Hapa ndipo wakaka wanapotamani kujiua

Marytina

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
9,290
7,143
Wakaka tupeni kila kitu kwa volume,quantity and quality mnayoweza iwe pesa, gari, tununulieni nguo,viwanja incase kabla ya kutuoa rasmi (kuishi pamoja)
ila musifanye hili
Msitusomeshe/Lipia gharama za kozi ndefu (miaka miwili kuendelea form 5&6,Diploma,degree kwa kuongozwa na mapenzi ya LOVE (not yale ya Agape)ahadi za ntakuja kuwa mkeo.

Nimegundua wakaka wengi hutaman kufa pindi wanaposalitiwa na wadada waliowalipia gharama za masomo kuliko hata waliwasaidia mambo wengine hata kama yana gharama kubwa kuliko masomo.

My take:Ukimsomesha mdada anza kufanya mazoezi ya kuzuia BP kubwa manake kuna siku kitawaka tu.
 
Sidhani kama ni kweli kwamba ndicho kinachoumiza sana!Tatizo linakuwepo pale mwanamk anapokua amempa mwanaume matarajio ili aweze kumtumia.Ila kama kila mmoja alikua genuine toka mwanzo kuhusu hisia zao na baada ya msaada mambo yakabadilika hamna haja ya kujuta.Huwezi kushawishi watu wasiwaendeleze wanaoamini wanaweza kua watarajiwa wao kwa maumivu yasiyotabirika..mwisho wa siku wakijaoana atakua amejipunja mwenyewe maana alitaka mke aliyesoma ila hakutaka kufanikisha kisa fikra za tukiachana!
 
Hasa hasa ulogwe umpeleke,nje ya nchi ndio kabisaaaaaa,unawapelekea wazee wa huko. Kwa kifupi ukifanya hivyo ewe mwanamme mwenzangu andika...umeumia.
 
vipi mamito....tayari mpatia mtu BP na sheli ukaona inavyokuwa eeh!!
Wakaka tupeni kila kitu kwa volume,quantity and quality mnayoweza iwe pesa, gari, tununulieni nguo,viwanja incase kabla ya kutuoa rasmi (kuishi pamoja)
ila musifanye hili
Msitusomeshe/Lipia gharama za kozi ndefu (miaka miwili kuendelea form 5&6,Diploma,degree kwa kuongozwa na mapenzi ya LOVE (not yale ya Agape)ahadi za ntakuja kuwa mkeo.

Nimegundua wakaka wengi hutaman kufa pindi wanaposalitiwa na wadada waliowalipia gharama za masomo kuliko hata waliwasaidia mambo wengine hata kama yana gharama kubwa kuliko masomo.

My take:Ukimsomesha mdada anza kufanya mazoezi ya kuzuia BP kubwa manake kuna siku kitawaka tu.
 
Mara nyingi mapenzi ya uongo huanza kwa kijisababu fulani. Kwa mfano, mdada anaweza kuwa choka mbaya ktk familia yao. Anapoona kuwa kuna mkaka anaweza kumsaidia, huwa yuko tayari kufanya lolote ikiwa ni pamoja kukubali mahusiano ya kimapenzi na hatimaye kutoa ahadi hewa ya kuja kuoana. Believe me, kama mapenzi yanatokana na kusaidiana tatizo fulani ambalo linahusiana na fedha, uwezekano wa mapenzi ya dhati ni mdogo sana.
Ushauri wangu kwa wakaka ni kufanya kama ninavyofanya mimi. Nianapohisi mdada ana tatizo na anadhani kuwa anaweza kupata msaada wangu, huwa siweki conditions. Nitamsaidia pasipo kumruhusu yeye kujirahisisha kwangu eti kwa lengo la kujiwekea mazingira ya kumsaidia zaidi. Kwa hiyo jamani, tukubali, kwenye mazingira kama hayo, hakuna mapenzi ya dhati!!!
 
Mh makubwa tena haya, kwa hiyo mtu akitaka kumsomesha GF asifanye kisa ataachwa? kwani mtu akitoa msaada anategemea malipo?
 
Kumlipia mtu masomo ni kama umefanya investment kubwa sana na mkaka hategemei -ve return ndio maana wanaumia sana.
Tunakabidhiwa funguo ya gari kadi anabaki nayo mwenyewe. Vikichacha unanyang'anywa gari fasta. Ila akikukosomesha hana ujanja. Aaah! Wakaka tusomesheni bwana, hatutaki magari. Hela za mafuta zenyewe hamtupi.
 
Nitamsomesha msichana kwa misingi ya undugu au familia yake imeshindwa kumsadia hivyo nampa msaada kama mwanadamu mwingine. Kaka yangu alimsomesha msichana kutoka sekondari (O-Level) mpaka akapata kazi, baada ya kuanza kazi akampata jamaa na kubeba mimba mara moja kaka yangu akabaki analia kama mtoto mdogo nusura ajiuwe na maisha yake yakaharibika mpaka leo. Kaka alimgaramia huyo binti kwa zaidi ya miaka 8. Kutoka na jambo hilo nilishajiwekea msimamo wangu " kamwe siwezi kumgaramia masomo mwanamke kwa kigezo cha kumuoa" nitamsomesha mwanamke ambaye ni mke wangu. Na watoto wangu nitawaeleza hilo jambo tokea wakiwa na umri wa miaka 15, "kumsomesha mwanamke kwa kigezo cha kumuoa ni sawa na kuugua kansa ya damu, kamwe wasijaribu kufanya hivyo".
 
