SMU...umenigusa sana hapo, kila cku najutiaga kiac nilivyomsumbua mama, nilimsumbua vya kutosha jamani, alinicmamia kidete bila yeye cjui nyamayao angekuwa mtu wa namna gani, asante sana mama kwa kunipigania, huwa nikikumbuka nackitika sana sana.
Mother love is the fuel that enables a normal human being to do the impossible. ~Marion C. Garretty, quoted in A Little Spoonful of Chicken Soup for the Mother's Soul
THERE IS APOWER IN MOTHERS TO PROTECT LIFE!!
Nakumbuka siku moja nikiwa Morogoro (nimechoka na mwili unahoma) nasubiri basi,nikitokea Dodoma nikielekea Mbeya, nilimwona mama mmoja pale stendi ya Msamvu yuko na rambo yake ameshindilia nguo na vingine humo pamoja na mtoto wake mkononi akiwa analia. yule mama alikuwa akihangaika sana kumnyamazisha. Punde nikamwona anakwenda okota ndizi iliyotupwa na abiria aliyekuwa ndani ya basi linaloondoka la Abood. aliirudi upesi kwenye rambo yake akatoa kijiko na kuanza kuiparua ile ndizi kwa nje kisha akampa mwanae. yule mtoto (umri wake ni chini ya mwaka) aliifukamia kwa nguvu sana. Jambo lile lilinishitua mno, Nikakumbuka, nalikuwa mtoto kwa mama. nikajiuliza hivi mama yangu nikiwa na umri kama huo alipitia maisha yanayofanana na hayo? ghafla, machozi yalianza kunitoka. Kwakuwa nilikuwa nimekaa chini tena nimejikunyata, nilipokuwa nafuta machozi hakuna aliyejua. nikiisha jifuta hayo machozi nilikwenda kwa huyo mama kumuliza kulikoni. akanijulisha kuwa kafukuzwa na mumewe walikuwa wanaishi "Kihonda" siku ya nne sasa analala nje ya nyumba. Sasa ameonelea bora arudi nyumbani Iringa lakini hana pesa yoyote. Tuliingia kwenye vihoteli vya pale pembeni nikamnunulia chakula chake na mwanae. Yule mama hakutaka vyakula vije sambamba, aliomba kije cha mwanae kwanza akamlisha. Kilipokuja chake mtoto akadandia kidogo tu kisha akakataa. Ndipo mama akala. Muda si mrefu mtoto akalala.
Who fed me from her gentle breast
And hushed me in her arms to rest,
And on my cheek sweet kisses prest?
My Mother.
Who ran to help me when I fell,
And would some pretty story tell,
Or kiss the place to make it well?
My mother.
~Ann Taylor
I am proud to be a mother! Glory to God.
Happy Mother's day to you all my JF friends! God bless you abundantly!
Asha D.
Unastshili pongezi kwa kufungua hii thread tamu!
Natamani kusema mengi sana juu ya kinamama,
Ila ni ukweli usiopingika, maneno hayatoshelezi!
Pia Mama ana nafasi ya peke katika Moyo wangu.
Hakuna kama mama. Tunashukuru sana kwamba mungu anazidi kutulinda, kikubwa ni kutupa hekima ya kuongoza familia zetu katika misingi ya upendo, uvumilivu, kusameheana kwa kila jambo. Hakuna mtu aliyekamilika kila mtu ana mapungufu yake.
Baba, kaka, waume zetu, zidini kutupenda, kutuongoza kwa kujua kwamba mko kwenye mikono salama iliyobarikiwa. Kuweni na huruma na sisi mama/dada/wake zenu. Shukuruni kwa kila jambo tukiomba hekima kutoka kwa mwenyezi mungu.
Nawatakia kila la kheri, nikiamini kwamba hakuna lisilowezekana kwake.
Happy Mothers day mama wote na asanteni sana kwa malezi yenu kwa watoto wetu na upendo wenu.
Kwa single mums yeyote yule, endelea uvumilivu na mungu awape nguvu za kumudu majukumu yote mlioachiwa.
Nawapenda wote.