Hamisi Damumbaya hafai kuwa Mlimani TV

Paul Kijoka

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
1,399
255
Ndugu zangu wanajamvi, kwanza kabisa naomba mnifahamishe CV ya huyu bwana maana nina wasiwasi na jinsi anavyofanya kazi zake. Pili nadhani ni vyema tukapa uchunguzi huru wa jinsi alivyotoka RFA na StarTV hadi Mlimani TV. Amekuwa akikidhalilisha chombo hiki cha wasomi hasa linapokuja suala la mahojiano na Vigogo wa CCM huku akijifanya yeye ndo anajibu hoja ama kuuliza maswali na kukemea au kukata simu kwa wale wenye mtazamo tofauti na vigogo hao.

Nina mifano miwili ya kwanini kiraza huyu afukuzwe kwenye TV ya wasomi,

Hivi karibuni alikuwa na akihojiana na Vijana wa vyama vya siasa CUF (alijitambulisha kama mwanasheria aliyehitimu UDSM), CHADEMA (mwanafunzi UDSM) na CCM (katibu toka harusha) na akaonesha weakness kubwa kwa kutoa muda mchache kwa kijana kutoka CHADEMA na kujaribu kumwingilia kila alipojitahidi kujenga hoja.

Week iliyopita alikuwa na Nape Nnauye kwenye kipindi ambacho sikutaka ata kujua jina lake. Mbali na kumsifia sana Damumbaya (nikosolewe kama nimekosea jina lake) alionekana wazi akiwa mwoga, mwenye mihemuko ya utii wa kipuuzi na kibaya zaidi alikuwa akijibu hoja za wapiga simu na kujidhalilisha. alikatia watu simu yaani nina hasira sana.......

Tumjadili.
 
Si mtizamaji wa hiyo TV, lakini kwa maelezo yako kama ndivyo ilivokuwa huyo hafai kabisa kuendesha kipindi cha aina hiyo.
 
Kujadili Wajinga wajinga kama hao humu Jamvini ni kuwapandisha chati tu wasizonazo. Huyo ni mmoja wa Vibaraka waliotumwa na Nape. Amevaa Chu pi kichwani lakini hajijui kama watu wanamwonaje.
 
Mi' sidhani kama Damumbaya anapaswa kufukuzwa pale Mlimani TV kwa kuwa
hata hiyo TV station yenyewe haiendi kama slogan yao isemavyo: "Elimu Kwanza",
yaani ni sawa na mchafukoge mtupu.

Ilipoanzishwa nilitarajia TV ya wasomi ingekuwa mfano kwa TV zingine lakini imekuwa
tofauti kabisa, wanaiga hadi pumba na kuziweka kwenye TV yao. This is SHAME!
 
Mimi naangaliaga Mlimani TV. Ni kweli observation zako ni sahihi kwa upande huo nadhani kwa CCM. Lakini pia ni kweli ana uwezo fulani kwenye mada au vpindi ambavyo anaviwasilisha vizuri.

Naomba tumpime kwa mizani sawa siyo kwa tukio moja au yanayohusu uhusiano wake na CCM tu. Ni mwanadamu ana haki zake na mapungufu yake
 
Tayari umetoa hukumu juu yake kwa mtazamo wako...nakushauri upeleke malalamiko yako kwa waajiri wake ili waweze chukua hatua.
Vinginevyo jitahidi kuvumilia tu kwani si kila ataishi kwa namna itakayokuridhisha wewe.
 
Nilikitizama hicho kipindi alipokuwa amem-host Nape, uko sahihi kwa tathmini yako lakini ni vizuri ukajua akiwa kama mwanahabari ni lazima alinde hadhi ya kipindi chake anachokiongoza na si kutoa nafasi kwa watukana matusi kupiga simu na kuwekwa hewani. Zipo sehemu alizochemsha siku hiyo lakini mara yingi sana amekuwa ni mtangazajia anayefanya ufurahie baadhi ya vipindi anavyoviongoza:A S 100:
 
Ukitaka usiumize kichwa pendelea kuangalia Straight talk Africa ( VOA ) na Hard Talk ( BBC ) hizo station za kidaku mnajitafutia wenyewe shida, hivi hujui kama Steve Nyerere na Zembwela ( comedians ) nao ni watangazaji?
 
