Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Handbag ya Madam

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by naima79, Aug 21, 2012.

 1. naima79

  naima79 JF-Expert Member

  #1
  Aug 21, 2012
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 205
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Habari zenu wapendwa, Jamani naomba mnisaidie nina tatizo dogo tu ambalo kadri siku zinavoenda naona linanikwaza, mume wangu kila nikirudi home kutoka job au popote tu lazima atavizia handbag yangu ataipekua, nimeshamkutia karibia mara 15 sikumuuliza wala sikuchukia, juzi nimemkutia tena na hafanyi hivo mbele yangu anapekua kwa usiri hivo ata kumkutia inakuwa ni bahati tu, hiyo ya juzi nilikuwa nimetoka chuo nikaenda kuweka handbag room, nimerudi sitting room nimekaa kama dakika 5 tu akaja nayeye alikuwa chumbani, akachungulia pale sitting room kaniona niko busy na mtoto akarudi tena chumbani, namie hapohapo nikaingia chumbani nikamkuta tena busy anachambua handbag yangu, jamani ata kama kuna kitu anatafuta kwa mara hizo zote angekuwa ameshakipata, mimi binafsi nachukia na nilishawai kumwambia karibuni tu kama mara ya 13 hivi kuwa kwanini unapenda kufungua handbag yangu, unatafuta nin nikamuuliza vipi mimi nikiwa nakagua mifuko yako ya suruali kila ukirudi utajisikiaje maana wanaume hawabebi handbag, nikamwambia naomba uwe na imani na mimi hili jambo kwakweli linanikwaza, tangia nimemwambia hiyo juzi kaninunia mpaka leo hii eid imepita kimyakimya tu, jamani nisaidieni nifanye nini ili huyu mtu awe na imani namm au anatafuta sababu?
   
 2. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #2
  Aug 21, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 13,021
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 180
  Kipo anachokitafuta huyo!
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Aug 21, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,014
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  snowhite, kwani wewe kinakuudhi nini iwapo huyo Mr wako akichungulia handbag yako?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Asabaya

  Asabaya JF-Expert Member

  #4
  Aug 21, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 1,319
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Shosti huyo hajiamini kama yuko peke yake.lakini kwakweli nitabia mbaya sana mwanamme kufungua Handbag ya mkewe
  malezi gani hayo alolelewa? tena usimcheke bora ajue kama hupendi na usichoke kusema,ama sivyo ukimuachia atataka akupekua mpaka kwenye chupi ajue kama umelala namwengine au laa.
   
 5. UPOPO

  UPOPO JF-Expert Member

  #5
  Aug 21, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 1,021
  Likes Received: 149
  Trophy Points: 160
  Naiman tupo wengi tunaokerwa na hali hii ,mimi mume wangu ana the same tabia mimi sijawahi kumwuliza ila naona nitaanza kwani mimi sijawahi hata kugusa pochi yake unless kama natafuta kitu na awe amenituma
   
 6. Jiwe Linaloishi

  Jiwe Linaloishi JF-Expert Member

  #6
  Aug 21, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 3,676
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Pole sana eid yote imepita kimya na kamvua kale kalivyoinogesha. kama huna wasisi na hakuna baya unalofanya jitahidi kuvumilia atapekuwa mpaka mwishowe ataache mwenyewe ukimkataza anaweza kupata sababu. anaonekana kachelewa badala ya kumendea simu anamendea handbag!!?
   
 7. naima79

  naima79 JF-Expert Member

  #7
  Aug 21, 2012
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 205
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mpitanjia, naona huyu mtu kwa hali hii aliyojiwekea inawezekana ata akikaa offisini ananiwazia mabaya tu mda wote, sasa hii hali itakuja kumuathiri bila sababu ya msingi

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. naima79

  naima79 JF-Expert Member

  #8
  Aug 21, 2012
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 205
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Thanks Asabaya

   
 9. naima79

  naima79 JF-Expert Member

  #9
  Aug 21, 2012
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 205
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  UPOPO mie mpaka nimekuja kumuuliza mda umepita nilikuwa siulizi mapema nilijua akijiridhisha ataacha mwenyewe, sasa naona tabia inaendelea tu ila kwakweli mimi nakwazika sana

   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Aug 21, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 11,455
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Anajaribu kutafiti kama na dollar nazo ni moja ya currency zinazoingia kwenye handbag. Khaa, wanaume kazi ipo!
   
