Happy Women's day wadada wetu wa hapa JF

what you are writing is correct and you just confusing your self sir,dont waste our time & energy to explain things which are open. this is not debate.

C'mon Ivuga, why are you calling it a waste of time and energy? which things are open and to who?
 
eeeh Mayassa wangu weeeee..hepi wimensi dei mke wangu Mayassa.....usijali safari siyo kifo Mayassa wangu nitarudi tu wala mabinti wa Kigali wasikupe hofu...
 
hakika katika kuazimisha siku ya mwanamke duniani ni dini moja tu ambayo hawathamini wanawake kwa vitendo na maneno, mimi nimo ndani ya dini hiyo, ila kwa mambo haya , nakeleka sana

427669_360385467335731_187358797971733_1119978_805466107_n.jpg
 
Nimependa hizi fikira mbadala. Kwa nini unaamini hivyo? Ningependa kujusikia mawazo yako.

Aksante SI, ubarikiwe. Though ningependa kusikia zaidi mawazo ya Dada Gaijin.

Tunapowapangia watu siku ya kumheshimu, kumthamini na kutambua mchango wa mwanamke, maana yake ni kuwa tunatoa ruhusa kwa hao watu kutofanya hayo katika siku nyengine. Hivi wewe mwanamke unakubali kupangiwa siku ya kujaliwa? Hilo ni moja.

Jengine ni kuwa kila tunapotaka nafasi za kipekee za mwanamke kwenye jamii, tunatoa picha kuwa mwanamke hawezi mpaka mwanamme amuwezeshe na ampangie mambo yake.

Huwezi kutaka usawa baina ya mwanamke na mwanamme lakini wewe mwanamke ukataka kila kitu upewe upendeleo maalum ama uwezeshwe na huyo huyo mwanamme.
 
Asante sana Gaijin kwa ufafanuzi. Ningependa kutumia jibu lako kwa kufafanua mtazamo wangu pia :
Tunapowapangia watu siku ya kumheshimu, kumthamini na kutambua mchango wa mwanamke, maana yake ni kuwa tunatoa ruhusa kwa hao watu kutofanya hayo katika siku nyengine. Hivi wewe mwanamke unakubali kupangiwa siku ya kujaliwa? Hilo ni moja.
Hivi tunapo sheherekea sikukuu ya Uhuru wa nchi, ina maana siku zingine hatuko huru? Au tunapo shererekea siku ya Ukimwi duniani (1st of December) ina maana siku zingine ruhsa kujiripua?
Kwa mtazamo wangu siku ya wanawake ni siku ya 'makumbusho' kuhusu inequalities, na ni fursa ya kukusanyika tena, kutoa azimio kuhusiana na mada ya mwaka huo na kuchanga mawazo.

Jengine ni kuwa kila tunapotaka nafasi za kipekee za mwanamke kwenye jamii, tunatoa picha kuwa mwanamke hawezi mpaka mwanamme amuwezeshe na ampangie mambo yake.
Nadhani mapambano ya wanawake sio ya kutafuta nafasi za kipekee, bali ni kutafuta usawa kati ya wanawake na wanaume. Sio siri kwamba wanawake wana nyanyaswa kuliko wanaume, hasa vijijini. Kiwango cha kazi wanacho fanya wanawake ni kikubwa ila hakithaminiki kama kazi ya jamii. Ikiwa mwanaume anafanya kazi hizo hizo naonekana kua shujaa na anatambuliwa kwa njia tofauti. Wanwake wanataka nafasi yao na mchango wao katika jamii utambuliwe.
kuna changamoto wanazo zipata wanawake ambazo zinahitaji mtazamo wa kipekee. Vitu kama maternity leave, gender based violence, equal pay, reproduction health, office space and career advancement vimekaa kumpendelea mwanaume zaidi kwa sasa, na kuna maana ya kurekebisha. Bila kuzichukulia changamoto hizo kama za wanawake kwa upekee itakua vigumu kufikia usawa.

Huwezi kutaka usawa baina ya mwanamke na mwanamme lakini wewe mwanamke ukataka kila kitu upewe upendeleo maalum ama uwezeshwe na huyo huyo mwanamme.
Wanaume ndio wanafanya uonevu huo udumu. Ukichunguza matatizo ya office space utagundua watu wengi katika management ni wanaume. Sasa utajadili na nani ukitaka kubadilisha mambo? Ukichunguza sheria za reproductive health utagundua wabunge wengi ni wanaume, sasa utapitishaje sheria ya kupendekeza 'choice'? Ukitazama sheria za kazi unaona kazi zina mpaka wa ma saa (maximum hours of work per week) ila unaambiwa hizo hazihusu kazi za nyumbani ambazo mara nyingi vijijini asilimia kubwa inafanya na wanawake. Sasa wanawake peke yao wanawezaje kubdili mambo bila kujadiliana na wanaume?
Sio kwamba wanaume wana njama au mpango mkubwa wa kuwanyanyasa wanawake, sidhani. Haya mambo yametokea kwa muda mrefu na yanaonekana kua kawaida. I think it is just time for another discourse, another approach on understanding and implementing the universal declaration on human rights.
 
Nadhani mapambano ya wanawake sio ya kutafuta nafasi za kipekee, bali ni kutafuta usawa kati ya wanawake na wanaume. Sio siri kwamba wanawake wana nyanyaswa kuliko wanaume, hasa vijijini. Kiwango cha kazi wanacho fanya wanawake ni kikubwa ila hakithaminiki kama kazi ya jamii. Ikiwa mwanaume anafanya kazi hizo hizo naonekana kua shujaa na anatambuliwa kwa njia tofauti. Wanawake wanataka nafasi yao na mchango wao katika jamii utambuliwe.

Kuna changamoto wanazo zipata wanawake ambazo zinahitaji mtazamo wa kipekee. Vitu kama maternity leave, gender based violence, equal pay, reproduction health, office space and career advancement vimekaa kumpendelea mwanaume zaidi kwa sasa, na kuna maana ya kurekebisha. Bila kuzichukulia changamoto hizo kama za wanawake kwa upekee itakua vigumu kufikia usawa.

Wanaume ndio wanafanya uonevu huo udumu. Ukichunguza matatizo ya office space utagundua watu wengi katika management ni wanaume. Sasa utajadili na nani ukitaka kubadilisha mambo? Ukichunguza sheria za reproductive health utagundua wabunge wengi ni wanaume, sasa utapitishaje sheria ya kupendekeza 'choice'? Ukitazama sheria za kazi unaona kazi zina mpaka wa ma saa (maximum hours of work per week) ila unaambiwa hizo hazihusu kazi za nyumbani ambazo mara nyingi vijijini asilimia kubwa inafanya na wanawake. Sasa wanawake peke yao wanawezaje kubdili mambo bila kujadiliana na wanaume?

Sio kwamba wanaume wana njama au mpango mkubwa wa kuwanyanyasa wanawake, sidhani. Haya mambo yametokea kwa muda mrefu na yanaonekana kua kawaida. I think it is just time for another discourse, another approach on understanding and implementing the universal declaration on human rights.
Mwali, yote uliyoyataja ni ya msingi sana kiasi kwamba nimeshindwa hata kuchagua lipi lina umuhimu zaidi, labda niongezee kidogo tu katika baadhi yao:
1. Usawa wa kazi: Sio vijijini tu bali hata mijini. Mke na mume wanatoka saa hiyo hiyo kwenda kazini, lakini mwanamke anaamka mwanzo kumtayarishia "bwana na watoto" chai. Wakati wa kutoka ofisini si hasha mwanamke kutoka mwisho kwa sababu "bosi" kalazimisha hili na lile lifanywe, lakini akifika nyumbani bado kazi zinamsubiri.

2. Kazi hiyo hiyo, mwanamke analipwa si chini ya 20% kasoro kuliko mwanamume. Nafasi nyingi za juu maofisini, idadi ya mawaziri serikalini, wabunge....wengi ni wanaume. Na ikitokea pahali mwanamke amekuwa raisi au mkuu wa shirika la kimataifa, hiyo inaanza kuwa hadithi na jambo la kupigiwa mfano. Cha ajabu, majumbani, mashuleni na vyuoni...duniani kote...wanawake ni wengi kuliko wanaume, wastani wa 60%, lakini mpaka leo hakuna bunge (nadhani) lililo na angalau 50-50% ya wanaume na wanawake.

3. Unyanayasaji wa kijinsia: Nitataja mfano wa nchi moja ninayoijua zaidi - Spain. Mwaka jana wanawake 70 waliuliwa na waume/ wapenzi wao na hakuna mwanamume hata mmoja aliyeuliwa na mwanamke. Sasa kuona takwimu kama hizi katika nchi "iliyoendelea", tuelewe katika nchi "zisizostaarabika" hali ni mbaya zaidi. Domestic Violence, ubakaji, biashara ya binadamu (kwa ngono), kufanyisha kazi watoto wadogo...ni matatizo ambayo mwanamke anakabiliana nayo popote alipo ulimwenguni.

4.Mwanmke kama chombo cha boashara: Angalia mfano matangazo ya biashara, mfano katika tangazo la gari jipya, tangazo la vyombo vya matumizi ya nyumbani...biashara haiendi kama hakuwekwa mwanamke nusu uchi. Hata kwenye masumbwi wanayopigana wanaume, wanawake nusu uchi ndio wanaonogesha shughuli.

6. Hilli la mwisho Mwali tunatafautiana kimawazo. Kwa mawazo yangu ni kuwa "wanaume kwa makusudi kabisa wanawanyanyasa wanawake". Hata kama ni kweli kuwa haya mambo yalianzia mbali na sasa yanaonekana ya kawaida, lakini ni nani aliyeyaanzisha?

Hata hivyo, pamoja na kuwa mwanamme yuko mstari wa mbele katika kuwanyanyasa, kuwawekea vikwazo na kuwarejesha nyuma wanawake, nahisi wanawake na wao wenyewe wanachangia kuyaendeleza haya. Juzi pahali fulani katika jukwaa hili niliuliza, "inakuwaje katika jimbo la uchaguzi ambako wanawake wapiga kura ni wengi kulliko wanaume, lakini akisimama mwanamke kugombea, wanawake wanawapigia debe wanaume na hata kuwapikia majungu wanawake wenzao?"

Bado changamoto ni nyingi. Ni miaka 101 tangu kuanza kuadhimishwa rasmi siku hii. Mafanikio yamepatikana lakini bado sana kwa mwanamke kujikomboa. Ni wakati sasa kwa wanawake kusimama imara. Wasisubiri tarehe 8 Machi kupakwa mafuta kwa nyuma chupa na wanaume bali mapambano yawe ya kila siku na kila mahali - majumbani, mashuleni, maofisini, kwenye vyombo vya kutunga sheria n.k. Kuna baadhi ya nchi siku hii wanaume hawaruhusiwi kupenyeza pua zao katika maadhimisho. Vita ya kumkomboa mwanamke ianze na mwanamke mwenyewe.

UWEZO, NIA NA SABABU MNAZO.
 
MamaMia

1. Usawa wa kazi: Sio vijijini tu bali hata mijini. Mke na mume wanatoka saa hiyo hiyo kwenda kazini, lakini mwanamke anaamka mwanzo kumtayarishia "bwana na watoto" chai. Wakati wa kutoka ofisini si hasha mwanamke kutoka mwisho kwa sababu "bosi" kalazimisha hili na lile lifanywe, lakini akifika nyumbani bado kazi zinamsubiri.

Mwanamke ambae umekomboka, una kazi yako ofisini, unaenda sawa kwa sawa na mumeo, unataka Siku ya Mwanamke Duniani ikusaidie kutatua tatizo lako na mumeo nyumbani? Kwa mfano tunataka siku hiyo ikusaidieje? Na mwanamme/mumeo kuambiwa katika siku moja hii, kutamsaidiaje?

2. Kazi hiyo hiyo, mwanamke analipwa si chini ya 20% kasoro kuliko mwanamume. Nafasi nyingi za juu maofisini, idadi ya mawaziri serikalini, wabunge....wengi ni wanaume. Na ikitokea pahali mwanamke amekuwa raisi au mkuu wa shirika la kimataifa, hiyo inaanza kuwa hadithi na jambo la kupigiwa mfano.

Wanawake wanataka liwe jambo la kupigiwa mfano. Wakati mie ninaona ni kumdhalilisha mwanamke kwa kusema ni "ajabu" kuweza kufika hapo alipo, wanawake wenyewe wanasema wapewe recognition-tena na mwanamme. Ukikataa kuwa wanawake wasipigiwe mfano basi lazima uvikatae viti maalum pamoja na Siku maalum ya wanawake, kwa sababu mantiki ni moja
Cha ajabu, majumbani, mashuleni na vyuoni...duniani kote...wanawake ni wengi kuliko wanaume, wastani wa 60%, lakini mpaka leo hakuna bunge (nadhani) lililo na angalau 50-50% ya wanaume na wanawake.

Ikiwa mashuleni na vyuoni wanawake ni wengi kuliko wanaume, kinachowashinda kuingia bungeni ni nini? Umewahi kufikiria kuwa labda wanawake wengi hawapendi siasa ndio maana si wabunge? Umejiuliza kwa nini wanawake wengine wanaweza kuwa wabunge lakini wengine hawawezi?

3. Unyanayasaji wa kijinsia: Nitataja mfano wa nchi moja ninayoijua zaidi - Spain. Mwaka jana wanawake 70 waliuliwa na waume/ wapenzi wao na hakuna mwanamume hata mmoja aliyeuliwa na mwanamke. Sasa kuona takwimu kama hizi katika nchi "iliyoendelea", tuelewe katika nchi "zisizostaarabika" hali ni mbaya zaidi. Domestic Violence, ubakaji, biashara ya binadamu (kwa ngono), kufanyisha kazi watoto wadogo...ni matatizo ambayo mwanamke anakabiliana nayo popote alipo ulimwenguni.

Kenya hapo wanawake wanawanyanyasa wanaume na kuwapiga na hata kuwavunja…Jee inamaanisha kuwa Kenya au wanawake hao wamejikomboa zaidi? Na ustaarabu wao uko katika kipimo gani?
4.Mwanmke kama chombo cha boashara: Angalia mfano matangazo ya biashara, mfano katika tangazo la gari jipya, tangazo la vyombo vya matumizi ya nyumbani...biashara haiendi kama hakuwekwa mwanamke nusu uchi. Hata kwenye masumbwi wanayopigana wanaume, wanawake nusu uchi ndio wanaonogesha shughuli.

Na kule mitaani wanawake wanaovaa nusu uchi na kuonyesha maungo ya mwili, wanaonewa na mwanamme pia? Na siku moja ya wanawake itaondoaje hili tatizo?

6. Hilli la mwisho Mwali tunatafautiana kimawazo. Kwa mawazo yangu ni kuwa "wanaume kwa makusudi kabisa wanawanyanyasa wanawake". Hata kama ni kweli kuwa haya mambo yalianzia mbali na sasa yanaonekana ya kawaida, lakini ni nani aliyeyaanzisha?

Ikiwa mwanamme anafanya kwa makusudi, sielewi kwa nini wanwake wamtegemee huyo huyo mwanamme kuwapangia mambo yao, kuwapa recognition, kuwaambia "mkiwezeshwa mnaweza." Vyote ni mfumo dume tu

Juzi pahali fulani katika jukwaa hili niliuliza, "inakuwaje katika jimbo la uchaguzi ambako wanawake wapiga kura ni wengi kulliko wanaume, lakini akisimama mwanamke kugombea, wanawake wanawapigia debe wanaume na hata kuwapikia majungu wanawake wenzao?"

Kwanza hatuwezi kutegemea mwanamke ashinde kila jimbo atakalosimama kwa sababu idadi ya wanawake jimboni humo ni kubwa. Huo utakuwa ni ukosefu wa mantiki kwa wanawake wapiga kura. Huwezi kumpigia mtu kura kwa kuangalia jinsia yake tu na hatuwezi kuwategemea waache kumchagua mwanamme bora kwa sababu mpiznani wake ni mwanamke japo kanjanja.

Hapo pa kuwapikia majungu, tunaomba twende na facts, imetokea wapi? Hii itasaidia kutuondoa kuongelea kinadharia tu
 
MamaMia [MAMMAMIA] Mwanamke ambae umekomboka, una kazi yako ofisini, unaenda sawa kwa sawa na mumeo, unataka Siku ya Mwanamke Duniani ikusaidie kutatua tatizo lako na mumeo nyumbani? Kwa mfano tunataka siku hiyo ikusaidieje? Na mwanamme/mumeo kuambiwa katika siku moja hii, kutamsaidiaje?

Nahisi yote unayozungumza ndio yaleyale ninayozungumza ijapokuwa kwa mitizamo tafauti. Nimesema mwisho wa maelezo yangu, kuwa ukombozi wa mwanamke hauji kwa kuadhimisha siku moja kati ya siku 365, bali ni "vita ya kila siku". Siku ya maadhimisho iwe ni kuangalia "wamefanikiwa lipi na bado lipi wanapaswa kulipigania"

Wanawake wanataka liwe jambo la kupigiwa mfano. Wakati mie ninaona ni kumdhalilisha mwanamke kwa kusema ni "ajabu" kuweza kufika hapo alipo, 1.wanawake wenyewe wanasema wapewe recognition-tena na mwanamme. 2. Ukikataa kuwa wanawake wasipigiwe mfano basi lazima uvikatae viti maalum pamoja na Siku maalum ya wanawake, kwa sababu mantiki ni moja
1. Sasa ikiwa "wanawake wenyewe wanasema wapewe recognition- tena na wanaume", hatuoni kuwa hapa na wanawake wenyewe wanachangia kujidhalilisha? 2. Hili hata mimi ninalipinga na linakuzwa na huu mfume dume ambao ninaupinga pia.

Ikiwa mashuleni na vyuoni wanawake ni wengi kuliko wanaume, kinachowashinda kuingia bungeni ni nini? Umewahi kufikiria kuwa labda wanawake wengi hawapendi siasa ndio maana si wabunge? Umejiuliza kwa nini wanawake wengine wanaweza kuwa wabunge lakini wengine hawawezi?

Kuweza na kutoweza ni uwezo wa mtu, na kutaka na kutoka kuwa mbunge ni hiari ya mtu, awe mwanamke awe mwanamume, isipokuwa imani yangu ni kuwa tusitarajie kuwa bungeni mabako ndiko sheria zinazotungwa, wanaume watatunga sheria na kuzitekeleza kwa dhati kuwatetea wanawake - kwa huo huo mfumo dume ulioutaja.

Kenya hapo wanawake wanawanyanyasa wanaume na kuwapiga na hata kuwavunja…Jee inamaanisha kuwa Kenya au wanawake hao wamejikomboa zaidi? Na ustaarabu wao uko katika kipimo gani?

Inapotokea mwanamke kumpiga mwanamume, au kinyume chake, sidhani kama huo tunaweza kuuita ustaarabu, bali pale inapofikia wakati mwanamke anasema "mpaka hapa basi, inatosha".

Na kule mitaani wanawake wanaovaa nusu uchi na kuonyesha maungo ya mwili, wanaonewa na mwanamme pia? Na siku moja ya wanawake itaondoaje hili tatizo?

Hii nilikwishaisemea kbala na hapo juu, kuwa mengine tusiwalaumu wanaume kuwa ni wadhalilishaji bali wanawake wenyewe wanachangi, iwe kijijini, mjini au hata nyumbani.

Ikiwa mwanamme anafanya kwa makusudi, sielewi kwa nini wanwake wamtegemee huyo huyo mwanamme kuwapangia mambo yao, kuwapa recognition, kuwaambia "mkiwezeshwa mnaweza." Vyote ni mfumo dume tu
.
Ili hayo yasitokee, ndio maana ninasema tena na tena, kuwa mwanamke hapaswi kusubiri favour ya mwanamume. Kuhusu hii kauli mbiu ya "mkiwezeshwa mnaweza", ninaipinga kabisa, kwani naamini wanawake wanaweza bila ya kuwezeshwa.

Kwanza hatuwezi kutegemea mwanamke ashinde kila jimbo atakalosimama kwa sababu idadi ya wanawake jimboni humo ni kubwa. Huo utakuwa ni ukosefu wa mantiki kwa wanawake wapiga kura. Huwezi kumpigia mtu kura kwa kuangalia jinsia yake tu na hatuwezi kuwategemea waache kumchagua mwanamme bora kwa sababu mpiznani wake ni mwanamke japo kanjanja
.

Hapa ninakubaliana na wewe kabisa kuwa "tuchague watu kwa uwezo wao" bila ya kupeana "fursa wala upendeleo maalumu", wala kwa sababu ya kuwa ni mwanamke au mwanamume.

Hapo pa kuwapikia majungu, tunaomba twende na facts, imetokea wapi? Hii itasaidia kutuondoa kuongelea kinadharia tu

Haya ni mawazo yangu tu kwa yale ninayoyaona yakitendeka, facts in figures sina.

Bado naamini kuwa, tunapotaja ukombozi wa mwanamke, ni kuwa kuna kitu hakiko sawa katika jamii zetu, kuna mambo yanapaswa kurekebishwa, sio kwa lengo la kuwa mwanamke amtawale mwanamme bali kutetea haki na fursa sawa. Siku ya maadhimisho haya, si alama kuwa ukombozi ndio umepatikana, bali kukumbushana kuwa kuna mambo hayako sawa. Mwali aliwahi kuuliza, je kuadhimisha siku za "UKIMWI, Diabetis, Cancer na mengineyo", ina maana siku nyengine watu huwa hawateseki na magonjwa hayo. Lengo ni kutoa mwamko juu ya tatizo, na bado kuna tatizo juu ya haki za mwanamke.
 
Back
Top Bottom