Wapendwa katika Bwana.


Miongozi hii ni mikubwa na inaweza kuwatisha baadhi ya waumini wa
Kikristo hasa wale ambao bado hawajampokea Roho Mtakatifu vizuri. Hata
hivyo, kwa uwezo wa Bwana Mungu wetu ni mpango rahisi. Suala la muhimu
ni haya kufahamika na kila Mkristo apendae kumtumikia Bwana. Pia
hatuna budi kuishukuru awamu ya nne ya serikali ya Mapinduzi ambao
imefungua milango kwa Ukristo na kushuhudia ongezeko la makanisa.



Bwana awe nasi!
Bw. Abdulahsaf wewe ni mjinga!, mjinga!, mjinga! and God knows wewe ni tatizo sana katika nchi changa kama hii ya kwetu. Hata nyumbani kwenu wewe ni mzigo! Kama sijakosea umesoma lakini maendeleo yako yapo kama mbumbumbu wa kijiweni kwa sababu ya roho mbaya na fitna. Unajua sababu? Hujiamini na unasumbuliwa na inferiority complex ambayo ni chronic.
Yaani upo tayari kutunga uongo(ambao hata dini yako inakataza) kwa maandishi mengi ili kuchonganisha watu wa imani tofauti kwa kuwa tu huduma zinazotolewa na watu wa dini unayoichukia zinakunyima raha
Roho mbaya, dhana na uzushi hata dini unayoiamini inakataza. Hakuna dini yoyote ya mwenyezi Mungu inayokubaliana na unachojaribu kukifanya hapa.
Yaani wewe hata ukimkuta mtu wa dini yako anasifia huduma ya shule, hospitali nk vinavyomilikiwa na wakristo hupati usingizi kwa kuwa roho inakuuma sana!
Kwa taarifa yako ukristo unaouponda haulazimishi wala kutumia hadaa ya shule na hospitali kubadili dini za nchi. Wapo fanatics wachache wa aina yako ambao ningeshauri mkutane mjadiliane maana na wao wanapenda majungu na uzushi kama wewe kwa kuwa wanadhani wataenda peponi kwa kufitini dini za wenzao.
Ushauri wangu: Maadamu hizo hospitali, shule nk hazikulazimishi kuwa mkristo wewe fuata dini yako kwa uadilifu na utaingia peponi kwa rehema za Mwenyezi Mungu.
Fitna unayojaribu kupandikiza haiisaidi nchi yako, haiisaidii dini yako, haikusaidii wewe na wala haikupeleki popote kama hutaacha roho yako mbaya na kufuata uadilifu aliokuamuru Mola wako kupitia dini unayoiamini. I tell you the truth, dini unayoiamini ndiyo ya kweli kwako na kazi yako ni moja tu kufuata mafundisho yake kwa haki na si unafiki na fitna kama hii uliyoipost hapa JF.
Pole sana kwa maradhi ya roho mbaya!
 
Chadema inaangalia mwanya huo ili kujipenyeza.

Poleni sana CHADEMA
Inakuwaje watu mnakuwa wajinga kiasi hiki wakati mnajua kuandika? Kwa hiyo wewe na akili yako umeona connection yoyote kati ya CDM na fitna aliyoandika mwenzako?
Mungu wangu!
 
Jamani chungeni lugha tumia kiswahili sanifu acheni ushamba wa kuchanganya L na R inaonyesha jinsi watu hamjasoma URAYA ni ULAYA

Asili ya kiswahili ni Tanganyika ,sisi Wazanzibar husema RASHID nyiyi =LASHIDI,ZAHOR nyiyi ZOHOlO with is with?. ULAYA nyiyi ULAYA.
 
