Tatizo la kuwa na harufu mbaya kinywani (bad breath) - Chanzo, dawa za kuzuia na ushauri

Hilo tatizo lako hata me nilikuwa nalo but sa hv limeisha linasababishwa na dawa za mswaki tunazotumia whtdent clget na n.k kwan zina floride ukitaka kujua madhara yanayosababishwa na floride nenda YOUTUBE andika hivi EFFECT OF FLORIDE IN BODY ITAKULETEA VIDEO YA DK 10 dawa me niliuziwa elfu 13 kama utaitaji sana nchek kwa no 0683672508 tatizo halitajirudia tena.
 
Una tonsil stones (Tonsilloliths)

Una kwangua ulimi wako wakati wa kupiga mswaki?

Unasafisha paa la kinywa chako wakati wa kupiga mswaki?

Fizi nazo unazisugua ukiwa unapiga mswaki?

Una floss kila siku?
 
Nilikuwa na tatizo hilo mara nyingi inasababishwa na vyakula vilivyojaa ndani ya ufizi katika maoteo ya meno ambapo huwezi kupapata kupasafisha kama unatumia mswaki, ni msafishaji meno aliyesomea kwa kazi yake ndiye anayeweza kufanaya hiyo kazi. Ushauri nasaha mkuu nenda kasafishe meno kwa msafishaji meno. hii huduma kwa tanzania sijuwi inapatikana wapi lakini mimi maranyingi hufanya huduma hii ninapokuwa matembezoni ng'ambo. Natanguliza shukurani.
 
50% ya WABONGO, WANANUKA mdomo!

Imeelezwa na wataalam wa afya kwamba zaidi ya asilimia 50 ya wabongo wana tatizo la kunuka mdomo kinomaaa. DuhhTatizo hilo tunaambiwa linasababishwa na magonjwa ya fizi na meno.Hayo yamo katika ripoti ya utafiti ilitolewa

jana jijini Dar es Salaam ktk mkutano wa mwaka wa Chama cha Madaktari wa Meno Tanzania (TDA).Dk Germana Lyimo wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,ambaye alifanya utafiti huo, alisema ulihusisha wanawake 400 wanaokwenda kwenye kliniki ya hospitali hiyo.Alisema ingawa tatizo hilo ni kubwa, lakini watu wengi hawajielewi kama wanatoa

harufu mbaya vinywani na kwamba mbaya zaidi, katika hali ya kawaida ni vigumu kwa mtu mwingine kumwambia mwenzake kuwa anatoa harufu mbaya."Kujisikia mwenyewe harufu yako ya mwili huwezi na hata kama ukijisikia

unaweza kuona kama ni hali ya kawaida wakati una tatizo kubwa,"alisema Dk Lyimo.
Alisema asilimia 90 ya ukubwa wa tatizo hilo, inatokana na watu kutozingatia usafi wa kinywa hasa kwenye fizi, meno na ulimi wakati asilimia 10 inatokana na magonjwa mengine yaliyoko ndani ya mwili wa binadamu.


Chanzo: 50% ya WABONGO, WANANUKA mdomo! | darhotwire


 
Halitosis -kutoa harufu mbaya mdomoni (kunuka mdomo)

husababishwa na
-chakula unachokula, kama vitunguu,samaki,vinywaji kama kahawa
-mdomo kukauka
-uvutaji wa sigara
-magonjwa kama kisukari na ugonjwa wa meno
-kutosafisha meno mara kwa mara
-unywaji wa pombe
-kansa
-infection bacteria au fungasi

tiba
-Hakikisha unasafisha meno ,ulimi na mdomo sehemu zote kwa dawa ya meno
-kama unaungonjwa hakikisha unatibu kwanza huo ugonjwa
-hakikisha mdomo usiwe mkavu
-kila baada ya kula blush meno yako ili kuondo mabaki ya chakula
-pima kama unainfection tumia antibiotic
 
Nina girlfriend wangu ana umri wa miaka 25 lakini ana tatizo la kunuka mdomo mpaka kufanya romance inakua shida. Yani nashindwa kuelewa, kwa sababu ni msafi sana anasafisha kinywa kila mara inavyotakikana lakini wapi.

