Chipolopolo
JF-Expert Member
- Feb 14, 2012
- 1,425
- 725
Chipolopolo,
Asante sana. Nakubaliana nawe kuhusu haja ya mimi kuweka ufafanuzi kuhusu picha za CUF Arusha kwenye Mjengwablog. Ukweli zimewekwa na mmoja wa walio kwenye timu ya Mjengwablog. Yumkini zina kasoro, lakini aliyeweka hakuwa na dhamira mbaya. Tukumbuke, hizi kazi zinafanywa na wanadamu. Makosa hutokea. Pale yanapotokea, basi, muhimu ni kukosoana ili marekebisho yafanyike.
Maana, ukiacha kublogu, nami nina kibarua changu kingine. Ndio maana ya kuwepo kwa wengine kwenye timu ya Mjengwablog ili wanisaidie. Na kutokana na kibarua changu, wakati mwingine yaweza kupita siku nzima au hata siku mbili bila mimi kuingia Mjengwablog. Na ninapoingia, nami naweza kuzishangaa picha za CUF Arusha kama wanavyoweza kushangaaa watembeleaji wengine. Na huo ndio ukweli kwa mazingira yangu ya sasa.
Usiku mwema.
Maggid
Iringa
0788 111 765
Maggid:
Huo ndio uungwana.Binafsi nimekuelewa vizuri, kabisa! Asante kwa kujali.