Hamas wanaweza kutengeneza rocket Je Tanzania tunatengeneza silaha?

Sidhani kama kuna umuhimu sana wa sisi kujitengenezea silaha.Kama viwanda vya kutengeneza bidhaa muhimu,mashirika kama ATCL,TRL etc yanafikia hali yaliyonayo then ipo wazi kuwa bado tuna maeneo mengi tunayopaswa kuyapa kipaumbele kabla hatujafikia kwenye hilo la kutengeneza silaha.
BTW;
Ushawahi kusikia zile "bunduki pori" zilizokuwa zikitengenezwa maeneo ya Mbozi-Mbeya???Wale waliokamatwa kwenye msako wa kutafta watengenezaji nadhani still wapo gerezani,na zana zao za kutengenezea possibly zitakuwa zilishakuwa destroyed.
 
Rocket za Hamas aim yake ya kubahatisha, na sisi hatupo kwenye conflict na mtu yoyote so itakua ni kupoteza resources tu.
 
Au silaha zote tunanunua?
Naomba habari kwa mnaojua!

Zamani sana tulikuwa na kiwanda cha kutengeneza silaha ndogo ndogo za kijeshi pale Morogoro kikijulikana kama Mzinga Corporation; mara ya mwisho nilikisikia mwaka 1989. Sijui kama bado kipo hadi leo.
 
Zamani sana tulikuwa na kiwanda cha kutengeneza silaha ndogo ndogo za kijesi pale Morogoro kikijulikana kama Mzinga Corporation; mara ya mwisho nilikisikia mwaka 1989. Sijui kama bado kipo hadi leo.

Mkuu Kichuguu, heshima yako. Mzinga Corporation bado ipo and going stronger. Silaha ndogondogo zikiwemo risasi zinatengenezwa pale. Nilisikia wakati fulani kuwa kuna wasiwasi wa usalama wa maji kwa jiji la Morogoro maana mto mzinga unamwaga maji kwenye ziwa Mindu a.k.a bahari ya Morogoro waliochimbiwa na Nyerere. Inasemekana kuwa mto mzinga una asilimia kubwa ya mabaki ya mercury yatumikayo kwenye utengenezaji wa silaha hizo. Mabaki hayo yanamwagwa mto mzinga. Sijui suala hilo lilifuatiliwa vipi na wahusika. Anayejua zaidi atupe mwanga.
 
Tanzania tunatengeneza silaha zile za asili kama pinde, mishale, mikuki, podo, marungu, ngao, sime, shoka,mapanga, Magobole etc etc sidhani kama tunaagiza nje hizi!!! Lakini tukija kwenye misiles na biological weapons tunategemea kununua kwa rafiki zetu wa nje ie China, USSR, US, Canada etc etc
 
Au silaha zote tunanunua?
Naomba habari kwa mnaojua!

Kutengeneza silaha ni muhimu sana kwa taifa lolote.Suala si kutengeneza tu lakini kuna R&D(Research and Development)-hapa ndio faida ya kutengeneza silaha inapatikana.
Viwanda vingi vinavyotengeneza silaha ni vya kiraia hivyo kuna ajira.Matokeo ya R&D mara zote yanaishia katika matumizi ya kiraia.
Hebu fikiria simu za mikononi zimekuwepokwa zaidi ya miaka 40 hasa kwa nchi zilizoendelea.Ilikuwa technologia ya kijeshi tu hapo nyuma.
Missile technology imeweza kupeleka satellites angani ambazo kwa sasa zinatumika kwa mawasiliano.
Pamoja na utengenezaji wa silaha pale Mzinga , wahusika tunaomba watueleze ule mpango wa kutengeneza an All- Weather- Vehicle kwa Tanzanian specifications ,pale Kibaha uliishia wapi.
Utengenezaji wa silaha ulio endelevu unaweza kuleta mafanikio ya kiraia yenye manufaa kwa jamii.
 
Back
Top Bottom