 11. Jiwe Linaloishi

  Jiwe Linaloishi JF-Expert Member

  #11
  Aug 21, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 3,676
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  we mstaarabu mi wa kwangu nikirudi nikiwa nimeutwika ananisachi wakati nakoroma.. kumbe hajui watakatifu tuko wachache
   
 12. naima79

  naima79 JF-Expert Member

  #12
  Aug 21, 2012
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 205
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Jiwe nimesahau tu kukujulisha ya simu, anaanzaga katika handbag anamalizia katika simu, tena simu ndio never miss, na wakati huohuo ana password ya yahoomail yangu, na anapassword ya fb pia, kwaiyo anapita huko kote daily japo sikwaziki katika hivo maana password nimempa mwenyewe
   
 13. Kambaku

  Kambaku JF-Expert Member

  #13
  Aug 21, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 1,083
  Likes Received: 354
  Trophy Points: 180
  Hamna tatizo kukagua chochote cha mkeo na yeye ni ruksa kukagua chochote cha kwako, kwanini uogope na hakuna magendo humo ndani? Kila atakachokiona akiuliza atapata jibu lake tu. Tatizo hapo ni kwanini anakagua kwa siri? Kwanini hakagui mbele yako tu.

  Jiamini Naima, mwache akague tu au kuna kitu hupendi akione?
   
 14. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #14
  Aug 21, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,879
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  We hebu ongea na mmeo kwa upole tu huna haja ya kutumia nguvu nyingi na hasira ili mfikie muafaka.Ushauri wa humu changanya na zako.
   
 15. naima79

  naima79 JF-Expert Member

  #15
  Aug 21, 2012
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 205
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hakuna chochote ambacho sipendi akione, ila napenda awe na imani na mimi, kwanini haniamini wakati mie mkewe na sina balaa lolote ambalo ananiwazia

   
 16. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #16
  Aug 21, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,434
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  anajua umekuja na mwanamme kwenye poch yako !!!!!
  mtegee mavi ya mtoto au mtego wa panya akiingiza tu mkono atanasa thenunamwambia kuna panya huwa anaingia ndani ya pochi kukagua kila siku leo ndio 16 yake pale pale mwambie ulikuwa unatafuta nini? alafu kila siku mpe mwambie kagua basi ili nipeleke ndani au unaiweka juu ya laptop yake au mahali ambapi lazima ataigusa!
   
 17. Bra-joe

  Bra-joe JF-Expert Member

  #17
  Aug 21, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,342
  Likes Received: 274
  Trophy Points: 180
  Kwa kuwa umekwishaijua hiyo tabia yake wasiwasi wako wa nini? Si usiweke vitu vya ajabu ajabu ktk hand bag yako, kuishi na mtu ni kujifunza mapungufu yake ili uweze kuishi nae. Hapo nakushauri kila siku ukifika nyumbani, baada ya kusalimiana tu, mpe hand bag yako aikague halafu akupelekee chumbani, ukifanya hivyo mara mbili tu msg itakuwa sent, pia usipende kuificha hayo hand bag yako, iweke peupe siku zote.
   
 18. Jiwe Linaloishi

  Jiwe Linaloishi JF-Expert Member

  #18
  Aug 21, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 3,676
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ok pole maadam ushamwambia ukweli mwache nafikiri kuna kitu anahisi juu yako ndio anatafuta ukweli jitahidi kumvumilia atachoka kufwatilia mwenyewe ataacha. password ya huku hujampa? tusije kuPM kumbe ni yeye tukakuharibia!!
   
 19. Bra-joe

  Bra-joe JF-Expert Member

  #19
  Aug 21, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,342
  Likes Received: 274
  Trophy Points: 180
  Au labda anatumia vipodozi vya kike? Anaona aibu kwenda kununua dukani watamshangaa, kwahiyo anatumia vyako kinyemela na wewe unahisi anakukagua kumbe la.
   
 20. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #20
  Aug 21, 2012
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,699
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Nawe mwombe password zake za simu, emails zote uone kama utapewa.... huyo mumeo anawivu ambao mie nauita ni wa kitoto kwanini hajiamini yaelekea anayoyafanya yeye huko nje wewe huyajui anadhani nawe unayafanya na ndio maana kutwa kiroho chake kiko juu kwa kukuwazia mabaya.... mkanye na usichoke kumkanya kwani anakuja kuathhirika kisaikolojia kwa kuhofia vitu ama mambo amabayo hayawazii kuyafanya.

  iko siku ukitaka kutoka ama akiwa anatoka atakagua chupi uliovaa asubui ndio atakayo kukuta nayo jioni ukitaka kuoga lazima uombe ruhusa maana ukioga kubadilisha kabla hajrudi kosa....
   
Loading...