Handbag ya Madam II - Nimepewa talaka

Kwa sababu mmeachana kwa sababu zisizo na kichwa wala mkia, mtarudiana tu. Lakini mshikishe adabu. Usipopata uhuru wako kipindi hichi hutakaa uupate tena.
Kwanza badilisha password za accounts zako zote. Kama anakuamini upya then hahitaji kukufanyia monitoring tena. Pili mkubaliane mambo ya msingi. Kama yeye ana marafiki na anaweza kuwasiliana nao basi nawe sawia.
Haya yote mpeane muda wa kupumua kwanza. Hebu kaa kwa dada yako uone utakavyofurahia stress free life. Usimtegemee kurudi kukutafuta, na wewe usitafute mambo yake ili usiumie. Hilo gereza la ndoa, either utoke ama ujitengenezee utaratibu wa kumudu mazingira. Muonyeshe upo uwezekano wa wewe kumuacha na kuendelea na maisha

Kingas'ti hayo ya nyekundu sikubaliani nayo, labda kama tunaongea theory na sio practical.
Kwa walio kwenye ndio watasema watakubaliana nami hivyo vitu kama tabia ipo ipo tu haiwezekani itatoka eti kwa makubaliamo.Thubutu!
 
Maana hiyo ya mawasiliano kuwakwaza wanaume ipo kitambo sana, tena kuliko wanawake wanaume wengi huumia sana na hilo
 
Yaani kaka hiyo paragraph ya pili siwezi kukubaliana na wewe, yaani mtu uache kuwasiliana na watu eti kwa sababu kuna mtu fulani hata kama anaitwa mke au mume anayo mawazo ya kijinga kuhusiana na mawasiliano hayo? Cha muhimu kufanya ni kumfahamisha huyo mtu ni nani na lengo la mawasiliano yenu ni nini? Kwa sababu kumbuka huyo mke ulikutana naye akiwa tayari mtu mzima huwezi hata siku moja kufikiri kwamba hajawahi kuwa na uhusiano na watu wengine shuleni, kazini, nyumbani na kwingineko. Jambo la msingi ni kuaminiana vinginevyo mtu akiamua kutoka nje ya ndoa anaweza akakuomba hata wewe mwenyewe kumsindikiza na ukamsubiri na mkarudi wote kumbe alienda kukutana na mwenzake. NI NGUMU SANA KUFIKIRI KWAMBA UNAWEZA KUMDHIBITI MTU MWENYE KICHWA KIMOJA NA UBONGO MMOJA KAMA WEWE KWA KUTUMIA KICHWA NA UBONGO HUOHUO MMOJA. Poor husbands with such stupid behaviour

Mitazamo, uelewa na misimamo imetofautiana kati ya mtu na mtu, ni jukumu letu kutoa kile tunachofikiria kwa mhusika kuwa ni sahihi na yeye mwenyewe atachuja kipi kibaya na kipi kizuri cha kuchukua. Unapokula samaki, hakuna anayekwambia toa mwiba, ila ukikuchoma utautoa mwenyewe na kuendelea kula minofu! Ndicho mpendwa wetu anachotakiwa kufanya.
Nakubaliana na changamoto zako maana mimi na wewe hatuko sawa!!! Ila ni vyema pia tutumia lugha nzuri.
 
Ok, nafurahi kusikia hivyo, kuwa muwazi, Matatizo ya simu nafikiri siyo hapa umeyasikia na wala si leo, wanaume wengi wapo hivyo, haya hayana ubishi umesikia sana kwa rafiki zako, ndio maana kitu kama upekuzi wa pochi na simu kwangu sio issue, issue ni kuchelewa kurudi maana waume wengi upekuzi kwa wake zao wanafanya sana, jichunguze hata wewe utasema,

Kuachana ni mbaya sana ila ikibidi sawa, visababu visivyo na msingi huwa vinakuwa na sababu kubwa imejificha! Yatuasa kuangalia vema maisha yetu na ya wanandoa wenzetu kisha tumshauri na ushauri wetu uwe wa kujenga sio kubomoa
 
Ndoa ni muunganiko wa watu wawili waliokulia makazi na wenye tabia tofauti, uvumilivu na kujaliana ni muhimu, ukiwa sana selfish ni hatari ukitaka tamthilia kupeleka kwenye ndio kabisa unaharibu. Hapa dada inabidi ajue anarudi usiku sana kwa sababu ipi au anakuwa sehemu gani aanzie hapo
 
Kwa maelezo yako tu nimeona umeleta/umeeleza ukweli si story ya kutunga..............

