Hapa ndipo wakaka wanapotamani kujiua

Wakaka tupeni kila kitu kwa volume,quantity and quality mnayoweza iwe pesa, gari, tununulieni nguo,viwanja incase kabla ya kutuoa rasmi (kuishi pamoja)
ila musifanye hili
Msitusomeshe/Lipia gharama za kozi ndefu (miaka miwili kuendelea form 5&6,Diploma,degree kwa kuongozwa na mapenzi ya LOVE (not yale ya Agape)ahadi za ntakuja kuwa mkeo.

Nimegundua wakaka wengi hutaman kufa pindi wanaposalitiwa na wadada waliowalipia gharama za masomo kuliko hata waliwasaidia mambo wengine hata kama yana gharama kubwa kuliko masomo.

My take:Ukimsomesha mdada anza kufanya mazoezi ya kuzuia BP kubwa manake kuna siku kitawaka tu.

I see umenikumbusha mbali sana.

Nilialikwa kwenye gradu moja chuo flani huko Moro nikamkuta kaka mmoja anamwaga uchozi kisa dada aliye kuwa ana mgharamia amemtosa siku hiyo ya kuhitimu masomo yake. Jamaa alikuja kajiandaa maua tena marose bado mabichi mazawadi yamejaa box akaambulia kibuti mbele ya watu.
 
Lakini mimi jamani kuna kitu najiuliza.
Hivi kaka unampenda mtoto wa form one, unamsomesha kwa malengo ya kuoa huoni kama huyu dada ni mdogo na akili yake inabadilika kadiri anavyokua na anavyozidi kukutana na watu wa aina mbalimbali?

Sio kweli kwamba moyo wa huyu binti utakuwa umefanya maamuzi thabiti kwamba wewe ni mume wake!! Hata kama wakati huo atajiona hivo, lakini naamini kuna kipindi atawaona watu wanaomvutia na anaowapenda yeye kwa nafsi yake mwenyewe. Na ufahamu wake uliokomaa kwa wakati huo.

Kwa upande mwingine binti wa hivi simlaumu hata kidogo. Bora hata wa chuo.....na hata wa chuo bora umuoe ujue unasomesha mke wako. Vinginevyo msaidie tu kama mwanadamu wa kawaida ikitokea akawa mke, unashukuru.
good point
 
Kaka Pole, sijui kuna nini ndani ya hii? Wengine huwasomesha wadada kuliko walivyosoma wao, Na kuishia Maumivuni.

tunakosa wanawake wenye hofu ya Mungu..anyway baadae wasaliti nao ukutana na machungu huko waendako..to every reaction there is ....
 
Tuliosomeshwa sijui tuchangie nini humu, ngoja nitarudi. ila nachojua kutoa msaada huwa hutakiwi kutegemea malipo ya kitu fulani, iwe ndoa urafiki au chochote
 
Tuliosomeshwa sijui tuchangie nini humu, ngoja nitarudi. ila nachojua kutoa msaada huwa hutakiwi kutegemea malipo ya kitu fulani, iwe ndoa urafiki au chochote
unajua gaga mwanzoni mnakuwa wapenzi (mke mtarajiwa)ndio anaamua kukulipia ada sasa tatizo linakuja pale unapobadili mawazo baada ya kugradueti.
Vipi aliyekusomesha mlikuwa wapenzi na status ya penzi lenu kwa sasa ikoje au na wewe unalaana ya wakaka?
 
Kama mkaka anakusomesha wewe, wakati si ndugu yake, na hana mtu mwingine anayemtegemea kumuoa isipokuwa wewe...ni makosa makubwa na uuaji kummwaga wakati unapograduate!
Unless kuwe na sababu iliyosababishwa na huyu mkaka mwenyewe, lakini siyo mdada aanze kusema "nimemwona anayenipenda zaidi"... aisee hapo nitamfanya kitumbaya hatasahau maishani!
 
kama sio wako huwezi kulazimisha mapenzi kamwe na dada zetu muwe na utu jamani...inauma sana coz huyo mwanaume unakuta anamalengo kumbe duh..Kabug
 
Wakaka tupeni kila kitu kwa volume,quantity and quality mnayoweza iwe pesa, gari, tununulieni nguo,viwanja incase kabla ya kutuoa rasmi (kuishi pamoja)
ila musifanye hili
Msitusomeshe/Lipia gharama za kozi ndefu (miaka miwili kuendelea form 5&6,Diploma,degree kwa kuongozwa na mapenzi ya LOVE (not yale ya Agape)ahadi za ntakuja kuwa mkeo.

Nimegundua wakaka wengi hutaman kufa pindi wanaposalitiwa na wadada waliowalipia gharama za masomo kuliko hata waliwasaidia mambo wengine hata kama yana gharama kubwa kuliko masomo.

My take:Ukimsomesha mdada anza kufanya mazoezi ya kuzuia BP kubwa manake kuna siku kitawaka tu.

Salute! Marytina: Msimamowangu ni huo sisomeshi kozi ndefu labda mkewangu wa ndoa naye awe amesha nizalia japo watoto wawili
 
najitolea kukusomea Pm zote. Mwanafunzi hutakiwi kuchoka kabla hujaanza shule. Sawa eeh.

Mmmmmh, Husninyo wewe,
Nasikia harufu ya kuibiwa msomeshaji hapa.
Halafu, mbona hawatokei?
Au mpaka kesho mchana nini?
 
Back
Top Bottom