Sema halua atasema arua,sema wazanzibari atasema wazanzibali,duh nomaa sema hallow aroooo
 
Written by administrator // 19/03/2011 // Habari-Picha, Kitaifa // 20 Comments

Jussa-564x272.jpg

Na Salma Said,
KONGAMANO la kudajadili katiba mpya ya Tanzania linaloendelea kufanyika Zanzibar limechukua sura mpya baada ya wanasheria na wananchi kuishauri Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuunda tume yake ya kukusanya maoni badala ya kutumia tume ya pamoja ya Muungano.
Wito huo umetolewa jana washiriki mbali mbali wakati wakijadili mada kuhusu katiba za Tanzania na Zanzibar, changamoyo juu ya mianya na utata uliopo iliyowasilishwa na Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Ibrahim Mzee Ibrahim katika ukumbi wa Eacrotanal Mjini Unguja.
Mwanasheria maarufu Zanzibar, Awadh Ali Said amesema Zanzibar haitonufaika na mjadala wa marekebisho wa katiba ya Muungano kama tume itafanya kazi hiyo ya kukusanya maoni Tanzania bara na Zanzibar kutokana na wananchi wake ni wachache kulinganishwa na Tanzania bara.
Kwa msingi huo alisema ili haki itendeke na kupata maoni ya mustakabali wa muungano juu ya muundo na aina ya Muungano ni vyema kukawa na tume mbili zitakazofanya kazi hizo moja upande wa Tanzania bara na nyengine Zanzibar.
“Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iunde tume yetu ya kukusanya maoni kwa sababu tupo wachache na tukiwa katika mkumbo wa pamoja hatutanufaika kulinga na mazingira ya Zanzibar” alisema Mwanasheria huyo huku akipigiwa makofi na washiriki wa kongamano kuonesha kuwa wanamuunga mkono.
Alisema Zanzibar ina mambo mengi ya kujadili kuhusu maslahi ya Zanzibar ikiwemo suala la jumuiya ya afrika mashariki kutokana na kuwa kuna mambo ambayo hayamo katika orodha ya mambo ya muungano kama afya, utalii na kilimo na ndio maana ipo haja kwa Zanzibar kuwa na ushiriki katika jumuiya hiyo ili iweze kutetea ipasavyo maslahi yake.
Naye Ahmed Omar Khamis alisema rais wa kwanza Zanzibar, Mzee Amani Karume hakuwa na mchango mzuri katika kuandaa makubaliano ya muungano na ndio maana kero nyingi zinajitokeza baada ya kutozingatiwa maslahi ya kisaisa na kiuchumi.
Hata hivyo alisema kwamba ili marekebisho ya katiba yalete faida na kuondoa kero zilizopo hivi sasa lazima kuwe na tume zitakazoweza kufanya kazi tofauti ikiwemo tume ya maoni ya Zanzibar na tume ya maoni ya Tanzania bara.
Alisema tume zilizopita ikiwemo ya Jaji Kisanga na Jaji Nyalali zilifanya kazi za kukusanya maoni kuhusu muungano lakini hadi sasa hakuna utekelezaji wowote uliofanyika kutokana mambo hayo yalitawaliwa na ujanja ujanja na kutahadharisha lazima umakini uwepo katika suala hilo.
“Tunaweza tukaletewa tume hapa kama zile za kina Jaji Kisanga na Jaji Nyalali zikatembea Tanzania nzima kukusanya maoni na matokeo ya tume hizo tukaja kuuambiwa asilimia 80 wamesema hivi na asilimia ishirini ndio wamesema hivi kwa hivyo bila ya shaka kwa kuwa sisi kidogo tutaonekana ni wachache kwa hivyo jambo la msingi hapa kuundwe tume itakayokusanya maoni kule Tanzania bara na sisi tuwe na tume yetu ambayo ikusanye kwa mujibu wa idadi yetu” alisema kijana huyo.
Akichangia katika mjadala huo Omar Mussa Makame alisema katiba ya muungano inahitaji kuangaliwa kwa umakini kwa vile sio mwafaka rais wa Zanzibar kula kiapo cha kutii na kulinda katiba ya muungano wakati amechaguliwa kwa katiba ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar mbali na kuapishwa kulinda katiba ya Zanzibar na ya Jamhuri ya Muungano hulazimika kula kiapo mara mbili cha kulinda na kutetea katiba ya muungano akiwa kama waziri asiyekuwa na wizara maalumu katiba baraza la mawaziri la Muungano.
Akiwasilisha mada yake Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Ibrahim Mzee Ibrahim alisema vifungu vingi vya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vina kasoro na kutoa mfano Rais wa Jamhuri ya Muungano anateuwa mawaziri kwa kushauriana kwa kushirikiana na waziri mkuu bila ya kushauriana na makamu wa kwanza wa rais au rais wa Zanzibar ambayo ni sehemu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Aidha alisema kwamba katiba hiyo ya Jamhuri ya Muungano imempa uwezo rais wa Jamhuri ya Muungano kuteuwa mawaziri kutoka Zanzibar na kuwapa madaraka katika wizara ambazo hazihusiani na masuala ya Muungano jambo ambalo linahitaji kujadiliwa katika marekebisho hayo ya katiba mpya.
Mzee alisema utata wa katiba katika jamhuri ya Muungano pia upo katika ibara ya 64 wakati bunge la jamhuri limepewa uwezo wa kutunga sheria zitakazotumika hadi Zanzibar wakati katiba ya Zanzibar ibara ya 132 imeweka wazi hakuna sheria itakayotungwa ambayo haihusiani na masuala ya muungano kutumika Zanzibar hadi itakaporidhiwa na baraza la wawakilishi.
Katibu huyo wa baraza pia alitoa mfano wa wizara ya mambo ya ndani na wizara ya ulinzi kuwa yapo mambo ndani ya wizara hizi hayamo katika orodha ya mambo ya muungano kama vile kikosi cha zima moto, magereza, na jeshi la kujengwa taifa JKT lakini wizara hizo zimekuwa zikiongozwa na wazanzibari na kusimamia mambo ambayo hayamo katika orodha ya mambo ya muungano.
Alisema hizo ni kasoro za kikatiba ambazo zinahitaji kuangaliwa pamoja na kesi za uchaguzi zinazohusu wabunge ambapo masharti ya katiba yameweka kesi hizo zisikiliziwa na mahakama kuu ya Tanzania wakati suala la mahakama halipo katika orodha ya mambo ya muungano na kila upande ina mahakama kuu yake.
Mjadala huo wa katiba mpya unayatarishwa na jumuiya zisizokuwa na kiserikali na suala la urais wa Zanzibar kuwa makamu wa rais wa muungano limekuwa likichukua nafasi kubwa katika mjadala huo kwa wajumbe baada ya wananchi wengi kupinga marekebisho ya 11 ya katiba yaliofuta wadhifa huo.
Jumuiya zisizokuwa za kiserikali zilizoandaa kongamano hilo ni jumuiya ya waandishi wa habari za Maendeleo Zanzibar (WAHAMAZA), jumuiya wa wanasheria Zanzibar(ZLS), Kituo Cha Huduma za Cheria Zanzibar (ZLSC) na Taasisi ya Utafiti wa Historia Ukanda wa Bahari ya Hindi Zanzibar (ZIORI)
Sikiliza wachangiaji wa kongomano hilo:








#gallery-1 { MARGIN: auto}#gallery-1 .gallery-item { TEXT-ALIGN: center; MARGIN-TOP: 10px; WIDTH: 33%; FLOAT: left}#gallery-1 IMG { BORDER-BOTTOM: #cfcfcf 2px solid; BORDER-LEFT: #cfcfcf 2px solid; BORDER-TOP: #cfcfcf 2px solid; BORDER-RIGHT: #cfcfcf 2px solid}#gallery-1 .gallery-caption { MARGIN-LEFT: 0px}





Picha zote kwa hisani ya Salma Said,
 
Mimi bado sijapata jibu ni kitu gani hasa Zanzibar wanahitaji na hawana sasa kwasababu ya muungano. Kama Zanzibar inahitaji haki zote za kutambuliwa kama Tanzania basi ni bora waombe Muungano uvunjwe kwasababu huwezi kuwa na Usawa ndani ya Muungano. Hata hapa USA kuna haki za State lakini huwezi kuita state nchi!!. Kama kuna mambo mengine wayaseme hewani watu tujue vizuri badala ya kulalamika.
 
Mimi bado sijapata jibu ni kitu gani hasa Zanzibar wanahitaji na hawana sasa kwasababu ya muungano. Kama Zanzibar inahitaji haki zote za kutambuliwa kama Tanzania basi ni bora waombe Muungano uvunjwe kwasababu huwezi kuwa na Usawa ndani ya Muungano. Hata hapa USA kuna haki za State lakini huwezi kuita state nchi!!. Kama kuna mambo mengine wayaseme hewani watu tujue vizuri badala ya kulalamika.

Mimi nahisi jibu lako Mh Kamundu ni Kurudishwa kwa Tanganyika ambayo ndio mshirika wa Muungano wa Zanzibar kuwa na Serekali 3 ili kuondowa utata wa mambo yasio ya Muungano, au kuvunjwa Muungano ambao wazanzibar wanaona ni mzigo walio bebeshwa kwa jina la Tanzania ukitaka zaidi sikiliza hapo.

Wanasheria washauri Zanzibar kuunda tume ya mabadiliko ya katiba | MZALENDO.NET
 
Mimi nahisi jibu lako Mh Kamundu ni Kurudishwa kwa Tanganyika ambayo ndio mshirika wa Muungano wa Zanzibar kuwa na Serekali 3 ili kuondowa utata wa mambo yasio ya Muungano, au kuvunjwa Muungano ambao wazanzibar wanaona ni mzigo walio bebeshwa kwa jina la Tanzania ukitaka zaidi sikiliza hapo.

Wanasheria washauri Zanzibar kuunda tume ya mabadiliko ya katiba | MZALENDO.NET
Abdulahsaf,
Naomba nikuunge mkono kwa kusema wakati mwingine dawa ni kuvunja muungano japo kwa miaka 50 kila upande ujue lake kwanza na kuwaachia historia vizazi vijavyo kwamba kama wanataka Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar basi watumie miaka kama 100 kujadili kabla hawajakubaliana kuungana kwa miaka kumi (10) ya majaribio na kama malalamiko ya mambo madogomadogo yataendelea basi wavunje muungano huo jumla na ikubalike ktk katiba zao kwamba haiwezekani watu hawa kuungana.
CCM hawana sera ya serikali tatu, CUF wanayo lakini wapo tayari kukaa kimya kwa ajili ya kutetea nafasi za Makamu wa Kwanza wa Rais na Mawaziri katika SMZ. Sasa mjadala utapitia wapi?.
Binafsi naona malalmiko mengine yanakuwa ya kipuuzi sana kiasi kwamba kama ndo mtazamo kamili kutoka Zanzibar pengine ni bora kusiwe na Muungano kabisa maana wakati mwingine hata sijui ulazima wake ni nini endapo kila wakati watu wanalalamika tu na wanacholalamikia ni mambo kama vyeo, zamu za madaraka, uanachama ktk jumuiya za kimataifa nk ambayo naona kama Tanganyika wangeweza kulalamika zaidi lakini wapo tuli hawana tatizo.
 
Mimi bado sijapata jibu ni kitu gani hasa Zanzibar wanahitaji na hawana sasa kwasababu ya muungano. Kama Zanzibar inahitaji haki zote za kutambuliwa kama Tanzania basi ni bora waombe Muungano uvunjwe kwasababu huwezi kuwa na Usawa ndani ya Muungano. Hata hapa USA kuna haki za State lakini huwezi kuita state nchi!!. Kama kuna mambo mengine wayaseme hewani watu tujue vizuri badala ya kulalamika.
Na naamini huwezi kupata jibu iwapo unafananisha Muungano wa USA na huu wa Tanganyika na Zanzibar. Kwani kule USA kuna marais wangapi vile?
 
Back
Top Bottom