Hanilizishi kwa lolote nifanyeje?

Jf never boring
Mke hamridhishi na anataka kumuacha na anawasikiliza wazazi wake kuhusu mke
Je aliwaolea wazazi wake au alioa kwa sababu yake mwenyewe

Sidhani kama anajielewa huyo. Dalili za kuwa na nyumba ndogo huwa zinaonekana hivihivi. Yawezekana jamaa kaona au kaonja sehemu nyingine, sasa ndo anajidai eti mkewe hamridhishi!!! Uzushi tu....!!!!
 
ukome wenzio huwa wanaridhika kwanza kabla hawajabebana,inaelekea wewe na mwenzio mlibebana kwanza kabla ya kujihakikishia nq kuridhika kama anatick vigezo vyote kwenye checklist yako.....shaurilo umelikoroga sasa linywe......

1,mchukulie mkeo kama binadamu sio object/toy la kukustarehesha na kukufurahisha tu.....

1.acha kugonga nje,in that way you will stop making comparison kati ya mkeo na vimada wengine....

1.mume ni mtu,binadamu tu kama wengine sio mfalme wa kutumikisha mwanamke/wengine...badilisha kwanza haya mawazo.....

1.saidia kazi za nyumbani,watoto...mtoe mkeo for dinner/shopping....naye atamake 'efforts' 'kukuridhisha.........mnh
 
kuna mambo kadhaa hapa kaka ambayo yanakupelekea kuwa hivo ulivo:-

1. inawezekana kabisa kuwa nyumbani mna ugomvi ambao ni wa mda mrefu na hamjaupatia suluhisho na hivo kitu fulani kimekukaa moyoni na ndo mana unaona hakuridhishi japo anafanya kile anachotakiwa kufanya lakini wewe huoni.

2. inawezekana umepata mwanamke wa nje, tatizo la binadamu wakipata watu kama hawa, (awe mwanamke au mwanamme), huwa kuna kuwa na ile kasumba ya kipya kinyemi...wengi sana huwa tunafanya makosa tukiwa na watu kama hawa kwa kujaribu kulinganisha utendaji wao hawa watu na wake zetu wa nyumbani, lakini sio sawa na sio sahihi kulinganisha, kwa vyovyote tu mara nyingi utaona kipya kizuri zaidi.... kwani shati jipya na lile la zamani lipi linakuvutia zaidi kaka?. Hii sababu ya pili mimi ndo naipa nguvu sana.. na kama ndio acha huyo anayetaka kukuharibia nyuma maana ukimchukua na baadae ukapata kifaa kipya kingine mambo yatakuwa ni yale yale.

3. inawezekana wewe bwana ni chovya chonya, unapenda kuonja kila mwanamke na hivyo ukakutana na tofauti baina yao...binadamu hawafanani kaka na ndivyo ilivyo, na kwa kuwa mkeo unae kila dakika mnatazamana kila leo, mnananihiuuu kila siku unaona umeshamchoka..kwani umemzoea, jua kuwa tatizo la kuchokana katika ndoa sio kwako wengi linawasumbua na tu kwa sababu hawajajifunza kuwa kwenye ndoa kuna uwezekano wa kuchokana hivyo kutafuta njia mbadala ya kukabili hali hiyo inapotokea na kuifanyia kazi...

Ninachoweza kukuambia kaka, ufanyayo ni ya muda mchache na usidhani kwa kumuacha mkeo itakuwa suluhisho...kama unadhani ni suluhisho jaribu utakuja kutupa ushuhuda hapahapa jf baada ya miaka kadhaa, kama unazo..achana na nyumba ndogo zitakuharibia mengi tu, mrudie mungu wako, kaa na mkeo umwambie haya unayotuambia kwa hekima na mtafute wapi mmeteleza mrekebishe..

vitabu vya mungu vinasema, "Mwanamke Mpumbavu huaribu nyumba yake kwa mikono yake" mimi naongeza "hata mwanaume mpumbavu " vivo hivyo", hope utazingatia haya
 
duh! aibu
sasa mie naona kwanza wewe you are not being true to urself...upo kupendezesha wazazi.
wazazi wameona mengi na ni muhimu kupata muongozo wao lakini wao ni wanadamu na wanaweza kukosea

ila kwanza ngoja niseme kuwa kama imefikia kuwa hakuridhishi basi wewe lazima ubebe lawama ya kuwa ulifanya uchaguzi mbaya.
baada ya hapo sasa mie naona sio haki kukaa kwenye nyumba ambayo mwsho wa siku wewe huna furaha na pia hii itaelekea mpaka kwa mke na watoto kama unao.....sasa paki vilago vyako ila angalizo ni kwanba muachane kistaarabu na hapa ndugu yangu kama kweli wewe mwanaume naomba kabisa ukubali kuwa mama apate nusu ya mali zako, na pia watoto watakaa kwake...hilo jiandae kabisa becoz wewe ndio ulimuoa na hivyo uamuzi wako mbaya lazima uwe tayari kuulipia.

kazi ni kwako!!!!

taratibu babu wewe! tuliambiwa mke mmoja hadi kufa na milele, sharti avumilie hadi hapo atakapoitwa na Muumba! Pia unapomshauri waachane yeye aende wapi? kwani haendi kuridhika pia kwani haruhusiwi kuoa hadi huyu aondoke duniani au kama anarudi dhambini kwani atakuwa anazini tu! My take, amfundishe namna ya kukukuruka taratibu ataelewa na atafurahi Muke mumoja kwa Mume mumoja!......
 
muache mwaya kwann ujiue na mijipreasure ndani ya house mana hapo lazima unacheat kinoma nje bisha
 
Nashindwa kukusaidia bwana. Maelezo yako ''hayanilizishi''. Doctor hawezi kukusaidi kama utamueleza tu naumwa. Inabidi ujielezee, from your story we can detect something. Hebu elezea kinachotokea hasa mkiwa hizo sehemu za ''kulizishana''. May be wewe ndiyo chanzo. Labda kila ukirudi unanuka mvinyo, au unaingia sehemu ya ''kulizishana'' bila kuoga, au kuna mgogoro na mwanamke ''hakulizishi'' kama mojawapo ya strategies zake za kufikisha ujumbe flani kwako. Kwahiyo kuna mambo mengi na hayo ni baadhi tu. Towa maelezo ya kutosha tukusaidie.
 
Nimekuwa nikipata taabu kwa muda mrefu kwani mke wangu hanilizishi kabisa, na wazazi wangu hawataki nimuache nisaidieni wanaJF

ndo maana watu huwa 'wanachunguzana' kwanza kabla ya kuoana mkuu. pole sana ndugu huna jinsi hapo zaidi ya kuwaudhi madingi wako tu
 
Nashindwa kukusaidia bwana. Maelezo yako ''hayanilizishi''. Doctor hawezi kukusaidi kama utamueleza tu naumwa. Inabidi ujielezee, from your story we can detect something. Hebu elezea kinachotokea hasa mkiwa hizo sehemu za ''kulizishana''. May be wewe ndiyo chanzo. Labda kila ukirudi unanuka mvinyo, au unaingia sehemu ya ''kulizishana'' bila kuoga, au kuna mgogoro na mwanamke ''hakulizishi'' kama mojawapo ya strategies zake za kufikisha ujumbe flani kwako. Kwahiyo kuna mambo mengi na hayo ni baadhi tu. Towa maelezo ya kutosha tukusaidie.

bolded n red: Ndo maana wageni wengi wanaojifunza lugha ya kiswahili huwa hawaelewi kwa haraka lugha hii.
 
Back
Top Bottom