Harakati za uamsho zaanza rasmi

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
[h=1]
lipumba.JPG
[/h]Written by ibnially // 10/09/2012 // Habari // 6 Comments


Na Masoud ali…
Waislamu nchini Zanzibar wamehimizwa kuwa na umoja na mshikamano katika kudai maslahi ya nchi yao. kwani umoja wa waislamu ndio utakaoleta ushindi licha ya kwamba wapo baadhi ya waislamu hawapo pamoja na wenziwao.
Hayo yameelezwa na Amir wa jumuiya ya uamsho Zanzibar {JUMIKI} wakati alipokua akiwahutubia waislamu wenye uchungu na kuchoshwa na muungano uliopo baina ya Tanganyika na Zanzibar katika muendelezo wa harakati za mihadhara ya kuamsha wananchi kuhusu matatizo mbali mbali yanayotokana na muungano.
Mhadhara huo ulifanyika katika msikiti wa Afraa kidongo chekundu ambao ulihudhuriwa na maelfu ya waislamu wanaume na wanawake kwa ajili ya kusikiliza kitu gani kipya kimejiri baada ya kuonekana kukaa kimya kwa harakati hizo kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Shekh Mselem amebainisha kuwa lengo la JUMIKI ni kutaka kurejesha heshima na hadhi ya Zanzibar kwa njia ya AMANI na utulivu bila ya kumwaga damu wala kupoteza roho za waislamu. Hivyo waislamu wasikubali kupotezewa lengo lao na baadhi ya watu wachache ambao wanapata maslahi kwa kuwakandamiza wenzawo.
Wakati huo huo naibu amiri wa JUMIKI fadhiilat shekh AZZAN amewapongeza waislamu kwa umoja wao waliouonesha katika kutii amri za viongozi wao dini hasa hasa kuhusu suala zima la sensa.
Vile vile amesisitiza ya kwamba JUMIKI hawajakaa kimya kama inavyodaiwa na baadhi ya watu amesema msimamo wake wa kudai maslahi ya zanzibar hauzimiki ingawa kuna mbinu nyingi zinaandaliwa juu yao za kutaka kuwapoteza viongozi wa harakati hizo.
 
Du at work again!!! Huko Zenj hapo 2015 sijui mambo yatakuwaje? Naomba uamsho sisitizeni muungano uvujwe kila upande uwe na serikali yake independent!!! Na nyie mnahitaj haki ya kujiwakilisha kikanda na kimataifa!!!! Hivi kule Afrika ya Mashariki mnawakilishwa au kujiwakilisha!!! Tukitengana itakuwa poa na fujo hatutaziona tena na CUF ibaki huko kwenu na huku Bara CDM. Angalau tujaribu tena vyama hivi pengine yale maisha bora yanaweza kupatikana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom