Happiness Katabazi: Waandishi wenzangu tuache kuongea sana bila kutenda na kujifunza

Uhalisia Jr

Senior Member
Sep 10, 2012
134
46
...nawakumbusha waandishi wenzangu tuache kuongea sana bila kutenda na kujifunza. Tuongee na kuandika kwa kuwa na vielelezo ambavyo mwisho wa siku vitaisaidia mahakama kuwatia hatiani watuhumiwa wa makosa mbalimbali.


  • Leo hii tunasema kabisa ni polisi ndiyo walioua lakini tunashindwa kutaja jina la polisi aliyeua. Ni sisi waandishi waandishi wa habari enzi zile za tukio la mauji ya wafanyabiashara wanne wa wilayani Mahenge mkoani Morogoro tulishupalia na kushikia bango kuwa ni polisi na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe ndiyo waliowaua wafanyabiashara hao bila ya kuwa na ushahidi na mwisho wa siku Mahakama Kuu chini ya Jaji wa Mahakama ya Rufani hivi sasa Salum Massati aliwaachiria huru kwa maelezo kuwa Jamhuri imeshindwa kuthibitisha kesi hiyo na akalitaka jeshi la polisi likawatafute wauaji na kwamba Zombe na wale washitakiwa wenzie siyo wauaji wa wafanyabiashara wale. Baada ya kuachiriwa huru Zombe aliyashitaki baadhi ya magazeti likiwomo gazeti la Uhuru, Tanzania Daima, Dar Leo kwa madai kuwa lilimhukumu kabla hajahukumiwa na kesi zipo mahakamani isipokuwa gazeti la Uhuru lilikwenda kumwomba msamaha Zombe na hatimaye Zombe akaiondoa kesi hiyo mahakamani wakaenda kumalizana nje ya mahakama.


  • Pia ningali nikikumbuka tukio la uvamizi katika ofisi za gazeti la Mwanahalisi ambapo watu wasiyojulikana walimjeruhi Mwandishi Saed Kubenea na Ndimara Tigambwage na sisi waandishi wa habari na jamii kwa ujumla tulifanya maandamano na kupiga kelele kutaka wahusika wakamatwe wafikishwe mahakamani na kweli polisi iliwafikisha mahakamani watuhumiwa hao pale Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Oktoba 2011, mahakama hiyo iliwaachilia huru kwa madai kuwa Jamhuri imeshindwa kuleta ushahidi wa kuthibitishia mahakama kuwa ni kweli washitakiwa hao ndiyo waliwajeruhi Kubenea na Ndimara.


  • Tukio jingine ni kuhusu mkataba wa kampuni ya kufua umeme ya Richmond. Tuliandika na kufikia hatua ya kujipa mamlaka ya kusema mkataba huo uliingiwa kwa misingi ya rushwa na kuandika makala za kumdhihaki Mkurugenzi Mkuu wa (TAKUKURU), Dkt. Edward Hosea ambaye alisema hakukuwa na tuhuma za rushwa katika mkataba huo na mwisho wa siku DPP-Dkt. Feleshi alimfikisha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mfanyabiashara Naeem Gire aliyekuwa akitetewa na wakili wa kujitegemea Alex Mgongolwa kwa makosa ya kutoa taarifa za uongo kuhusu kampuni hiyo ya Richmond, lakini mwaka jana Hakimu Mkazi Waliarwande Lema, alimwachiria huru baada ya kumuona hana kesi ya kujibu.


  • Tukio jingine ambalo sisi wanahabari, wanasiasa na waharakati ni lakupinga hukumu ya mahakama ya kimataifa ya ICC, iliyoipa kampuni ya Dowans-Tanzania, tuzo ya Dola za Kimarekani milioni 56, ambapo tulisema ni rushwa na haiwezekani la mwisho wa siku Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilikubali tuzo hiyo isajiliwe hapa nchini na wiki iliyopita mahakama hiyo tena ilitupilia mbali ombi la TANESCO lilokuwa linataka mahakama itoe amri ya kuzuia utekelezwaji wa hukumu ya mahakama kuu ya Tanzania iliyoruhusu tuzo hiyo ya Dowans isajiliwe.

Kwa mifano hai hiyo hapo juu, nataka kuwaasa sisi wanahabari tusiwe watu wenye kasumba ya kupayuka payuka bila kuwa na ushahidi kwani tukumbuke yale tunayoyaandika ndiyo umma wanayoyaamini na kuyafuata....


Source: wavuti - wavuti
 
Huyu mwana mama anaripotia taasisi gani,? Anaonekana kama mwandishi wa wale wale waficha maovu
 
Back
Top Bottom