thank dear!
Waelimishe na wakaka wengine, manake penda usipende kumsomesha mdada ni kansa iko siku itajionesha
 
Kumlipia mtu masomo ni kama umefanya investment kubwa sana na mkaka hategemei -ve return ndio maana wanaumia sana.
Tunakabidhiwa funguo ya gari kadi anabaki nayo mwenyewe. Vikichacha unanyang'anywa gari fasta. Ila akikukosomesha hana ujanja. Aaah! Wakaka tusomesheni bwana, hatutaki magari. Hela za mafuta zenyewe hamtupi.
Husy usiombe kaka yako aingie kwenye scandal hii.Mimi mjomba kaka yangu flani alitaka jiweka kamba kisa mdada aliyemsomesha
 
Haya yote ni "mapenzi vigezo". Swali rahisi ni kuwa kama asingekuwa na hela hiyo dada asingempenda? Na wazazi walishiriki na binti yao katika utapeli? Pale UDSM kuna wahadhiri wamechanganyikiwa kabisa kwa sababu ya kusomesha vibinti vitapeli! Wengine hawataki tena kusikia neno kuoa, au mwanamke kwenye vichwa vyao! Wameamua kuoana na pombe!!
 
Lakini mimi jamani kuna kitu najiuliza.
Hivi kaka unampenda mtoto wa form one, unamsomesha kwa malengo ya kuoa huoni kama huyu dada ni mdogo na akili yake inabadilika kadiri anavyokua na anavyozidi kukutana na watu wa aina mbalimbali?

Sio kweli kwamba moyo wa huyu binti utakuwa umefanya maamuzi thabiti kwamba wewe ni mume wake!! Hata kama wakati huo atajiona hivo, lakini naamini kuna kipindi atawaona watu wanaomvutia na anaowapenda yeye kwa nafsi yake mwenyewe. Na ufahamu wake uliokomaa kwa wakati huo.

Kwa upande mwingine binti wa hivi simlaumu hata kidogo. Bora hata wa chuo.....na hata wa chuo bora umuoe ujue unasomesha mke wako. Vinginevyo msaidie tu kama mwanadamu wa kawaida ikitokea akawa mke, unashukuru.
 
Husy usiombe kaka yako aingie kwenye scandal hii.Mimi mjomba kaka yangu flani alitaka jiweka kamba kisa mdada aliyemsomesha

wapo rafiki zangu hayo mambo yamewakuta. Mimi nafikiri wakaka wanaposomesha wapenzi wao wasiwekee asilimia mia kwamba watawaoa kama vumbi alivyosema.
Ila ni vizuri kuwaendeleza wapenzi wenu na mchukulie ni jambo la kawaida kama mambo mengine mnayowafanyia.
 
umesema vema mama,mimi ntamsaidia kama sehemu ya mapenzi yangu kwake nikimaanisha nnapo kuwa nae nitatamani kuplay part ktk maisha yake na aina maana kuwa ni lazma kumuoa ingawa nakubali kabisa kufanya yooote haya kuna future unatengeneza
 
Upo sawa kabisa, kusomesha kwa kigezo cha kuoa ni kujitafutia Kifo, kuna mifano mingi ya ndugu zetu walioangukia katika mtego huo
 
wewe leta utani lakini juzi jmosi mkaka kapelekwa hospital hoi kameza midawa kisa demu aliyemsomesha.[/QUOTE]

Ikiwa huyu kaka alihisi katumiwa kwa kumsomesha baadaye kuwekwa kando, inaonesha na yeye pia alikuwa anatumia pesa zake kutaka kununua penzi. Kama angekuwa kaka mwenye akili kidogo, angeshukuru kuwa imetokea hiyo mapema mara tu baada ya dada kumaliza masomo, vyenginevye "angeliendelea na biashara" isiyolipa maisha. Mapenzi hayanunuliwi.

Unapomsomesha mtu ili kutoka ujinga na baadaye anakuwa mjinga zaidi, mwepuke kama njaa.
 
Lakini mimi jamani kuna kitu najiuliza.
Hivi kaka unampenda mtoto wa form one, unamsomesha kwa malengo ya kuoa huoni kama huyu dada ni mdogo na akili yake inabadilika kadiri anavyokua na anavyozidi kukutana na watu wa aina mbalimbali?

Sio kweli kwamba moyo wa huyu binti utakuwa umefanya maamuzi thabiti kwamba wewe ni mume wake!! Hata kama wakati huo atajiona hivo, lakini naamini kuna kipindi atawaona watu wanaomvutia na anaowapenda yeye kwa nafsi yake mwenyewe. Na ufahamu wake uliokomaa kwa wakati huo.

Kwa upande mwingine binti wa hivi simlaumu hata kidogo. Bora hata wa chuo.....na hata wa chuo bora umuoe ujue unasomesha mke wako. Vinginevyo msaidie tu kama mwanadamu wa kawaida ikitokea akawa mke, unashukuru.

Well said LD. Na kama mtachunguza, wengi wanawasomesha wasichana ni watu wenye umri mkubwa na kipato. Kwa nini wasitafute watu wa umri wao? Mara nyengine unaweza hata kusema wamejitakia na yanayowakuta ni stahiki yao. "Fanya wema wende zako, usingoje shukurani"
 
Back
Top Bottom