Akilala na kuamka ndiyo kabisa kiukwel sijawahi kumwambia coz naona vibaya nifanyeje?

Naomba ushauri wenu na kama kuna doctor nasubil ushauri wake.

Samahan kama sijaweka sawa maneno yangu, ila naamini ntakua nimeeleweka.

=======

Kutibu Kunuka Mdomo Mtu

Mara nyingi mtu huwa hajijui kama anatoa harufu mbaya mdomoni mwake, hii ni kwasababu ya cells wa pua huwa tayari washajikubalisha na ile harufu ya mdomo na aghlabu humfanya mtu asijijue kuwa yeye anatoa harufu mbaya.

Kuna sababu nyingi zinazomfanya mtu atoe harufu mbaya ya mdomo miongoni mwao ni:-

Upungufu wa usafi
Mara nyingi mtu mwenye kutoa harufu mbaya huwa hashughuliki katika usuguaji mzuri wa meno,Hupiga mswaki juu juu tu.

Uutumiaji wa tumbaku na vitu kama hivo
Mtu mwenye kutumia tumbaku hufanya mdomo wake uwe na harufu mbaya hii ni juu ya bakteria wanaojijenga katika meno.

Matatizo ya Sinus (mvimbo/mzibo wa ndani ya pua)
Tatizo hili linaweza kumkuta mtu yeyote yule kwani maradhi haya yanatokana na allergies au enviromental situation.
Mara nyingi pua huziba na kusababisha makamasi kupita katika njia ya koo na huifanya koo kutoa harufu mbaya ambayo hupitia mdomoni.

Tonsis
Maradhi haya pia husababisha maradhi ya kutoa harufu mbaya mdomoni.

Na sababu nyengine ambazo husababisha maradhi ya harufu mbaya ni kama diabetes, kidney failure, Chronic Bronchitis & Decay teeth.

Lakini kama ilivyo kuwa hakuna maradhi bila dawa lakini dawa ya maradhi haya ni usafi wetu sisi wanaadamu.

Hizi ni njia ambazo zitamsadia mtu kuondosha harufu mbaya ya mdomo:

Mtu anapopiga mswaki ni lazima asugue ulimi wake mara tatu na kawaida ya kupiga mswaki upige kwa muda wa dakika 15.

Pia ni muhimu kwenda kumuona daktari wa meno muda baada muda

Tumia mswaki mmoja kwa muda wa miezi 3 tu baada ya hapo badilisha mswaki. Hii ni kuepuka kuumiza meno na mafizi kwa kutumia mswaki kwa muda mrefu.

Kila baada kumaliza chakula piga mswaki laa kama upo sehemu ambayo huwezi kupiga mswaki basi sukutua kinywa chako hadi uhakikishe huna mabaki ya chakula.

Kula Carrot kwa wingi baada kumaliza chakula

Kunywa maji mengi

Tumia mouthwash kwa kusukutua na hakikisha unapiga mswaki kabla ya kwenda kulala.Mkuu Kafuta Tupo hapa Ma Great Thinker.
 
Kunuka mdomo kuko tofauti,kuna kunuka mdomo kwa kawaida na kwingine ni ugonjwa.Harufu ya mdomo ya kawaida sehemu kubwa inatoka kwenye uchafu wa ulimi siyo meno.Ukiwa naye anagalia rangi ya ulimi wake,kama ni white kuna mkusanyiko wa mabaki mengi.

Asafishe ulimi,na kupiga mswaki wengine hawahui,hupiga meno ya chini tu yajuu hawahangaiki nayo.Try that,kijiko kimoja cha asali daily kinaweza saidia.

Usije ukawa wewe ndiyo una...just kiddin.Fanyia kazi hayo.Kama itakuwa bado seek medical advice.From my point of view.
 
Nina girlfrnd wangu ana umri wa miaka 25 lakin ana tatizo la kunuka mdomo mpaka kufanya romanc inakua shida.Yaani nashindwa kuelewa, kwa sbb ni msafi sana anasafisha kinywa kila mara inavyotakikana lkn wapi,akilala na kuamka ndiyo kabisa.Kiukweli sijawahi kumwambia coz naona vibaya nifanyeje?

