Elections 2010 Hapa Kuna Mushkeli

AHADI nyingi za Serikali ya awamu ya nne zilizomo kwenye ilani ya uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) 2005-2010 hazijatekelezwa badala yake viongozi wake wamekuwa na majigambo ya kuwaadaa wananchi bila bila chochote.
Akichangia mjadala wa bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni jana, Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Bi. Halima Mdee, alisema anawashangaa viongozi wa Serikali kujigamba mbele ya wananchi bila aibu kwamba wamefanikiwa kutekeleza ilani yao jambo ambalo si kweli.
“Hebu tuache unafiki, sisi ni wanasiasa yaliyomo kwenye ilani ya CCM mengi hayajatekelezwa na hayatekelezeki, lakini mmekuwa mkipita barabarani na kuwadanganya wananchi kuwa mmetekeleza mambo mengi.
“Nasikia mnataka kuandika ilani nyingine, mi nadhani msijihangaishe na kuandika nyingine, tumieni hii hii ya mwaka 2005 maana hamjatekeleza mlioahidi humo, endeleeni nayo tu na mrudi kwa wananchi muwaambie mmeshindwa,” alisema Bi. Mdee.
Alisema jinsi serikali ya CCM inavyozidi kuwa madarakani ndivyo wananchi wanavyozidi kuwa katika hali duni kimaisha na kutoa mfano wa kufilisika kwa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kwamba mwaka 2005 ilikuwa na ndege nne lakini hivi sasa ipo mbioni kuzikwa kabisa.
“lakini shirika hilo sasa hivi liko ICU (chumba cha wagonjwa mahututi)”.Alisema Mbunge huyo.
Kuhusu sera ya ubinafsishaji alisema jumla ya makampuni 60 zilizobinafsishwa lakini sasa zinazofanya kazi ni chache na kwamba hiyo ni dalili ya kushindwa kwa serikali.
Alisema Rais Jakaya Kikwete, alipoingia madarakani aliwaahdi wananchi kuwa kila wilaya itakuwa na chuo cha ufundi ahadi ambayo haijatekelezwa hadi asa.
Alisema uwiano wa kipato kati ya mwanamke na mwanamume ni mdogo sana na kuongeza kuwa wanawake wanazidi kuwa katika hali duni ya maisha huku Serikali ikijigamba kwamba wanawake wamekombolewa na kupiga hatua kubwa zaidi.
Naye Mbunge wa Temeke (CCM) Bw. Abbas Mtemvu, alionesha dalili ya kumjibu moja kwa moja Bi. Mdee alipoanza mchango wake kwa kutoa hadithi kwamba 'mtoto acha kupiga mayowe acha watu waone wenyewe' hivyo kusababisha vicheko kutawala ukumbi wa Bunge.
Alisema Serikali ya CCM imefanya mambo mengi na imetekeleza mambo mengi yaliyomo ndani ya Ilani yake hivyo si suala la mtu kuambiwa kwa madai kwamba mambo hayo yanaonekana hadaharani.
Kwa upande wake mbunge wa Lupa (CCM) Bw. Victor Mwambalaswa, aliishauri Serikali kuacahana ununuzi wa magari ya kifahari yanayogharimu mamilioni ya fedha za walipa kodi ambazo zingetumika katika shughuli za maendeleo.
Aliitaka Serikali kuiga nchi jirani za Kenya, Zambia na Rwanda ambayo Rais wake aliamuru kuuzwa kwa magari yote ya kifahari na kununua magari ya bei ya chini.
Alisema magari ya kifahari yanachangia matumizi makubwa serikalini huku wananchi wakiendelea kuwa maskini.
CHANZO MAJIRA
 
AHADI nyingi za Serikali ya awamu ya nne zilizomo kwenye ilani ya uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) 2005-2010 hazijatekelezwa badala yake viongozi wake wamekuwa na majigambo ya kuwaadaa wananchi bila bila chochote.
Akichangia mjadala wa bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni jana, Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Bi. Halima Mdee, alisema anawashangaa viongozi wa Serikali kujigamba mbele ya wananchi bila aibu kwamba wamefanikiwa kutekeleza ilani yao jambo ambalo si kweli.
"Hebu tuache unafiki, sisi ni wanasiasa yaliyomo kwenye ilani ya CCM mengi hayajatekelezwa na hayatekelezeki, lakini mmekuwa mkipita barabarani na kuwadanganya wananchi kuwa mmetekeleza mambo mengi.
"Nasikia mnataka kuandika ilani nyingine, mi nadhani msijihangaishe na kuandika nyingine, tumieni hii hii ya mwaka 2005 maana hamjatekeleza mlioahidi humo, endeleeni nayo tu na mrudi kwa wananchi muwaambie mmeshindwa," alisema Bi. Mdee.
Alisema jinsi serikali ya CCM inavyozidi kuwa madarakani ndivyo wananchi wanavyozidi kuwa katika hali duni kimaisha na kutoa mfano wa kufilisika kwa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kwamba mwaka 2005 ilikuwa na ndege nne lakini hivi sasa ipo mbioni kuzikwa kabisa.
"lakini shirika hilo sasa hivi liko ICU (chumba cha wagonjwa mahututi)".Alisema Mbunge huyo.
Kuhusu sera ya ubinafsishaji alisema jumla ya makampuni 60 zilizobinafsishwa lakini sasa zinazofanya kazi ni chache na kwamba hiyo ni dalili ya kushindwa kwa serikali.
Alisema Rais Jakaya Kikwete, alipoingia madarakani aliwaahdi wananchi kuwa kila wilaya itakuwa na chuo cha ufundi ahadi ambayo haijatekelezwa hadi asa.
Alisema uwiano wa kipato kati ya mwanamke na mwanamume ni mdogo sana na kuongeza kuwa wanawake wanazidi kuwa katika hali duni ya maisha huku Serikali ikijigamba kwamba wanawake wamekombolewa na kupiga hatua kubwa zaidi.
Naye Mbunge wa Temeke (CCM) Bw. Abbas Mtemvu, alionesha dalili ya kumjibu moja kwa moja Bi. Mdee alipoanza mchango wake kwa kutoa hadithi kwamba 'mtoto acha kupiga mayowe acha watu waone wenyewe' hivyo kusababisha vicheko kutawala ukumbi wa Bunge.
Alisema Serikali ya CCM imefanya mambo mengi na imetekeleza mambo mengi yaliyomo ndani ya Ilani yake hivyo si suala la mtu kuambiwa kwa madai kwamba mambo hayo yanaonekana hadaharani.
Kwa upande wake mbunge wa Lupa (CCM) Bw. Victor Mwambalaswa, aliishauri Serikali kuacahana ununuzi wa magari ya kifahari yanayogharimu mamilioni ya fedha za walipa kodi ambazo zingetumika katika shughuli za maendeleo.
Aliitaka Serikali kuiga nchi jirani za Kenya, Zambia na Rwanda ambayo Rais wake aliamuru kuuzwa kwa magari yote ya kifahari na kununua magari ya bei ya chini.
Alisema magari ya kifahari yanachangia matumizi makubwa serikalini huku wananchi wakiendelea kuwa maskini.
CHANZO MAJIRA

Unajua Tanzania ina wilaya ngapi na vyuo vya ufundi vingapi?:confused2:
 
Back
Top Bottom