Afadhali wao CUF wameleta kitu cha kujadili yaani document rasimu na mapendekezo yao, chadema hawana muda wa kuandaa hata mapendekezo lakini kila siku wanadai...aise kelele nyingi utendaji zero.
CUF ni chama kimechuja, kinatafuta kuregain kutumia cheap popularity. Hiyo rasimu zero ya katiba iliandaliwa na vyama vyote vya upinzani ikiwemo chadema, na hiyo rasimu haikuwahi kufikishwa kokote. CUF wameiibua bila hata kuifanyia review kuona kama kuna kitu kimebadilika toka itengenezwe na wakaipeleka kwa waziri husika. Kama sio kutafuta umaarufu, kulikuwa na haja gani ya kuipeleka kwa maandamano na bila kujali kuwa yemezuiliwa na polisi
CUF ni "Bata" kama alivyosema Mwanasheria Mkuu Jaji Werema, wanapiga kelele, kudai kwa nguvu, ili iwape ccm na serkali yake nafasi ya kusema kuwa mnadai katiba kwa nguvu. Chadema inapeleka hoja Bungeni, ili kuunda utaratibu, nadhani issue hapa sio katiba mpya kwa kuwa hilo limeshapita hata JK kailikubali, issue ni utaratibu gani unafaa wa kukusanya maoni. CUF hiyo ya kwao sijui ilikusanywaje kama sio ile rasimu ya vyama vyote. Tukishakuwa na one central point ya kukusanya maoni kila wadau watapeleka maoni yao kwa utaratibu utakaokubalika, si kwa maandamano wala kupigana virungu!!
Kimsingi CUF walichemka, na of all stupid thing they did kumpelekea Celine Kombani, that was mistakes na hotuba ya JK ya 31st imewaumbua sana sana. Ni vyema CUF wakajua kuwa kwa mwendo huo wanazidi kujipunguzia umaarufu, kwani wamechemsha issue ya Zenji sasa inabidi kujitafakari ili kuona jinsi ya kuifanya iwe na umaarufu stahili TZ Bara.
I want to believe kuwa CDM wanafanya vizuri, kudai katiba hii kwa utaraibu ule unaokubalika na ambao hautakuwa na vurugu. Huo mtego wameuvuka kwani CCM ilishailabel CDM kuwa ni chama cha fujo. Kuipeleka bungeni is the most smart move kuliko kuwawasilisha rasimu 0 kwa maandamano, halafu walioandamana wenywe hawajui hata maana ya katiba loh