Has Kikwete lost his "Legitimacy" to Lead?

swali/hoja ni has JK lost his legitimacy to kead Tanzania? kuna mchangiaji ambaye ameuliza legitimacy na inapatikane/inapoteaje. nadhani tunapaswa kuanzia hapo.

nijuavyo mimi JK had legitimacy to lead this country kwenye awamu yake ya kwanza. baada ya watz kutoridhika na utendaji wake, hawakumchagua kuwaongoza kwenye uchaguzi wa mwaka jana. badala ya kukubaliana na maamuzi ya watz, tume na watendaji wa chinichini walichakachua matokeo na kumpachika ushindi. from thereon, JK has no legitimacy ya kuongoza nchi ya watu wasiomtaka. kwa hiyo haya mengine yote yatokeayo, hayawezi tena kumwongezea/kumpunguzia legitimacy, ambayo in the first place HANAYO!
 
Nimekupata mkuu,ila ya kwamba legitimacy inapoteaje na kupatikanaje,hilo tumelizumgumzia,pia rejea kwenye original post.

Kama kuna ushahidi wa hilo la kuchakachua uchaguzi,then yes ilegitimacy queastions should be raised,hamkufanya hivyo,sasa hii ya uhujumu uchumi.

Legitimacy pia inaweza kupotea kama akitumia nguvu ya dola vibaya,there are many instances that a leader can loose his legitimacy to lead...

Gaddafi walisema yake ilianzia alipotumia ubabe ama nguvu ya dola dhidi ya umma,it just depends.

Kwenye hili mimi naona uhalali wa kuongoza JK hana tena,hana nguvu ya kutulinda yeye kama amiri jeshi mkuu,kuna udhaifu ambao emepelekea yeye kukosa uhalali wa kuendelea kuongoza taifa.

Unless anaongoza banana republic!
 
Imebidi nicheke sana.
Mkuu mimi na mambo ya siasa nilikuwa mbali mbali,nikawa natemebelea JF kama guest,zikalipuka zile kasfa kuanzia Buzwagi,Kagoda,MEREMETA,EPA nk. Nikajiunga na JF,na kwa mara ya kwanza nikawa nafuatilia sana haya mambo.

Sasa nimechoka kabisa,nimeshakaribishwa na kina Asha D kule kwenye chit chat,inaonekana ninaweza kuendelea kutumia kule zaidi.

Haya mambo kama una akili na uwezo wa kufikiri hayafai kabisa kuyaona!

Mkuu kweli ni vitu gani hivi?

Ukifuatilia siasa za bongo you can go crazy!
 
Naomba ufafanuzi hapa. Kwanza, EL alimshauri JK kuvunja mkataba. Ulikuwa wakati gani? baada ya wapinzani kulalamika kwa wananchi na bungeni au kabla? Pili, kabla ya wapinzani kulalamika nani alikuwa kinara wa kuingia mkataba na Richmond? Pengine majibu ya maswali haya yanaweza yakatupa picha zaidi ya hali halisi ya purukushani hii ya aina yake.
 
Uhalali wa sababu ya kujiuzulu kwa EL ulipotea pale ilipogundulika kuwa haikuwa sababu hiyo ya kujiuzulu kwake ama ushahidi ulitumika kumu implicate haukuwa wa ukweli.

Kwamaana ya kwamba alijiuzulu kwa kutumia ushahidi potofu,hilo tayari linaondoa uhalali wa sababu ya yeye kujiuzulu...

Hilo pia limepelekea legitimacy ya mkuu wa nchi kuongoza kupotea kwasababu sasa ushahidi una muimplicate yeye directly,na machoni pa watanzania alioapa kuwalinda dhidi ya maadui wa ndani na nje,ikiwa ni pamoja na uchumi,na kuwajibisha wala rushwa,kuwaongoza na kuwaambia ukweli,siyo tu credibility yake imekwisha,bali uhalali kabisa wa kuendelea kuisimamia katiba hii aliyoapa kuilinda haupo.

Nadhani hapo ndipo penye shida kwa wengi wetu kupaelewa.
 
Kwa mujibu wa EL huko kwenye kikao chao cha NEC,ni wakati bunge lilipogunduwa kuwa kampuni hiyo ni feki na kwamba serikali inatakiwa iwalipe hao RICHMOND $100,000 kwa siku!

Na pia kwa mujibu wa EL,kinara wa kuingia mkataba huo ni JK,yeye alikuwa mtekelezaji wa amri kutoka juu.

EL alimpigia JK simu wakati JK akiwa nje ya nchi...

Habari ndo hiyo,pitia posti za nyuma tumeshalizungumzia hilo.
 
Tunakaribia pazuri Jmushi....soon tutafika kweli nakwambia wacha hii mbegu mpya ya richmond isambae kwanza,.kisha taji la miba litavishwa tu kwa msaliti wa hii nchi
 
Kwa mujibu wa EL huko kwenye kikao chao cha NEC,ni wakati bunge lilipogunduwa kuwa kampuni hiyo ni feki na kwamba serikali inatakiwa iwalipe hao RICHMOND $100,000 kwa siku!

Na pia kwa mujibu wa EL,kinara wa kuingia mkataba huo ni JK,yeye alikuwa mtekelezaji wa amri kutoka juu.

EL alimpigia JK simu wakati JK akiwa nje ya nchi...

Habari ndo hiyo,pitia posti za nyuma tumeshalizungumzia hilo.
Mimi nadhani mnaupotosha ukweli.

So far, Lowasa amesema yeye alitaka kuuvunja mkataba wa Richmond akaambiwa atulize boli. Huwezi kuuvunja mkataba kama tu huna akili kichwani mwako. Kuingiza Dowans badala ya Richmond was the best solution.

Umeme ulikuwa unapatikana kwa bei nafuu kuliko mikataba mingine, mpaka bunge letu puuzi lilipoamua kuuvunja huo mkataba na matokeo yake ni mgao wakati umeme upo, na malipo ya mabilioni.

Nataka nijue ni nani aliwaambia Tanesco waingie mkataba na Richmond?

Huwezi kuvunja mkataba kigangwe kama mnavyofikiri, hata mkienda mahakama yeyote duniani mnakuwa mnaonekana vichekesho.

Lowassa atuambie nani aliwapa mkataba Richmond, asituambie nani alitaka kuuvunja, hiyo haitusaidii.
 
SOBY said:
Lowassa atuambie nani aliwapa mkataba Richmond, asituambie nani alitaka kuuvunja, hiyo haitusaidii.
Lowassa awaambie mara ngapi?

Ama unazungumzia kitu gani mkuu?

Umeshaambiwa aliongea na JK akiwa nje ya nchi na akapewa go ahead,maneno hayo alimwambia JK mwenyewe na Mkapa ndo akamwambia JK auchune tu asije akaja tolewa nishai.
 
Uhalali wa sababu ya kujiuzulu kwa EL ulipotea pale ilipogundulika kuwa haikuwa sababu hiyo ya kujiuzulu kwake ama ushahidi ulitumika kumu implicate haukuwa wa ukweli.

Kwamaana ya kwamba alijiuzulu kwa kutumia ushahidi potofu,hilo tayari linaondoa uhalali wa sababu ya yeye kujiuzulu...

Hilo pia limepelekea legitimacy ya mkuu wa nchi kuongoza kupotea kwasababu sasa ushahidi una muimplicate yeye directly,na machoni pa watanzania alioapa kuwalinda dhidi ya maadui wa ndani na nje,ikiwa ni pamoja na uchumi,na kuwajibisha wala rushwa,kuwaongoza na kuwaambia ukweli,siyo tu credibility yake imekwisha,bali uhalali kabisa wa kuendelea kuisimamia katiba hii aliyoapa kuilinda haupo.

Nadhani hapo ndipo penye shida kwa wengi wetu kupaelewa.
Hakujiuzulu kwa sababu ya kushindwa kuuvunja mkataba, bali kwa kuhusika kuuleta huo mkataba.
Mbona Pinda haadhbiwi kwa kusimamisha malipo DOWANS?
 
Lowassa awaambie mara ngapi?
Ama unazungumzia kitu gani mkuu?
Ni lini lowasa alisema JK ndiye aliyeileta Richmond?
If you want to create illegitimacy, nadharia iweke pembeni, bring s some facts at least a memo or a witness from TANESCO.
 
Hakujiuzulu kwa sababu ya kushindwa kuuvunja mkataba, bali kwa kuhusika kuuleta huo mkataba.
Mbona Pinda haadhbiwi kwa kusimamisha malipo DOWANS?
Exactly!

Na ndizo tuhuma alizokuwa akizijibu EL huko kwenye kikao cha NEC,kwamba nani ni RICHMOND!
 
This war is "umoja wa wahalifu mafisadi (EL) backed by churches VS. JK goverment no more truth than this..
 
This war is "umoja wa wahalifu mafisadi (EL) backed by churches VS. JK goverment no more truth than this..
Ni kipi ambacho wewe unadhani JK angekifanya kumlinda EL?

Ni wazi alishindwa,alijaribu kwa kusema ni "Ajali ya kisiasa"

Lakini kwasababu mwezake nayeye ana ambitions za urais, basi tumegunduwa kuwa aliyetakiwa kujiuzulu ni nani.
 
JK mkuu halindi mtu yeyote katika nafasi yake ..anachofanya anakupa nafasi kama rafiki yake lakini nafasi hiyo utailinda mwenyewe kwa utendaji wako na kuwajibika kwako..

Kuhus EL niliwahi kuandika hapa kuwa "kilichotokea ni kwamba JK alimwambia EL clean the mess" akashindwa kuwa handle kina mwakyembe before kupeleka hilo jambo bungeni japo alikuwa na nafasi kama PM ku-pre-empt hizo findings na allegations akawaomba/ongea nao kiutu uzima/kiuongozi wapeleke ripoti nzuri akashindwa..

Alitegemea urafiki wake na JK, ikala kwake kama ambavyo kina mattaka, mramba, mgonja etc walitegemea rais atawasaidia kama alivyo fanya Mkapa lakini JK anastahili tofauti kabisa...clean the mess yourself otherwise you quit..ndio maana ngeleja haondoki kwasababu anajua kuchakachua tume..za bunge..

EL akaanza kampeni zake kwenye makanisa (Sumaye na Mkapa wakaingia kichwa kichwa based on church background) lakini anaendelea na anataka kuleta mgawanyiko mkubwa wa jamii ya kitanzania..
 
Exactly!

Na ndizo tuhuma alizokuwa akizijibu EL huko kwenye kikao cha NEC,kwamba nani ni RICHMOND!
Nani ni Richmond?..
Naomba usipindishe ukweli bro, Lowassa hajamake statement yoyote inayomuimplicate JK kama ni owner au facilitator wa Redevco.
Who brought Redevco in the picture? Walipatikanaje?
 
Kwahiyo SOBY and Topical mnachotaka kusema hapa ni kwamba ugomvi kati ya EL and JK ni kuhusu kuvunjwa kwa mkataba siyo na siyo kuletwa kwa RICHMOND?

Ok,mnachotaka kusema kuwa Waliokataa kuvunja mkataba hawahusiani na RICHMOND?Na pia wale walotaka uvunjwe pia na wao ndo walieta RICHMOND?

Mnaona mnavyoji confuse?

Basically mnataka kusema JK and EL wanagombana ugomvi usokuwa wao?
 
Mkuu,

Mimi ninavyofahamu issue ya EL kujiuzulu ni kwamba ni makosa yake wala si ya JK (yaani kakosa busara za uongozi akategemea urafiki wake na rais basi)

Makosa aliyofanya na anayofanya ni:

Mosi: kushindwa ku-handle tume ya mwakayembe in first place ni weakness kubwa sana (hakufanya homework yake kama PM na leader) ambacho hata ngeleja anamshindwa au dharau au kiburi inamsumbua nionavyo mimi.

Pili: Baada ya ile mess alimtegemea JK pekee lakini JK akamwambia aende aka clean the mess peke yake bungeni akashindwa akazira (BIG mistake)

Tatu: anaendeleza siasa za majitaka na uasi na makundi ambayo for sure analigawa chama chake (hana busara) mwisho wa siku anajitengenezea maadui wengi kuliko marafiki wa ukweli hapo ndio tofati ya JK na EL, lowassa hana rafiki wa ukweli zaidi ya watu anao bull kwa pesa wakati ana marafiki wa ukweli waliomjenga na kumwamini akiwemo yeye..
 
Kwahiyo SOBY and Topical mnachotaka kusema hapa ni kwamba ugomvi kati ya EL and JK ni kuhusu kuvunjwa kwa mkataba siyo na siyo kuletwa kwa RICHMOND?

Ok,mnachotaka kusema kuwa Waliokataa kuvunja mkataba hawahusiani na RICHMOND?Na pia wale walotaka uvunjwe pia na wao ndo walieta RICHMOND?

Mnaona mnavyoji confuse?

Basically mnataka kusema JK and EL wanagombana ugomvi usokuwa wao?
Kulikuwa na kamati tatu mkuu,
Kamati ya makatibu Wakuu (Nishati, Fedha)
Kamati ya wanasheria
Kamati ya wataalam.
JK aliongea na kamati ya maPS, akaambiwa aache Richmond, Dowans ikauchukua mkataba, na Tanesco wakalipwa hela zao due to incapacity.Hapo mimi sioni kosa.
Kamati ya wataalam, ndiyo iliyokuwa inashughulika nani apewe contract na Ofisi ya waziri mkuu ilikuwa inafuatilia kwa ukaribu mchakato mzima.
Msabaha na balozi Kazaura waliiambia kamati ya bunge kuhusu Richmond kuwa ni kampuni ya Lowassa na Rostam.... mbona hamzungumzii hili?
Mbona hamzungumzii mkataba uliosainiwa kati ya Yona na Gire kuhusu bomba la mafuta?
Tusidanganyane, Mkapa,Yona , lowassa na sumaye ni maswahiba waliojitahidi kutengeneza fedha nyingi through energy na ni lazima wawajibishwe, ikiwezekana wanyongwe.
 
Back
Top Bottom