Hasheem Thabeet atinga Blazers!

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,775
3,610
hasheem.jpg


Mchezaji wa kulipwa wa mpira wa kikapu wa Tanzania, Hasheem Thabeet amechukuliwa na klabu ya Portland Trail Blazers inayoshiriki kwenye Ligi ya Mpira wa Kikapu nchini Marekani (NBA) kutoka klabu ya Houston Rockets.


Kwa mujibu wa taarifa za kwenye mitandao mbalimbali, Portland Trail Blazers imefanikiwa kumnyakua Mtanzania huyo kutoka Rockets kwa kubadilishana na mchezaji mwingine Marcus Camby, jana ambayo ilikuwa siku ya mwisho iliyowekwa na NBA kwa ajili ya klabu zinazocheza ligi hiyo kufanya utaratibu huo wa kubadilishana wachezaji.
 
Back
Top Bottom