Naomba ushauri wenu na kama kuna doctor nasubiri ushauri wake.Samahani kama sijaweka sawa maneno yangu,ila naamin ntakuwa nimeeleweka
.

Pole sana, mpeleke kwa dentist akamuangalia vizuri meno yake. Yawezekana mengi yameoza na hivyo kusababisha kutoa harufu mbaya kinywani, hivyo itabidi asafishwe vizuri hayo yaliyooza.

Ila mwambie pia awe anasafisha meno kwa uzi huku akipitisha kwa kila njia ya meno nayo husaidia kuondoa mabaki kwenye meno. Nahisi itamsaidia ndugu yetu.

Ila ngoja mzizimkavu aje atakusaidia pia.
 
Wengi wamekushaur lakin tafadhar kawaone madaktar Hasa pale Muhimbil jengo la Afya ya Kinywa na Meno.
 
Habari za kazi wanaJF. Ninaomba msaada wa kufahamu uhusiano kati ya harufu na tezi za mate. Huwa ninashangaa mtu akinua harufu mbaya mate yanajaa mdomoni lakini hayamezi bali anatema na kunakuwa na uafadhali fulani hivi, pia mtu akinusa harufu nzuri mate hujaa mdomoni lakini hayatemi, anayameza.

Jamani kuna siri gani ya uumbaji wa Mungu?
 
Dah hii itakuwa bomba sana alafu sijawahi isikia yaelekea haijulikani asante sana mtaalamu maana nondo zako yaelekea unachimba kwakuwasaidia watu
Mkuu Josephine03 dawa zangu hata uki google huwezi kupata huko ninako zipata si rahisi mtu kuzipata Dawa zangu ni za asili na zinatibu ile mbay hiyo ni

moja tu kati ya Dawa zangu zipo nyingi tu Dawa za kutibu kuondowa harufu ya mdomo.Na ingine hii hapa Dawa ya

kuondowa harufu ya Mdomo chukuwa kijiko kimoja cha Asali changanya na kijiko kimoja cha unga wa Mdalasini changanya na maji

ya moto glasi moja kunywa kila siku asubuhi kabla ya kula kitu utaweza kukaa kutwa nzima pasipo na mdomo wako kutoa harufu mbaya fanya hivyo kisha uje unipe feedback.
 
Last edited by a moderator:
Wadau mimi nasumbuliwa na tatizo la kutoa harufu mbaya mdomoni napiga mswaki mara kwa mara nasugua kinywa vizuri sana lakini nikikaa baada ya muda ukiongea harufu mbaya inatoka inanikera sana naombeni tiba sahihi ya tatizo hili kwa sasa natafuna sana banzoka angalau kupunguza harufu nisipotafuta banzoka hali ile ile naombeni msaada wenu
cha kwanza nakupongeza kwa kuwa muwazi, kujua tatizo na kutafuta suluhishi

tafuta mtaalam wa tiba ya kinywa, lakini pia baadhi ya harufu hutokana na matatizo yaliyo zaidi ya kinywa mfano, sinuses, mfumo wa chakula (harufu yaweza hata kutokea tumboni), mfumo wa hewa na shida nyingine very common pamoja na tonsils (pamoja na tonsils stones), sigara, pombe, matatizo ya figo na maini.... au hata kuoza kwa internal organs

for more info, google, kwa mfano link More on bad breath (Halitosis) | Go Ask Alice!

au ya tonsils stones GNARLY TONSIL STONE REMOVAL!!!! - YouTube

Tonsil Follicle - YouTube
 
Waungwana msaada demu kachomoa nisimkisi Kisa nanukia pombe nimekula bia kadhaa tumeingia gheto kakataa anakwepesha mdomo nimepiga mswaki bado harufu aiishi nifanyeje?kama kua Dawa ya kutafuna kupuliza nk nk msaada
 
Mh! Pombe ina harufu mbaya jamani. Kama sewage. Halafu ukichanganya na maroba unanuka kama spitali sijui?!! Kwanini ulazimishe kumkisi? Potezea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom