Hapa ndipo ufahamu na uzalendo wa Mr. President huwa nautilia mashaka

Hivi ni lini CCm na mwenyekiti wao watajifunza kuwajibika kwa makosa yao! kila inapoletwa hoja ya maana juu ya mustakabari wa nchi na wananchi wana CCM haraka hukimbilia kusema CDM! haya hapa hoja ni Kwa nini Rais anachagua wananchi wa kuwalinda! haraka wanaCCM wamekimbilai CDM! ni lini CCM mtaacha kuota juu ya jinamizi la CHADEMA?
 
Karibu sana JF. Napenda kukutaarifu/kukusisitiza kwamba this is home of Great Thinkers na sio upuuzi

JF haina uhusiano wowote na chama chochote cha siasa. Kunawanasiasa wengi tu ambao ni member hapa JF, ila JF sio member wa chama chochote. Hivyo huna sababu ya kuwajulisha cdm kuwa wewe ni gamba kupitia JF.

Kuhusu uhalifu, sote hatukubaliani, lakini hatuwashughulikii kwa kuwaua. Hivyo ni kinyume cha sheria. Au waliyemuua mwana ccm ni wahalifu kuliko walioua tarime!? .

Kama kweli wewe ni ccm na unadhani cdm itasubiri miaka 100 kushinda uraisi, pole sana! Sijui upo kwenye shimo gani? Waulize akina Butiku, Kaduma, nawengineo watakuamsha na sio kusikiliza redio uhuru tu!

Ukitaka kujua u.j.u.ha wa hawa viongozi wetu ni jinsi wanavyojikanganya katika mambo. Wamewapiga risasi kwa kuwaita majambazi waliovamia mgodini. Fine. Sasa inakuwaje serikali hii hii inataka kuwasaidia wafiwa mazishi? Unaua mwizi halafu unamsaidia azikwa, na unatoa rambi rambi? Du! TUJIULIZE HAPA
 
hivi ni lini ccm na mwenyekiti wao watajifunza kuwajibika kwa makosa yao! kila inapoletwa hoja ya maana juu ya mustakabari wa nchi na wananchi wana ccm haraka hukimbilia kusema cdm! Haya hapa hoja ni kwa nini rais anachagua wananchi wa kuwalinda! Haraka wanaccm wamekimbilai cdm! Ni lini ccm mtaacha kuota juu ya jinamizi la chadema?

najibu kwenye red tu; ni mpaka pale mtakapoacha kuwapigia kura. Napita
 
Muganyizi punguza jazba,halafu great thinker ni mtu mwenye busara, huwa hatukani ovyo.kuolewa ni sehemu ya maisha, kama vile ambavyo wengine wanavyoishi kwa namna mbalimbali.hebu niambie wale wananchi unasema walikusanyika kudai haki zao, je haki inadaiwa kwa mapanga? na kwamba ndio unasisitiza kuwa watu wadai haki kwa mapanga?

We unajua njia ngapi za kudai haki? We unadhani haki inapatikana kwa kuchekacheka kama kiongozi fulani ambaye anakili kuwa haijui dowans. Unapofumbia macho kitu ambacho kiko wazi lazima watu wakufananishe na mtu aliyeko kwenye ndoa, maana hata kama mmeo anakunya kitandani baada ya kulewa hutasema kwa majirani, utazidi kumpamba tuuu. Wewe huyo(kwenye picha) angekuwa bibi yako ungesemaje? Anapendeza?
 
Hodi wana JF. nimekuwa ni msomaji maarufu sana lakini nikawa nashindwa kuchangia hoja kwa kuwa sikuwa member wa jamvi.lakini nimelazimika kujiunga nanyi ili tuwe pamoja.ila nasikitika kuwaarifu wana chadema kuwa mimi ni gamba laini (ngozi) ambayo kila mtu anayo,kwa hiyo sisi sote ni watu wa magamba ila magamba hayo yanapokuwa magumu kama ya nyoka au kenge basi upo umuhimu wa kuyavua ili libaki gamba laini.Sasa ndugu yangu ,kama serikali itawaacha watu wafanye watakalo,nchi hii hatafika popote.walevi wataenda kuvamia TBL ili wapate bia za bure,majangili watavamia mbuga wapate meno ya ndovu na kila mtu atafanya ki vyake.hebu fikiria kama polisi wasingefanya hivyo walivyofanya,leo hii mgodi huo ungekuwaje.hebu niambie hao chadema wakichukua nchi watawanyanganya polisi SMG zote wa wabakiwe na virungu? wahalifu ni wahalifu tu hata kama watakuwa ni ndugu zako wa tumbo moja.Tusikumbatie ujinga, hakuna nchi au serikali inayopenda kuua watu wake, lakini pia hakuna serikali inayokubali kundi la wahuni kuvuruga utawala wake,hao watashughulikiwa kwa nguvu zote.subirini chadema ichukue nchi ili mukagawane hizo dhahabu na wanyama huko serengeti,miaka 100 sio mingi mutatawala tu.

Karibu,

ila fikiri kwanza kabla ya kuandika, ulichosema kinafahamika lakini ni kwa nini serikali yako imeacha mgogoro huu mpaka umefikia hapo?, unajua historia ya mgogoro wa North Mara?, Serikali imeshachukua hatua gani mpaka sasa? hii ya kuua watu? fikiri vizuri ndugu.
 
tutegemee nini kutoka kwa biased President?Juzi kati na Arusha kuna mlinzi mmoja wa kampuni ya madini kauwawa na majambazi,mboni hakutoa tamko wasakwe kwa udi na uvumba?
 
Mbona hatujawasikia viongozi wacdm wakisema loilote kuhusu Mwankenja? Au huyo si raia wa Tanzania?
 
Kweli nimeamini kikwete ni Popular sana, never goes a day without having a post about KIKWETE this shows how much support Mr President is enjoying even during these tarbulent times.
Hapana mimi nina mtazamo tofauti na wewe. Huyu ni mtu aliyepewa atulindie nyumba(nchi) yetu kwakutoa maamuzi fulani fulani, ni mtu anayejua siri ya pato la nyumba (nchi) na matumizi yake etc. Inabidi uwe unafuatilia kwakaribu nyendo zake hasa unapoona mambo yanaenda mrama maana, unaweza kuamka ukakuta nyumba si yako tena. Akiachia ngazi au kumaliza muda wake no body will bother. Nafikiri hilo liko wazi hata kwa marais waliopita.
 
Kweli nimeamini kikwete ni Popular sana, never goes a day without having a post about KIKWETE this shows how much support Mr President is enjoying even during these tarbulent times.

kwa mwendo huu kamwe hatufiki. Yaani mtu akitajwa kila siku bila kujali kinasemwa nini juu yake basi is enjoying support. Nadhani JF muanze kufikiria mtandao mwingine. This is not the kind of thing we subscribed for.
 
wewe ndio unapaswa ujipime, sioni tatizo la hii nyuzi.

Namuunga mkono mleta nyuzi, jk ana watu ambao anafikiri wanastahili kuishi na wengine hawana haki hiyo. Jk ni muuaji, yeye ni amiri jeshi mkuu, mauaji yote yanayofanywa na majeshi yetu yana mkono wake, na sidhani kama muuaji anaweza kutoa tamko au rambirambi za mauaji aliyoyafanya.

mchangiaji atakuwa chama cha dovutwa
 
Jesuit: I guess haupo mentally ok. Hivi habari iliyoletwa hapa ina uhusiano gani na CHADEMA? Ni watu wangapi wameuawa na majambazi hapa nchini na hatukuwahi kusikia Rais akitoa tamko lolote? Iweje leo ameuawa kiongozi wa CCM basi harakaharaka kuagiza wauaji wasakwe? Ni mara ngapi wameuawa watu mhimu kwa nchi yetu wakiwemo maprofessor ambao tunawahitaji sana kwa maslahi ya wengi, lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na serikali kukabiliana nayo? Je unakumbuka yale mauaji ya watanzania zaidi ya 10 kule ukerewe? Rais alisema nini juu ya yale? Acheni ushabiki wa kishamba jamani, ihurumieni nchi yenu. Huyu Rais ana shida, nashangaa kwanini watu hamuoni hilo
alipouawa Prof. Mwaikusa, wauaji walisakwa?
 
Back
Top Bottom