Si mtizamaji wa hiyo TV, lakini kwa maelezo yako kama ndivyo ilivokuwa huyo hafai kabisa kuendesha kipindi cha aina hiyo.

Mkuu, watu hawa ni hatari sana. Sisi peke yetu hatuwezi kubadirisha na kukomboa umma wa waTz. Hawa wanasikika kila siku redioni na TV wakijifanya kujua kila kitu na kuzidi kuupoteza umma.
 
Kujadili Wajinga wajinga kama hao humu Jamvini ni kuwapandisha chati tu wasizonazo. Huyo ni mmoja wa Vibaraka waliotumwa na Nape. Amevaa Chu pi kichwani lakini hajijui kama watu wanamwonaje.

Ni kweli mkuu. Ni vyema ujue wajinga kama hawa ndo wenye nafasi kubwa nchini mwetu. Ndo kesho utasikia ni viongozi na wamepewa ridhaa na viongozi ili kuendelea kutengeneza watanzania kuwa KISUKULE kabisa.
 
Mi' sidhani kama Damumbaya anapaswa kufukuzwa pale Mlimani TV kwa kuwa
hata hiyo TV station yenyewe haiendi kama slogan yao isemavyo: "Elimu Kwanza",
yaani ni sawa na mchafukoge mtupu.

Ilipoanzishwa nilitarajia TV ya wasomi ingekuwa mfano kwa TV zingine lakini imekuwa
tofauti kabisa, wanaiga hadi pumba na kuziweka kwenye TV yao. This is SHAME!

Hii ni aibu kwa taifa. Ni ujinga wa kutisha. Lakini ngoja tuwakumbushe kina Mkandara na watu wao kuwa siku zao za kuandaa wasomi misukule zinakaribia mwisho
 
kwa taarifa za ndani ya cuf ni kuwa yule ni kijana wao ndio maana wanaopewa ukaribisho ktk vipindi vyake ni cuf mara nyingi sana kuliko CDM kwa hiyo hata magamba anawaita tu kwa kuwa ki-tv chenyewe ni cha udsm ambapo ni serikali kwa upende mwingine
 
Lakini jamani siyo kweli kwamba samaki mmoja kioza basi eti wote wameoza, japo kuna wengine hapo Mlimani TV lakini siyo kwamba nao ni kama huyo mnayemlalamikia, mwacheni afe kivyake, na wengine wasafi wanaopeperusha bendera ya Mlimani Tv vizuri tuendelee kuwapongeza ili kuwapa moyo wa kuzidi kututumikia Watz, vinginevyo na huyo sijui ndiyo Damumbaya ajifunze na kubadilika kutokana na udhaifu wake huo, na pale aliposema katika bunge la katiba kuwa vyombo vya habari vidhibitiwe kurusha mijadala ya katiba mpya, kama vipi avue gamba!
 
Kama ndiye aliyetoa wazo hill huyo hafai kuwa mwanahabari hata kidogo.
 
Lakini jamani siyo kweli kwamba samaki mmoja kioza basi eti wote wameoza, japo kuna wengine hapo Mlimani TV lakini siyo kwamba nao ni kama huyo mnayemlalamikia, mwacheni afe kivyake, na wengine wasafi wanaopeperusha bendera ya Mlimani Tv vizuri tuendelee kuwapongeza ili kuwapa moyo wa kuzidi kututumikia Watz, vinginevyo na huyo sijui ndiyo Damumbaya ajifunze na kubadilika kutokana na udhaifu wake huo, na pale aliposema katika bunge la katiba kuwa vyombo vya habari vidhibitiwe kurusha mijadala ya katiba mpya, kama vipi avue gamba!

Hatufai kabisa,mlimani ebu mrudisheni chumba cha muziki
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom