HASHEEM Thabeet ampiga mtama TID!

Iko kazi masupa staa wetu ..najaribu kutafakari chanzo cha ugomvi wao hahah!
na wewe ni paparazzi mzuri sana kasoro tu ungemtafuta Shigongo angekupa chanzo cha ugomvi
 
Hasheem namwona hapa IFM shule na VOGUE lake anafungulia muziki mkubwa milango yote wazi na wapambe wake kisa anatafuta attention kwa wasichana.....????????? kama mtu anabisha leo mida ya saa 11 na nusu pitia pale IFM chuo utajionea mwenyewe.

Duh jamaa anashindwa kuimbisha?
 
Ilikua majira ya saa kumi unusu nikiwa natoka club billcanas pamoja na rafiki yangu ANNA tukiongozana kuelekea mlango mkubwa wa kioo nikiwa naongea na simu na Hisbert kwa sauti ya juu maana kelele za muziki zilikua zinasumbua nikiwa nimesimama nje ya mlango wa kioo ghafla akatokea bwana HASHIM ambaye alikua counter akiongea na wakata ticket akaja nje na kunipiga bonge la mtama nikaaunga chini ya sakafu na kuzirai kwa dakika kadhaa,mabaunsa wakanibeba na kuniweka pembeni maana nilikua mlangoni,nilipozinduka nilisikia maumivu makali kwenye mabega,mkono wangu wa kulia na mguu ambao unafanya kutembea kwangu kwa taabu,nikaangalia mkononi simu yangu sikuiona tena,nikawauliza mabaunsa wake jamaa amekwenda wapi!wakadai ameondoka tayari...nikajikokota kuelekea kwenye gari yangu na kuelekea polisi kutoa taarifa niweze kupata matibabu,nilipofika nikaaandika statement nikapewa namba ya case CD/RB/6848/10 pia nikapatiwa PF3 nikaenda hospitali nikapata matibabu,sasa hivi niko kitandani siwezi kutembea vizuri,pia nitashindwa kuperfom kwenye harusi ambayo tayari nishalipwa pesa tayari.SWALI langu ni kwanini ameamua kunidhalilisha vile mbele ya CLUB na FANZ ambao nilikua nawatumbuiza?kwanini ameamua kuniharibia kazi yangu?kwanini ameamua kunipiga bila ya kumkosea?JE NI SAWA HIVI JAMANI....naona MACHOZI YANANITOKA SINA CHA KUMUELEZA MAMA YANGU.

source http://topbandtz.blogspot.com/

story mbona hazieleweki!
 
Tatizo kubwa la huyu dogo ni ulimbukeni na kutokuwa na mtu wa kumuongoza.....mama yake ange play role kubwa katika hili (ingekuwa ni wenzetu) lakini mpaka azoee usupa staa itakuwa too late already.....we angalia actions zake, anavyoji-express etc..ni kichefuchefu sana....

Hasheem, hatuna budi kukwambia kama tuliokutangulia kwa mambo mengi, kwa mfano hayo Ma Vogue tunayasukuma siku nyingi hapa umatumbini, hapa kwetu siyo ishu, we angalia barabarani zilivyo za kumwaga na bado tuna SUVs nyingine kama kawa...na mijengo ndiyo balaa..lakini inatokana na mazoea ya hivi vitu...

Hizo hela kibongobongo zinazonekana nyingi lakini kwa style na level ya maisha ya USA, kuangukia pua ni dk 2.. mi nakuambia ukweli kama kaka ako wala sikuonei wivu sababu niko kwenye mstari ulioonyooka sihitaji hata senti ya mtu moja--HEBU KUA!
 
Sawa "kaka yake Hasheem"..nakubaliana na ushauri wako wa busara wa maisha ya kijana au mdogo wako...hapa pia naona kama tunakimbilia kumlaumu Hasheem bureee...kuwa superstaa hakumfanyi mwanadamu kuwa malaika na akiudhiwa na wapuuzi type ya kina TID asikasirike na ku-react accordingly...

Hivi nyie wadau mnamfahamu vizuri TID na kero zake???..au mnamsikia tuuu juu juu...dogo ni fara mbayaa...kiujumla ni mngesee sanaa...sasa yeye anapomletea Hasheem upuuzi ambao hata mie angeniletea ningemtuliza kadri ya uwezo wangu....

Pia ikumbukwe Hasheem kuja bongo..aka... nyumbani sio dhambi na hagombwi wala kukatazwa kuja kuwajulia hali ndugu jamaa na marafiki achilia mbali mama yake mpenzi na mzazi wake wa pekee....

Kuhusu kununua magari ya kifahari...mie pia sioni tatizo katika hilo..unless mniambie sie watoto toka chokambaya familiez tukizipata tuendelee kuendesha vi-korora limited basi ndio nyie wengine muendeshage mi-vogue....

Kuhusu kujiachia uswazi na starehe mnazodai sio za adhi yake ..naona mnataka hasheem ajijengee billionaires club yake akija bongo aje na mastaa wenzake wa nba akiondoka ifungwe...haiwezekani hata kidogoo...UKIENDA ROMA FANYA KAMA WAFANYAVYO WARUMI...na mkataa kwao MTUMWAA.

Kwa kweli mie naungana na Hasheem katika harakati za kutetea haki zangu za msingi no matter how high or low i am to my society

hat i see ni kwamba anataka kulipwa tu hana lolote, anatafuta njia ya kutokea. eti alipigwa akazirai, ooh hawezi kutembea, yuko kitandani hawezi kuperfom kwenye harus, what a pity! yawezekana alimkorofisha mwenzie kwa makusudi ili ampige na kumlipa. Idiot TID, grow up.
 
[COLOR=Red said:
hivi nyie wadau mnamfahamu vizuri tid na kero zake???..au mnamsikia tuuu juu juu...dogo ni fara mbayaa...kiujumla ni mngesee sanaa...sasa yeye anapomletea hasheem upuuzi ambao hata mie angeniletea ningemtuliza kadri ya uwezo wangu....[/COLOR]
yote uliyosema ni kweli kabisa mkuu hatukatai,na kuhusu T.I.D,ni kweli pia kajamaa kana maudhi sana hasa kakishapuliza ndumu kanakera mno aisee,kaliwai kuniuliza siku moja`` unanijua mimi nani wewe``nilikakosa ngumi moja kali sana mungu jaalia.tunachosema huu ugomvi ni too low kwa hasheem ku react,halafu ukizingatia yuko na wapambe,sielewi wapambe kazi yao nini,alitakiwa awaachie wao hiyo kazi ya kumpa displine.
 
hat i see ni kwamba anataka kulipwa tu hana lolote, anatafuta njia ya kutokea. eti alipigwa akazirai, ooh hawezi kutembea, yuko kitandani hawezi kuperfom kwenye harus, what a pity! yawezekana alimkorofisha mwenzie kwa makusudi ili ampige na kumlipa. Idiot TID, grow up.

Sijajua TID ni wa Kabila gani, manake kama anatokea kule Mbeya au Kagera, kupigwa na mtu maarufu kama Hasheem Thabiittiiii ni sawa na kugongwa na gari kama Aston Martin au Vogue. Inakuongezea umaarufu zaidi!
 
Ilikua majira ya saa kumi unusu nikiwa natoka club billcanas pamoja na rafiki yangu ANNA tukiongozana kuelekea mlango mkubwa wa kioo nikiwa naongea na simu na Hisbert kwa sauti ya juu maana kelele za muziki zilikua zinasumbua nikiwa nimesimama nje ya mlango wa kioo ghafla akatokea bwana HASHIM ambaye alikua counter akiongea na wakata ticket akaja nje na kunipiga bonge la mtama nikaaunga chini ya sakafu na kuzirai kwa dakika kadhaa,mabaunsa wakanibeba na kuniweka pembeni maana nilikua mlangoni,nilipozinduka nilisikia maumivu makali kwenye mabega,mkono wangu wa kulia na mguu ambao unafanya kutembea kwangu kwa taabu,nikaangalia mkononi simu yangu sikuiona tena,nikawauliza mabaunsa wake jamaa amekwenda wapi!wakadai ameondoka tayari...nikajikokota kuelekea kwenye gari yangu na kuelekea polisi kutoa taarifa niweze kupata matibabu,nilipofika nikaaandika statement nikapewa namba ya case CD/RB/6848/10 pia nikapatiwa PF3 nikaenda hospitali nikapata matibabu,sasa hivi niko kitandani siwezi kutembea vizuri,pia nitashindwa kuperfom kwenye harusi ambayo tayari nishalipwa pesa tayari.SWALI langu ni kwanini ameamua kunidhalilisha vile mbele ya CLUB na FANZ ambao nilikua nawatumbuiza?kwanini ameamua kuniharibia kazi yangu?kwanini ameamua kunipiga bila ya kumkosea?JE NI SAWA HIVI JAMANI....naona MACHOZI YANANITOKA SINA CHA KUMUELEZA MAMA YANGU.

source http://topbandtz.blogspot.com/

Ukiisoma hiyo statement ambayo TID ameiweka kwenye blog yake it's obvious kuwa ana mpango wa kumchomoa pesa Hasheem. Hiyo kusema bodily harm, loss of income kwa kushindwa ku-perform kwenye harusi na future events, loss of property (mobile phone handset), etc. Hapo anatengeneza mkao wa kula tu.

Kitendo chake cha kufungua RB ni wazi kuwa anataka kutengeneza mazingira ili Hasheem atoe pesa to settle the matter out of court. Kwani superstar huyu wa NBA akiwa na criminal case kortini itamsababishia matatizo makubwa huko kwenye kazi yake Marekani. Nadhani hii itakuwa fundisho kubwa kwa Hasheem na masuper star wengine kuwa makini sana na personal conduct zao.

Swali dogo la kujiuliza, Je TID angepigwa mtama na kijana wa MBAGALA angeenda kufungua RB polisi na kutoa official statement kusema kaumia na amekosa kipato kutokana na kipigo? Pia TID aeleze ukweli kuhusu ugomvi, sidhani kama Hasheem alimshambulia tu TID bila sababu yoyote.
 
:llama:strategy bwana..T.I. D tayrai yupo kwenye kumbukumbu za magereza, tabia za mfungwa hata akitoka jela huwa zinabadilika kwa muda sana na hata katika kuomba nafasi nyeti za kazi ua hati pasi ya kusafiri nk huwa wanakuuliza moja ya kigezo ni kama ulishwahi kupatikana na hati yotote ya jinai kwani inafahamika kuwa watu wengine uharifu upo damuni. T.I.D ni mkorofi na pengine kweli anataka kupanda chati kupitia jina la Hasheem. Lakini bado binafsi naona Hasheem nae ni limbuke wa kutupwa, hajastaarabika hata kuweza kujua nafasi yake katika jamii ni ipi. Shida hii imekuwa kwa masupa staa wengi sana wa kibongo hata kama atakaa nje ya nchi ulimbukeni upo pale pale.

Wapo wale ambao wakiwa Dar akisafiri mikoani nae anataka aonekane huko ni supa staa..atawauliza wenyeji kama "mnanijua mimi" iwapo hawamtazami!. Hasheem ameonyesha taswira hiyo hiyo ya kutaka kunyesha kuwa yeye ni nani kwa watanznia wenzake kupitia kipondo. Hata kama ni maarufu vipi, kuvunja sheria hakukupi umaarufu...kwa kusema "yeye ni mtoto wa Sinza" au whichever bado pia hakumaanishi upo juu ya sheria kuwashuhulikia wengine ipasavyo.

Hasheem kama atajieshimu ataishia kubaya na atapoteza jina muda si mrefu kama huyo T.I.D. Dunia ina mambo. maisha si kulasimisha watu wakuone wewe ni nani ila acha wao ndo wajilazimishe kukujua wewe ni nani. Vinginevyo Hasheem atapoteza kwa kucheza cheza na watoto wa mchangai kama akina T.I.D.
:blah:
 
Tusiwe wepesi kwa kumlaumu TID, au Hasheem kwa kusikiliza story ya upande mmoja.
Some explanations in here don't make sense at all. Eti mtu kwa sababu ana hela asiende kuona wazazi na jamaa Tanzania badala yake awe anaenda St. Tropez na Hawaii, are you for real ??? Au kwamba Hasheem anaenda likizo nyumbani eti kwa sababu hajulikani Marekani !! Ukweli ni kwamba Hasheem anajulikana US , sio kujulikana kama Obama, au Michael Jordan, au Kobe. Lakini anajulikana kwa kiasi cha kutosha tu, i know, because i have witnessed it.
Let us wait for explanation from the other side as well, before we starting judging people.
 
Grizzlies' Thabeet didn't knock out R&B singer

By Mark J. Miller

Memphis Grizzlies center Hasheem Thabeet(notes) was out at a club last weekend with his three bodyguards and some kind of scuffle happened in another part of the place. He supposedly was removed from the club but then got to hear later that not only was he supposedly involved in the little tiff, he had apparently knocked out R&B singer T.I.D.

Thabeet's agent is saying that his client was in a private part of the club when the fight broke out and had absolutely nothing to do with it, according to Fox TV in Memphis.

The agent is thinking that T.I.D. wanted some publicity and some extra airtime on the radio
Jamaa amekuja na mabaunsa kutoka US?
 
Huyu kijana si alishawahi kualikwa Ikulu yetu kama mgeni maalumu wa presidaa? Ikulu yetu bwana kweli uchochoro, hata hawajachunguza kama jamaa ni mhuni tuu?
 
Hawa maceleb wabongo mabwege kweli? Huyu Hasheem mwenyewe hata kikapu chenyewe hakiwezi basi wanasumbuuuuaaaaa
 
:llama:strategy bwana..T.I. D tayrai yupo kwenye kumbukumbu za magereza, tabia za mfungwa hata akitoka jela huwa zinabadilika kwa muda sana na hata katika kuomba nafasi nyeti za kazi ua hati pasi ya kusafiri nk huwa wanakuuliza moja ya kigezo ni kama ulishwahi kupatikana na hati yotote ya jinai kwani inafahamika kuwa watu wengine uharifu upo damuni. T.I.D ni mkorofi na pengine kweli anataka kupanda chati kupitia jina la Hasheem. Lakini bado binafsi naona Hasheem nae ni limbuke wa kutupwa, hajastaarabika hata kuweza kujua nafasi yake katika jamii ni ipi. Shida hii imekuwa kwa masupa staa wengi sana wa kibongo hata kama atakaa nje ya nchi ulimbukeni upo pale pale.

Wapo wale ambao wakiwa Dar akisafiri mikoani nae anataka aonekane huko ni supa staa..atawauliza wenyeji kama "mnanijua mimi" iwapo hawamtazami!. Hasheem ameonyesha taswira hiyo hiyo ya kutaka kunyesha kuwa yeye ni nani kwa watanznia wenzake kupitia kipondo. Hata kama ni maarufu vipi, kuvunja sheria hakukupi umaarufu...kwa kusema "yeye ni mtoto wa Sinza" au whichever bado pia hakumaanishi upo juu ya sheria kuwashuhulikia wengine ipasavyo.

Hasheem kama atajieshimu ataishia kubaya na atapoteza jina muda si mrefu kama huyo T.I.D. Dunia ina mambo. maisha si kulasimisha watu wakuone wewe ni nani ila acha wao ndo wajilazimishe kukujua wewe ni nani. Vinginevyo Hasheem atapoteza kwa kucheza cheza na watoto wa mchangai kama akina T.I.D.
:blah:

wakamwulize JERRY MURO:hug:
 
Back
Top Bottom