Huyo jamaa hakupendi kabisa na alikuwa anakutafutia sababu ili akuache ndo maana
alikuwa anakupekua pekue apate pa kushika na ameona wewe unampenda
na kumuheshimu ndo maana akakutenda .........Usirudiane nae kabisa sababu
atakutenda zaidi akuletee mwanamke ndani ya nyumba.....................

Kuwa na siku njema asikuumize kichwa wanaume hakuna wa tofauti wanafanana tabia
 
kupekuwa sio sababu, waume wengu wanafanya hivyo hata kwa kunyata hili halina ubishi, kama hujui basi tambua hilo, yeye alikuwa anapekuwa wazi wazi. Kusema hakuna tofauti nakataa ndio maana kuna wanaopiga na wasiopiga kuna ambao hawatoki nyumbani bila sababu na kuna ambao kushinda nyumbani ni adhabu.

Tabia huwa zinatifautiana, Ukweli ni kwamba asiogope ndoa,
 
kwa kweli dada yetu mumeo ana wivu uliopitiliza...je hajui kuwa wewe nawe una marafiki?sikatai kuhoji ni nan kakupigia simu nk, bt muhimu ni kulinda heshima ya unayemuuliza au anadhan wewe huongei na watu? ana mapungufu gan mumeo?naamin hiyo anayotumia ni defense mechanism ya jambo fulani...sasa kama walijua hilo jambo then tuanzie hapo..
I mean kwanza mueleweshe akuelewe kuwa wewe umempenda yeye kama alivo na ndio maana umeolewa naye..hakikisha unamthibitishia hilo vizuri.
kisha dai uhuru wako, na katika hili kuwa extra serious, maana nina hofu kama kaanza huku mwishowe usijeshangaa ukiambiwa hakuna kufanya kazi au kwenda hata kwenu. usikubali ndoa yako ivunjike kiurahisi, lakin ili ndoa yako idumu lazima na wewe uwe wazi na akuelewe...he has to understand women needs to be loved na sio used.
pole sana dada. Mungu akuongoze katika hilo.
 
Kwa maelezo yako tu nimeona umeleta/umeeleza ukweli si story ya kutunga..............

Huyo jamaa hakupendi kabisa na alikuwa anakutafutia sababu ili akuache ndo maana
alikuwa anakupekua pekue apate pa kushika na ameona wewe unampenda
na kumuheshimu ndo maana akakutenda .........Usirudiane nae kabisa sababu
atakutenda zaidi akuletee mwanamke ndani ya nyumba.....................

Kuwa na siku njema asikuumize kichwa wanaume hakuna wa tofauti wanafanana tabia

hapana desi, huyu jamaa ana wivu wa kupindukia....nahisi ana inferiority complex ya kitu flan!!
Saita Ama!
 
Dada changanya akili, chuja kila sentensi, tulia tafakali halafu muombe mungu ndio ufanye maamuzi, usiwe na haraka katika kufanya maamuzi, jubu utalalojipa litakuwa na uhakika
 
Mimi kawaida yangu huwa hata sina muda wa kufikiria kwamba mwenzangu huwa ananisaliti, namwamini kwamba kwa kuwa anajua yeye ni mke wangu basi atakuwa wangu peke yangu akiamua kunisaliti hiyo ni juu yake. Lakini kamwe sitapoteza amani yangu kuanza kupekua simu sijui pochi, sijui katumiwa msg gani na nani? huo utoto siwezi kufanya.
Niwape true stori mimi na wife tumebalishana handsets sasa juzi nimekuta jina la kiume huyo jamaa nikampigia nikiwa namfananisha jamaa ambaye tuliwahi kusoma wote mwenye jina kama lake lakini akesema sio yeye na wala hatoki mkoa wa jamaa yangu, akataja mkoa anaotoka wife ndiyo nikmtajia kwamba nimeoa mkoa huo, nikamuuliza eneo analotoka ikaonekana ni kulekule anakotoka wife, kutaja kijiji akasema yeye anatoka kijiji cha jirani na cha wife. Mwisho nikamuuliza kuhusu mke wangu akasema anamfahamu na walisoma wote shule ya msingi. Akanitajia baba yake na ndugu zake wengi. Tukacheka sana na kufurahi kama mtu na shemeji yake. Niliporudi nyumbani nikamweleza wife katika hali ya kawaida tu na yeye akaniambia hivyo hivyo kwamba walisoma wote na ikaishia hapo. Na mpaka sasa sijawahi wala sina wazo lolote baya kuhusiana na huyo kaka. Na mara nyingi tumekutana na wanaume ambao wanafahamiana na wife tunatambulishana na kufurahiana tu, vivyo hivyo kwa upande wangu tukikutana na wadada ninaofahamiana nao wala hakuna anayepoteza muda kumfuatilia mwenzake. Hiyo yote ni kwa sababu tunaaminiana BASI, na tunaishi ndoa ya furaha sana tu na Mungu anazidi kutubariki sana.
 
Pole sana kwa maisha yasio na kuaminika, Ni Maisha magumu sana

Mtegemee Mungu ktk yote Yeye atakufanikisha

Mume/Mke mwema Hutoka Kwa Bwana TU
 
kwa kweli dada yetu mumeo ana wivu uliopitiliza...je hajui kuwa wewe nawe una marafiki?sikatai kuhoji ni nan kakupigia simu nk, bt muhimu ni kulinda heshima ya unayemuuliza au anadhan wewe huongei na watu? ana mapungufu gan mumeo?naamin hiyo anayotumia ni defense mechanism ya jambo fulani...sasa kama walijua hilo jambo then tuanzie hapo..
I mean kwanza mueleweshe akuelewe kuwa wewe umempenda yeye kama alivo na ndio maana umeolewa naye..hakikisha unamthibitishia hilo vizuri.
kisha dai uhuru wako, na katika hili kuwa extra serious, maana nina hofu kama kaanza huku mwishowe usijeshangaa ukiambiwa hakuna kufanya kazi au kwenda hata kwenu. usikubali ndoa yako ivunjike kiurahisi, lakin ili ndoa yako idumu lazima na wewe uwe wazi na akuelewe...he has to understand women needs to be loved na sio used.
pole sana dada. Mungu akuongoze katika hilo.

Asante sana kamanda ubarikiwe mno kwa ushauri wako
 
Kwa maelezo yako tu nimeona umeleta/umeeleza ukweli si story ya kutunga..............

Huyo jamaa hakupendi kabisa na alikuwa anakutafutia sababu ili akuache ndo maana
alikuwa anakupekua pekue apate pa kushika na ameona wewe unampenda
na kumuheshimu ndo maana akakutenda .........Usirudiane nae kabisa sababu
atakutenda zaidi akuletee mwanamke ndani ya nyumba.....................

Kuwa na siku njema asikuumize kichwa wanaume hakuna wa tofauti wanafanana tabia

i beg to differ,kila binadamu ana tabia zake wala sio wote wako hivyo,haijalishi ndoa zinavunjika lakini haimaanishi hakuna ndoa zenye furaha,hawa wanaume ni waume zetu,baba zetu na ni watoto wetu pia so kugenerelize kuwa wanaume ni wabaya au wanawake ni wabaya kwa sasbabu tumetendewa ubaya na mwanaume mmoja nini mmoja hata wawe sita,mimi bado naamini katika mtu binafsi kwenye maamuzi yake!haya ya wanaume/wanawake wote ni sawa yanatuharibia kweli mahusiano/ndoa bila kujijua!NIHUKUMU KWA MAKOSA YANGU SIO MAKOSA YA MWANAMKE MWENZANGU nd the vice versa is true!
 
Back
Top Bottom