Harufu ya Rushwa?

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,724
Ndani ya wiki mbili ambazo zinaisha leo, Halmashauri ya Wilaya ya Meru walitoa Tangazo kuwa kuna viwanja 70 vilivyopimwa, hivyo wananchi wanatakiwa kuchukua fomu kwa tshs 10,000/= na kuzijaza!

Wajanja tukawahi mapeema na tukajaza hizo fomu!...Lakini cha ajabu nimepita huko leo, nikakuta list ya watu walioomba viwanja hivyo 70 kwa sasa imepita 2600, na bado milango iko wazi, na hela inazidi kupokelewa!
Na strictly viwanja viko 70!

Hii mambo ikoje wandugu?..Hiyo si dalili ya ufisadi na kujipatia mapato isivyo halali kwa wakuu wa Manispaa hii?...Nimeachwa hoi!...Labda mnisaidie wandugu...!
 
Hapo munaibiwa kupitia uuzwaji wa fomu, kwani kitachofuata ndiyo watateuliwa wanunuzi halisi, ambao nahisi wako tayari wameteuliwa na nyie ni wasindikizaji. Hapo ulipo elewa kuwa umeishaibiwa na kiwanja hupati, afadhali hiyo shs 10,000 ungekuwa umenunua nyama, maziwa au mayai ungekula upate virutubisho, sasa warutubisha watu wa halmashauri!!

Nchi hii tambarare bwana, kwani hata mie nilishangaa kuona shule nyingi za private zinauza fomu za kuomba kuingia kidato cha kwanza hadi 3000 wakati wanajua nafasi wanazo 90 au 135 tu. Check sasa mwanao akifanya mtihani, walimu au mawakala wao wanaanza kuwatafuta wazazi na kuomba laki 2 (200,000/=) za kusaidia kurekebisha matokeo!! Sijui nchi hii tuikimbie twende Botswana au Dubai?? No body is taking any action!!!
 
jamaa ni wezi sana hawa hata kuna jamaa mmoja pia ae alikua analalamika hivyo hivyo. Unajua huu ni wizi hata huko bagamoyo tuliomba viwanja toka mwaka 2005 na tumekwishalipa kila kitu lakini hadi leo bado hatujapata na kila siku wanatoa majina machache machache ya watu wanaopewa viwanja na kama ukienda na pesa ya rushwa unauziwa hata kama haupo kwenye list inakera sana hili jambo la viwanja, yaani kwenye hizi halmashauri kuna urasimu sana
 
Hapo munaibiwa kupitia uuzwaji wa fomu, kwani kitachofuata ndiyo watateuliwa wanunuzi halisi, ambao nahisi wako tayari wameteuliwa na nyie ni wasindikizaji. Hapo ulipo elewa kuwa umeishaibiwa na kiwanja hupati, afadhali hiyo shs 10,000 ungekuwa umenunua nyama, maziwa au mayai ungekula upate virutubisho, sasa warutubisha watu wa halmashauri!!

Nchi hii tambarare bwana, kwani hata mie nilishangaa kuona shule nyingi za private zinauza fomu za kuomba kuingia kidato cha kwanza hadi 3000 wakati wanajua nafasi wanazo 90 au 135 tu. Check sasa mwanao akifanya mtihani, walimu au mawakala wao wanaanza kuwatafuta wazazi na kuomba laki 2 (200,000/=) za kusaidia kurekebisha matokeo!! Sijui nchi hii tuikimbie twende Botswana au Dubai?? No body is taking any action!!!

Sa nifanyeje ndugu...nikiwavamia ofisini watanifunga wale...! We hujasikiaga M.P.Pinda akisema kuwa Mafisadi wana nguvu sana?

Yani nikubali pesaangu iliwe kirahisi namna hiyo wakati naona?

Nashangaa kuna ofisi nzuuuri ya TAKUKUNGURU(Masanilo Version) pale Ilboru, laki ni ndo sijui hawaoni majitaka haya yanayofanywa na Manispaa hii...

Bora kuhamia kwa CHIPO ZINDOGA!
 
Back
Top Bottom