Harakati za kuondowa hukumu ya kifo vs hali halisi

Ngekewa

JF-Expert Member
Jul 8, 2008
7,705
1,288
Wanaoua albino nao wauawe-Mchungaji Saturday, 24 October 2009 05:01 *Asema Biblia inasema auaye kwa upanga atakufa kwa upanga
*Ni Mwenyekiti wa Kongamano la Wachungaji, Maaskofu 150

Na Elisante Kitulo


KUTOKANA na wimbi la mauaji ya albino kuendelea kuitikisa nchi, Serikali imetakiwa kutunga sheria mpya ili wale wote wanaohusika na mauaji hayo wauawe hadharani.

Hatua hiyo imekuja siku mbili baada ya mwanafunzi wa Darasa la Pili katika Shule ya Msingi Nyawilimilwa mkoani Mwanza, ambaye alikuwa na ulemavu wa ngozi, kuuawa kwa kukatwa shingo na mguu wake kunyofolewa.

Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste Mbeya Bw. William Mwanalanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kongamano la Wachungaji na Maaskofu wapatao 149 kutoka mikoa mbalimbali linaloendelea hapa jijini.

Mchungaji Mwanalanga alisema kutokana na wimbi la mauaji hayo kuibuka tena siku za hivi karibuni Serikali inatakiwa kuchukua hatua kali zaidi ili kukomesha mauaji hayo ikiwa ni pamoja na kutunga sheria itakayotoa hukumu ya kunyongwa hadharani kwa wauaji wa maalbino.

Alisema kuwa Haki za Binadamu zimekuwa zikitafsiriwa ndivyo sivyo jambo ambalo limechangia kuongezeka kwa uharifu katika jamii .

"Mimi pia ni mwanaharakati wa haki za binadamu, lakini haki hizo hazikukusudia kutetea uhalifu katika jamii zetu kama ilivyo sasa bali kuleta amani na utulivu, hata Biblia inasema auaye kwa upanga naye atakufa kwa upanga sasa ni vipi tupinge adhabu ya kifo kwa watu kama hawa?." alisema.

Akizungumza kwa uchungu mwingi Mchungaji Mwanalanga alisema inasikitisha sana kuona albino anauawa kama mnyama katika nchi yake na wahusika wakiendelea kuishi kupitia mwavuli wa haki za binadamu.

Aidha, Mchungaji Mwanalanga alisema kuwa kuna siri nzito inayowahusisha baadhi ya viongozi na wafanyabiashara maarufu hapa nchini na vitendo hivyo vya kinyama.

"Tumepokea taarifa kuwa kuna kijana aliyekuwa katika mtandao wa mauaji hayo ameokoka na yuko tayari kutaja orodha ya viongozi wanaohusika katika mauaji hayo, alisema.

Aidha, Mchungaji Mwanalanga alisema kuwa umoja wa wachungaji nchini utafanya maandamano makubwa kushinikiza viongozi wanaojihususha na mauaji hayo waondolewe madarakani na kuchukuliwa hatua za kisheria pale ushahidi utakapopatikana.

Alieleza kuwa Serikali inatakiwa kutangaza hali ya hatari katika mkoa wa Mwanza ikiwa ni pamoja na kuunda kikosi maalum cha askari kufanya msako na kuwakamata wanaohusika na vitendo hivyo.

Alisema anasikitishwa na kitendo cha wabunge wa Mkoa wa Mwanza kukaa kimya kama hawajuai nini kinatokea na kuwataka wachukue hatua za kukemea vitendo hivyo bungeni na kwenye majimbo yao ya uchaguzi.

Kongamano hilo linahusisha wachungaji na baadhi ya waislamu wenye utaalamu mbalimbali likilenga kutafuta namana ya kuisaidia Serikali katika sekta ya afya, maji na utunzaji wa mazingira.





JEE ZILE HARAKATI ZA KUONDOWA HUKUMU YA KIFO ZINASEMAJE KUHUSU KAULI HII?
 
Back
Top Bottom