Harambee ya CHADEMA Arusha

Tunaomba mheshimiwa Mbowe mwenyekiti wetu atushirikishe na sisi tulio nje ya Arusha tujue njia tutakayoitumia kuchangia
 
Wakuu nasikiliza Clouds FM arusha, nimesikia tangazo ambalo Mwenyekiti wa Chadema na Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni Mh. Mbowe akiwakaribisha wafuasi wote wa chadema ktk harambee ya kuchangia chama ambayo itafanyika Naura Spring hotel tarehe 23/03/2012 kuanzia saa 1 jioni.Viva Chadema!

Unafaidika vipi na utajiri wa chama cha Mafisadi
 
Walalahoi wote nchini, tuchangie CHADEMA sasa hivi ili na sisi tupate kuwa WANAHISA katika kuwekeza kwenye juhudi za ukombozi wa taifa letu.

Kwa nini tujiruhusu kupoteza hii fursa nzuri sana kwetu kushirikishwa shughuli muhimu kama hivi kwa chama chetu?
 
TANGAZO KWA MARAFIKI WA CHADEMA

Mpendwa RAFIKI WA CHADEMA, napenda kukujulisha kuwa Ijumaa ya tarehe 23 Machi 2012, kutakuwa na hafla maalumu ya kukiwezesha chama itakayofanyika katika hotel ya NAURA SPRINGS, ARUSHA.

Tiketi zinapatikana kwa Mr Amani Golugwa 0754 912 914, na
Elifuraha Mtowe – 0754 710 077Hafla hiyo itarushwa LIVE NA STAR TV kuanzia saa 2 hadi saa 4 usiku.

Mh Freeman Mbowe (mb) na Katibu Mkuu Dr Wilbroad P Slaa watawaongoza wabunge wa chadema na marafiki wote katika mpango huu maalumu wa kuchangia chama wa "MOVEMENT FOR CHANGE".
Marafiki watakula chakula cha pamoja nakubadilishana mawazo.

Imetolewa na Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha,

Ng Amani S Golugwa
 
Mkuu si mngesema basi hata bei ya ticket nisije nikaharibu voucher yangu kumpigia Amani Golugwa nikakuta sina uwezo wa kununua ticket.
 
Mimi nitashiriki nanyi live kwa njia ya Mpesa. Kuchangia ukombozi live huku nchi nzima inaona kuna raha zake. Tuko pamoja.
 
Aiseeee! nilidhani watafanyia Dodoma, Tanga, Rukwa, Shinyanga au Pwani kumbe ni kule kule Arusha!
 
Hakuna shida sisi wengine tupo mbali na Arusha lakini tutashiriki kupitia Star TV kutoa michango yetu tupo pamoja Makamanda.
 
Hayo ni maeno wasiyo itakia meme chadema tafadhali changia ili uweze kukombolewa kama hutoweza kufika Naura tupia hata kwenye M_Pesa
Brother tunaendelea kuchanga, wacha wabeze kwani wao wanachukua za serikali. Wanatumia pesa za wizara wanazosimaia kufanyia kampeni. Hakuna lisilo na mwisho,tunao uchungu na nchi yetu mwisho haupo mbali.
 
Back
Top Bottom