Elections 2010 Hapa Arusha, kweli NEC haimthamini mpigakura!!!!!!!!!!!!

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Kuanzia jana na leo asubuhi ninaendela kukagua vituo vya kupiga kura hapa Arusha mjini na nimebaini ya kuwa NEC haimthamini hata chembe mpigakura.

Makaratasi yenye majina ya wapigakura yamezagaa sakafuni na kuwalazimu wapigakura kuokota baadhi ya makaratasi hayo kuhakiki majina yao kama huu siyo mkakati wa kuwazuia wapigakura wasipige kura basi ni nini?

Jamani hivi NEC watasema gundi hawana ya kuhakikisha makaratasi yenye orodha ya wapigakura yanagangamala kwenye kuta au watakuwa na visingizio vipi na kwa nini tatizo hili limeanza uchaguzi huu?
 
KAKA WASHAJUA KUWA JIMBO HILO LIMEKWISHA CHUKULIWA NA CHADEMA CHINI YA MH; GODBLES LEMA NDIO MAANA HAWAWEZI KUWATHAMINI KWA LOLOTE. WANANCHI MSIOGOPE SIKU YA KUPIGA KURA NENDA KITUONI UTAMKUTA KARANI MWONGOZAJI UKIWA NA KITAMBULISHO ATAKUPA MAELEKEZO JUU YA KUPIGA KURA. VOTE FOR SLAA PLEASSSSSSSSSSS:israel:
 
ni bora wakarekebisha kwa maana tunaambiwa mabilioni ya shilingi yameidhinishwa kwa kazi hii; uchaguzi mkuu 2010.
 
Kama hawana gundi si ununue na kuyabandika vizuri? Au unataka imprest yote ya stationery itumike kwa kiwango cha 100% wakati wenzao za matundu ya choo nyingi zinabaki kwa watendaji?
 
Kuanzia jana na leo asubuhi ninaendela kukagua vituo vya kupiga kura hapa Arusha mjini na nimebaini ya kuwa NEC haimthamini hata chembe mpigakura.

Makaratasi yenye majina ya wapigakura yamezagaa sakafuni na kuwalazimu wapigakura kuokota baadhi ya makaratasi hayo kuhakiki majina yao kama huu siyo mkakati wa kuwazuia wapigakura wasipige kura basi ni nini?

Jamani hivi NEC watasema gundi hawana ya kuhakikisha makaratasi yenye orodha ya wapigakura yanagangamala kwenye kuta au watakuwa na visingizio vipi na kwa nini tatizo hili limeanza uchaguzi huu?

Halafu wana akili siyo nzuri. Hapa DSM jamaa yangu mmoja kaniambia katika kituo cha Ilala Mchikichini (nyuma ya soko la nguo) orodha za majina wamebandika nje ya geti ya bohari moja. Hakuna kinga yoyote ya jua au mvua. Jee ikija mvua, orodha hizo si zitaharibika?
 
Back
Top Bottom