Happyness Magesse anaulizwa Kiswahili anajibu Kiingereza

Pius Msekwa aliwahi kulauimiwa alipowaambia watu waache WIVU WA KIKE........ kila mtu ana uhru wa kujieleza kwa lugha anayoona ni rahisi......
mimi mwenyewe juzi nilienda kijijini kwetu ambako nimezaliwa na kukulia huko kuna wakati nilikuwa nachanganya sana liswahili badala ya kilugha sikufanya hivyo kwa makusudi ila niu MAZOEA tu, kama HAPINESS anapokea maelekezo na malezi na mambo yote ya fani hiyo kwa YAI what do you expect????
 
Kuulizwa kiswahili na kampuni ya utangazaji ya Tanzania ni alama ya utaifa.

Kushindwa kujibu Kiswahili ni alama ya kutokuwa makini katika mambo ya mahusiano ya jamii, kitu ambacho warembo hawa -ukiachilia mbali urembo na ulimbwende- hupimwa kwacho.

Katika neema za mahusiano jamii ameshindwa kujinyesha kama gwiji hapo.
 
Watu kama Happyness Magesse ni watu wa kuonewa Huruma. Kizungu chenyewe hakijui. Kwa mfano akiwekwa Abonge laivu na watu kama Wakina Shayo na Mashaka, hicho kiinglishi chake si atajiaibisha? Ndo kawaida zetu wabongo. Mtu akitoka tu nje ya Tanzania hata kwa wiki kiswahili anakuwa amekisahau. Hata na mimi kiswahili nilikisahau nilipoenda kwa mzee Madiba

Lugha yoyote ile mtumiaji wake hujitahidi aonekane anaijua barabara. Lakini nafikiri kabla ya mahojiano huwa kuna maandalizi na makubaliano ni lugha gani itumike kwa faida ya wasilikizaji ama watazamaji. Na si kweli kuwa kukaa nje ya nchi muda mrefu ndiyo unasahau lugha yako. Hapana. Nimekaa nje zaidi ya miaka 10 na inapita siku nyingi tu bila kuongea kiswahili. Na mara nyingi pale tu nikipiga simu Tanzania. Lakini bado ninaongea kiswahili safi tu? Hizo zote ni mbwebwe na minjonjo ili mtu aonekane yuko katika anga na mang'amuzi ya juu.

Lugha ni chombo cha mawasiliano na si kweli kuwa ndiyo kipimo cha mang'amuzi ya mtu!
 
jamani watz tujifunze kutoka nchi za asia kwani wameendelea kutokana na lugha yao. Wafanyakazi wa huko kwao ni lugha zao kama kijapani,kichina tu na kingereza ni kiduchu sasa huku sisi tabu yetu hipo hapo mtu anaona akiongea ngeri ndokapanda vidato kumbe hakuna kitu. Hata viongozi wetu wakiojiwa BBC/VOA naonaga wanaulizwa kiswahili wanajibu ngeri kweli? Tubadilike watz.
 
Don't you think they have a point though? Utaulizwaje Kiswahili kisha ujibu kwa Kiingereza? Kama huyo anaye kuuliza analenga jamii inayo zungumza Kiswahili je?

May be she's more confortable with her kiingereza...
 
Hii kudu... kudu mbona kali, hii imekaa kichekesho kweli kweli! Raha ya JF ndio hii watu tucheke.
 
Aaaah! wewe ndiyo ushangawe! mbona hata humu JF tabia hiyo ipo tele?
In short ni kwamba, kuna watu wanadhani wakiongea kiingereza hadhi yao inaongezeka.


sio kudhani, bali ndio hali halisi. Ukitaka hata dem we ongea kingreza tu. ukitaka kumaliza ubishi we ongea kingreza tu. ukitaka kujenga jina we ongea kingreza tu. kiswahili ruksa kuvunja ila kingreza mwiko. utawasikia hata wakubwa, sijui kiswahili chake vizuri ila ni ku maintain...
 
Kisha baadae unasikia...'of kosi yesi!'...mmmh!!!..Kiswahili au Kiingereza?
Lugha za wenyewe zinakazi kweli.

huyo huyo wakati anakabidhi taji kw miss mwingine alipata fursa ya kuwauliza wanyange maswali pale jukwaani kwa mtindo wa kuchagua swali. unataka kuulizwa kingereza au kiswahili.... then utasikia, "I repeat again...!!
 
Naona anachemka, kama mwana JF alivodai kuwa kuna watu wanadhani kuongea kingereza ndo ujanja au usomi, basi hawa dada zetu haswa 'masister du' km tulivozoea kuwaita wanajitahidi sana kuongea km wamarekani, hii si sahihi, yes si mbaya kujua kuongea lugha ingine, lakini km we ni mahiri huwezi kuulizwa kwa kihaya ukajibu kichaga!! labda uombe huwezi kuongea 'fluent' upewe mkalimani. inaeleweka kabisa. watu wa hivyo wakienda kwa bibi zao kijijini utasikia 'ooh yaa,aah u know, wajua sijazoea sometimes,aah wakati mwingine nakuwa very busy, i mean kazi nyingi kabisa!! nininiiiii? ulimbukeni basi tuite ni ashule 9 kutoeleimika hukoo). waache tabia hiyo, tuwe sahihi na matumizi ya lugha kwa wakati wake. katika JF its okay kuwasiliana vyovyote!! sio ktk deep profile ya jamii!!
 
Huyu si tunaema tumemchagua aka-promote image ya Tanzania? Nadhani inabidi asipewe contract yoyote, ka sababu hajiamini, hajipendi na hajielewi
 
Lakini mi naamini na yule aliyekuwa anamhoji alipaswa kuwa amezungumza na yule binti mapema na kuyaweka masuala haya wazi: yaani je, ni lugha gani itumike. Sidhani jamaa alifikia kumvamia tu kwa maswali. Naamini walishaonana mapema na kuongea kabla ya mahojiano na kujiandaa kwa kuanza kuhojiana. Yule mwandishi alipaswa kumsaidia yule mdada badala ya kuleta kile kichechesho cha ajabu. Au jamaa kuona mwenzake "anatema Ung'eng'e" naye angebadili lugha walau kuleta uwiano, na baadaye watafsiri. Ingekuwa nafuu.
 
Nilikuwa nafuatilia matangazo ya TBC1 Jumamosi jioni tarehe 20 Mwezi huu, nikaona mahojiano kati ya mtangazaji wa TBC1 na miss Tanzania wa zamani na mwanamitindo Happyness Magesse yaliyofanyika huko Afrika ya kusini.
Jambo moja lilinishangaza, kila mtangazaji alipokuwa akimuuliza kitu (kwatumia lugha yetu ya taifa), basi Happyness alikuwa anajibu kwa
ung'eng'e wa hali ya juu! ikawa kama kituko hivi, ........

Mfano;
Swali..."Hebbu tuambie, nimafanikio gani umepata toka ulipojiunga na fani hii......"?
Happyness..." You know, if your talented and you want to succeed, yuo "kudu, kudu, kudu be zis o zat.........."
Ilikuwa hivyo kipindi kizima!!

Sasa hapa nauliza jamani, dada yetu huyu kiswahili hajui? au amekisahau baada ya kukaa sana 'Sauzzi'! Au toka alipokuwa huku alikuwa hakijui amezaliwa nje ya bongo!?
Ninini hiki??

Simlaumu, ni haki yake kujieleza kwa kutumia lugha ambayo atakuwa huru kujieleza kwa kuwa lugha zinazotambulika kutumika kwenye shughuli rasmi nchini kwetu si ni Kiswahili na Kiingereza.

Angetumia Kichina, Kisukuma, Kinyamwezi, Kichaga au Kijerumani tungekuwa na haki ya kumlaumu.
 
...jamani jaribu kuelewa kidogo,watu wengine humu tunaishi states zaidi ya miaka 10 na kuanzia nyumbani familia,kazini,supermarkets,barabarani,viwanja etc na shule zote tulizopitia ,radio,Tv na watu wote ni English tuu,sometimes unaweza usione au kuongea na mtu wa kiswahili for a month sasa unategemea nini lugha nitakayo zungumza,imefika point siwezi tena kuongea kiswahili 100% lazima nichanganye tuu bila kujua...sio arrogance nafikiri ni kuzoea na rahisi zaidi kujieleza kwa lugha unayotumia kila siku,kama ilivyo home mtu akiongea tuu unaweza kujua kama ni msukuma,mzaramo,mlugulu etc hata huku baada ya muda mtu akiongea tuu utajua katoka wapi New York,west,southern,Britain,liberia,Nigeria,midwest etc ni lugha tuu wakuu hakuna la ajabu hapo au majivuno,ila ni vizuri sana kutochanganya lugha ingawaje ni ngumu sana
 
Aaaah! wewe ndiyo ushangawe! mbona hata humu JF tabia hiyo ipo tele?
In short ni kwamba, kuna watu wanadhani wakiongea kiingereza hadhi yao inaongezeka.

mhh mkuu sidhani kwamba kuchanganya english na swahili ni big deal!!! system ya elimu yetu ndio yakulaumu primary kiswahili, secondary school english, univerities english, business- swahili, maofisini etc
 
Jamani msimseme sana bibie mtajuaje kwamba na yeye anajua, Lakini hebu turudi kwenye hizi filamu za bongo...wanavyochanga lugha hadi wanachekesha..ndio sehemu ya mbinu za uigizaji? maneno yanavyotamkwa kama vile amelazimika kuyakariri.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom